Majambazi wamemuua rafiki yangu kikatili sana. Imeniuma mno

Kwanini wamemkata mapanga huyo baraka na kumpora.halafu kaachwa huyo rafiki yake kaumia kidogo tu na karususiwa kutoka hospital?

Umejiuliza hili?
 
Pole dalali,, rafiki yako apumzike kwa amani.
Nakupa tip.
Kama unataka kujua kuwa ni na kulipiza kisasi ,, marehemu akishaoshwa pale unapomuangalia na kumuoga kwa mara ya mwisho.
Chukua fimbo ndogo iwe mbichi mchape huku unamuuliza amekufanye na waliomfanyia ni nani??? Unamchapa kidogo tu huku unamwambia ahakikishe analipa kisasi akimaliza kulipa kisasi alale atulie...... Mkishazika majibu utaleta hapa.
Hahaha mambo mengine bn ,sasa ndugu wakuruhusu uchape maiti yao au unatafuta kipigo au kuitwa mwanga??
 
Kwakweli hawatamruhusu labda awaelezee vizuri wamuelewe vizuri sana tofaut na hapo ni hakuna. unajua kila kabila Wana Imani zao na kila familia Zina imani zao.
 
Habari za usiku wakuu bila shaka, mupo salama.

Leo imekuwa siku mbaya sana kwangu baada ya kupokea taarifa za kifo cha rafiki yangu, gERVASS maarufu kama Baraka. Alikuwa anaishi maeneo ya Malamba Mawili, sehemu inaitwa Bwawani. Ni mitaa ambayo niliwahi kuishi pia. Baraka alihamia huko tangu mwaka 2022 na akaanza biashara yake ya duka la mangi. Biashara ilimwendea vizuri sana hadi akanunua pikipiki yake mpya mwezi mmoja uliopita.

Hivi majuzi alisafiri na pikipiki yake pamoja na rafiki yake anayeitwa Macho. Walianza safari kutoka Dar kwenda Rombo. Safari ilikuwa inaendelea vizuri hadi walipoingia Mkoa wa Kilimanjaro usiku wa manane. Kumbe njiani kulikuwa na sehemu majambazi waliweka waya barabarani. Inasemekana walikuwa kwenye mwendo wa kasi, wakakunasa kwenye huo waya na kuanguka vibaya sana. Helmet yake ilipasuka na kichwa kikapata majeraha makubwa pamoja na sehemu nyingine za mwili.

Bila huruma, majambazi wakamshambulia kwa mapanga kisha wakachukua pikipiki yake na begi lake ambalo lilikuwa na kadi ya pikipiki, fedha na vitu vingine kadhaa.

Aliwahishwa katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Madaktari walijitahidi kupambana kuokoa maisha yake, lakini usiku wa kuamkia leo alifariki dunia.

Taarifa hii imeniumiza sana, hasa ukizingatia kuwa mwaka juzi alioa na tayari ana mtoto mdogo wa takriban miaka miwili. Leo nilipopita kumuona mke wake, nimejikuta nikiishiwa nguvu. Ni binti mdogo sana, hata miaka 25 hajafikisha, sasa anaenda kubeba jukumu la kulea familia peke yake akiwa mjane.

Baraka alikuwa na ndoto kubwa sana maishani. Ndoto zake zimekatishwa kikatili na watu wenye tamaa ya mali ambayo hawakuitafuta kwa jasho lao.

Nitaenda Rombo kumzika rafiki yangu Baraka. Nitaenda hadi Useri kuomboleza pamoja na familia yake. Nimeambiwa Macho hakupata majeraha makubwa, aliumia kidogo tu na tayari ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Majambazi nawachukia sana. Mmeua kijana mdogo mwenye ndoto zake. Bora hata mngemchukulia pikipiki, lakini uhai wake mkamuachia.
Pikipiki si chombo cha kusafiria usiku, usalama wake ni mdogo sana.

Hatari kama hizo za kuwindwa kama mnyama, wanyama wakali, hitilafu za kiufundi za chombo nk nk.

Ukiona usiku unaelekea kuanza, jisalimeshe 'senta' yoyote ulale, udamkie mwendelezo.

Fundisho kwa vijana na watumiaji wengine wa vyombo hivyo vya usafiri.

Pole yake na pole kwa familia.

Apumzike kwa amani.
 
Habari za usiku wakuu bila shaka, mupo salama.

