babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 16,476
- 21,202
Mshua alikua anachapa nusu saa tu tuko mpakani Malawi huko toka Mbeya mjini.Two Hours kwa barabara hizi hizi kweli?
Mshua alikua anachapa nusu saa tu tuko mpakani Malawi huko toka Mbeya mjini.Two Hours kwa barabara hizi hizi kweli?
sema usafiri wa Pikpiki ni usafiri hatari huenda kuliko usafiri mwingine wa aina yoyoteMshua alikua anachapa nusu saa tu tuko mpakani Malawi huko toka Mbeya mjini.
Mimi natoka mafinga kwenda rungwe mbeya kila wiki nishazoeaDuh Nchi hii unasafiri usiku na pikipiki
Umejuaje ni wachaga? Wanaofaa ni vibaka wa kabila gani?Hawa vibaka wa kichaga hawafai kabs
Oya hapa mboni km kuna harufu fulani inasikika ikiangazia upande huu, sijaelewa vizuriNimeambiwa Macho hakupata majeraha makubwa, aliumia kidogo tu na tayari ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Halafu fresh nyinyi hamuwekewi waya?Mshua alikua anachapa nusu saa tu tuko mpakani Malawi huko toka Mbeya mjini.
Na Mbaya Zaidi,,Uraibu Wa Mastimu Kupita Kiasi,,Huondoa Utashi Na Kuivuruga Akili Haswa...Vibaka wengi ni waraibu wa bangi na mapomhe makali
KABISANa Mbaya Zaidi,,Uraibu Wa Mastimu Kupita Kiasi,,Huondoa Utashi Na Kuivuruga Akili Haswa...
Nimenusa kitu pia hii mpaka uwe intelligence makini ndio unaweza kuelewa hivi hivi ni rahisi sana kuaminiMbona kama Macho kacheza huu mchezo,kua huo waya ulikua unasubiri PIKIPIKI yao tu?
Kua hio njia vyombo vingine vya usafiri havipiti?
Kua huo waya specific ulikua wa kunasa PIKIPIKI ya baraka tu?
Pikipiki yenyewe anaenda iuza 300,000 tu hmn llloteHawa mbwa wanakuibia halafu wanakuua, nimeanza kuelewa kwanini wakishikwa ni kifo tuu
Kwa hio unataka kusema walikua wamepiga vitu gani huku wanaendesha?Na Mbaya Zaidi,,Uraibu Wa Mastimu Kupita Kiasi,,Huondoa Utashi Na Kuivuruga Akili Haswa...
Miaka ya 80 waya utoke wapi?Halafu fresh nyinyi hamuwekewi waya?
Unikaribishe wakati huo naweza kuwa msaada ,ila kaa ujue hata mkimuelewa ila yeye ndiye mshukiwa namba moja na itoshe mimi kusema hakuna asichoelewa kuhusu mauaji ya huyo mtotoHapo sijajua nikienda msibani nitajua mengi sana mana yote haya ni yale nimepata Huku dsm na ajali imetokea Kilimanjaro. Huyo rafiki yake inabidi baada ya amzishi nikae naye sehemu nimpe Bia kadhaa huku nikimdadisi
Issue ya kadi ni mambo ya usalama wa barabarani na chombo chenyewe ikiwa qtasimamishwa au kutokea sintofahamu ya kiusalama ,simlaumu kutembea nayo ila namponhezq kwa kujitambuayanafikirisha sana mkuu sijajua lengo lake ilikuwa ni nini
Huyo hata asinge safiri wangemsondeka tu.Hapo umeongea,
Honda Paris-Dakar hapo kwenda Kili ni Masaa mawili tu imefika toka Dar.
Pikipiki inaitwa Boxer,Tvs,yoshugi, hyangui,shingsho michina na unapiga nayo long trip huogopi.
Kawahishwa tu hata asingeweza kurudi nayo
Rafiki yake Macho ndio Jambazi, mbaficha nini story ilivyojieleza ipo wazihapo majambazi walimuuaje?
Pole, Pikipiki ilikuwa aina gani?Habari za usiku wakuu bila shaka, mupo salama.
Leo imekuwa siku mbaya sana kwangu baada ya kupokea taarifa za kifo cha rafiki yangu, gERVASS maarufu kama Baraka. Alikuwa anaishi maeneo ya Malamba Mawili, sehemu inaitwa Bwawani. Ni mitaa ambayo niliwahi kuishi pia. Baraka alihamia huko tangu mwaka 2022 na akaanza biashara yake ya duka la mangi. Biashara ilimwendea vizuri sana hadi akanunua pikipiki yake mpya mwezi mmoja uliopita.
Hivi majuzi alisafiri na pikipiki yake pamoja na rafiki yake anayeitwa Macho. Walianza safari kutoka Dar kwenda Rombo. Safari ilikuwa inaendelea vizuri hadi walipoingia Mkoa wa Kilimanjaro usiku wa manane. Kumbe njiani kulikuwa na sehemu majambazi waliweka waya barabarani. Inasemekana walikuwa kwenye mwendo wa kasi, wakakunasa kwenye huo waya na kuanguka vibaya sana. Helmet yake ilipasuka na kichwa kikapata majeraha makubwa pamoja na sehemu nyingine za mwili.
Bila huruma, majambazi wakamshambulia kwa mapanga kisha wakachukua pikipiki yake na begi lake ambalo lilikuwa na kadi ya pikipiki, fedha na vitu vingine kadhaa.
Aliwahishwa katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Madaktari walijitahidi kupambana kuokoa maisha yake, lakini usiku wa kuamkia leo alifariki dunia.
Taarifa hii imeniumiza sana, hasa ukizingatia kuwa mwaka juzi alioa na tayari ana mtoto mdogo wa takriban miaka miwili. Leo nilipopita kumuona mke wake, nimejikuta nikiishiwa nguvu. Ni binti mdogo sana, hata miaka 25 hajafikisha, sasa anaenda kubeba jukumu la kulea familia peke yake akiwa mjane.
Baraka alikuwa na ndoto kubwa sana maishani. Ndoto zake zimekatishwa kikatili na watu wenye tamaa ya mali ambayo hawakuitafuta kwa jasho lao.
Nitaenda Rombo kumzika rafiki yangu Baraka. Nitaenda hadi Useri kuomboleza pamoja na familia yake. Nimeambiwa Macho hakupata majeraha makubwa, aliumia kidogo tu na tayari ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Majambazi nawachukia sana. Mmeua kijana mdogo mwenye ndoto zake. Bora hata mngemchukulia pikipiki, lakini uhai wake mkamuachia.
Wewe unayo hiyo pikipiki kazi mdomo tuPole , hao ni vibaka hakuna jambaz anapoteza mda kuiba vitu kama pikipiki.