Leo imekuwa siku mbaya sana kwangu baada ya kupokea taarifa za kifo cha rafiki yangu, gERVASS maarufu kama Baraka. Alikuwa anaishi maeneo ya Malamba Mawili, sehemu inaitwa Bwawani. Ni mitaa ambayo niliwahi kuishi pia. Baraka alihamia huko tangu mwaka 2022 na akaanza biashara yake ya duka la mangi. Biashara ilimwendea vizuri sana hadi akanunua pikipiki yake mpya mwezi mmoja uliopita.

Hivi majuzi alisafiri na pikipiki yake pamoja na rafiki yake anayeitwa Macho. Walianza safari kutoka Dar kwenda Rombo. Safari ilikuwa inaendelea vizuri hadi walipoingia Mkoa wa Kilimanjaro usiku wa manane. Kumbe njiani kulikuwa na sehemu majambazi waliweka waya barabarani. Inasemekana walikuwa kwenye mwendo wa kasi, wakakunasa kwenye huo waya na kuanguka vibaya sana. Helmet yake ilipasuka na kichwa kikapata majeraha makubwa pamoja na sehemu nyingine za mwili.

Bila huruma, majambazi wakamshambulia kwa mapanga kisha wakachukua pikipiki yake na begi lake ambalo lilikuwa na kadi ya pikipiki, fedha na vitu vingine kadhaa.

Aliwahishwa katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Madaktari walijitahidi kupambana kuokoa maisha yake, lakini usiku wa kuamkia leo alifariki dunia.

Taarifa hii imeniumiza sana, hasa ukizingatia kuwa mwaka juzi alioa na tayari ana mtoto mdogo wa takriban miaka miwili. Leo nilipopita kumuona mke wake, nimejikuta nikiishiwa nguvu. Ni binti mdogo sana, hata miaka 25 hajafikisha, sasa anaenda kubeba jukumu la kulea familia peke yake akiwa mjane.

Baraka alikuwa na ndoto kubwa sana maishani. Ndoto zake zimekatishwa kikatili na watu wenye tamaa ya mali ambayo hawakuitafuta kwa jasho lao.

Nitaenda Rombo kumzika rafiki yangu Baraka. Nitaenda hadi Useri kuomboleza pamoja na familia yake. Nimeambiwa Macho hakupata majeraha makubwa, aliumia kidogo tu na tayari ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Majambazi nawachukia sana. Mmeua kijana mdogo mwenye ndoto zake. Bora hata mngemchukulia pikipiki, lakini uhai wake mkamuachia.
Na yeye ali'risk' sana. Kulikuwa na haja ya kutoka Dar-Kilimanjaro kwa pikipiki?
 
Mbona kama Macho kacheza huu mchezo,kua huo waya ulikua unasubiri PIKIPIKI yao tu?
Kua hio njia vyombo vingine vya usafiri havipiti?
Kua huo waya specific ulikua wa kunasa PIKIPIKI ya baraka tu?
Hapana, hawa wanafunga wire unalala barabani pande zote mbili, mmoja anakuwa mbali kidogo. Sasa yule ndio anatoa taarifa kwa wenzie nyanyua wire wanakuja wanafunga juu upande wa pili. Wakimaliza wanashusha tena.

Huu uwizi wa namna hii wakati pikipiki za kichina zinashamiri waliwahi kutumia hata jangwani dar es salaam usiku wa manane.

Pole kwa wafiwa, lkn wanaohusisha hili jambo na huyo aliyepakiwa kwangu mimi siafikiani nao labda kama tukio hilo lingetokea dar.

Yani mtu awe na risk ya kupanda pikipiki kutoka dar avuke mikoa miwili kwenda kupora pikipiki kilimanjaro ambayo wakigawana hela haizidi laki tano.
 
Pole dalali,, rafiki yako apumzike kwa amani.
Nakupa tip.
Kama unataka kujua kuwa ni na kulipiza kisasi ,, marehemu akishaoshwa pale unapomuangalia na kumuoga kwa mara ya mwisho.
Chukua fimbo ndogo iwe mbichi mchape huku unamuuliza amekufanye na waliomfanyia ni nani??? Unamchapa kidogo tu huku unamwambia ahakikishe analipa kisasi akimaliza kulipa kisasi alale atulie...... Mkishazika majibu utaleta hapa.
Mental health is real
 
Aah basi ni dili la Macho
Macho ntuu wa Dili😭Yaani Majambawazi wawavamie mmoja afe mwingine kaachwa bila kichapo wala kuchukuliwa kitu! Uenda alikuwa anawasiliana na hao majambawazi njia nzima. Inaonekana Marehemu alikuwa na pesa kiasi na hii pia ikawa sababu. Macho ni suspect no 1 RIP Baraka
 
Back
Top Bottom