Majambazi wamemuua rafiki yangu kikatili sana. Imeniuma mno

Habari za usiku wakuu bila shaka, mupo salama.

Leo imekuwa siku mbaya sana kwangu baada ya kupokea taarifa za kifo cha rafiki yangu, gERVASS maarufu kama Baraka. Alikuwa anaishi maeneo ya Malamba Mawili, sehemu inaitwa Bwawani. Ni mitaa ambayo niliwahi kuishi pia. Baraka alihamia huko tangu mwaka 2022 na akaanza biashara yake ya duka la mangi. Biashara ilimwendea vizuri sana hadi akanunua pikipiki yake mpya mwezi mmoja uliopita.

Hivi majuzi alisafiri na pikipiki yake pamoja na rafiki yake anayeitwa Macho. Walianza safari kutoka Dar kwenda Rombo. Safari ilikuwa inaendelea vizuri hadi walipoingia Mkoa wa Kilimanjaro usiku wa manane. Kumbe njiani kulikuwa na sehemu majambazi waliweka waya barabarani. Inasemekana walikuwa kwenye mwendo wa kasi, wakakunasa kwenye huo waya na kuanguka vibaya sana. Helmet yake ilipasuka na kichwa kikapata majeraha makubwa pamoja na sehemu nyingine za mwili.

Bila huruma, majambazi wakamshambulia kwa mapanga kisha wakachukua pikipiki yake na begi lake ambalo lilikuwa na kadi ya pikipiki, fedha na vitu vingine kadhaa.

Aliwahishwa katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Madaktari walijitahidi kupambana kuokoa maisha yake, lakini usiku wa kuamkia leo alifariki dunia.

Taarifa hii imeniumiza sana, hasa ukizingatia kuwa mwaka juzi alioa na tayari ana mtoto mdogo wa takriban miaka miwili. Leo nilipopita kumuona mke wake, nimejikuta nikiishiwa nguvu. Ni binti mdogo sana, hata miaka 25 hajafikisha, sasa anaenda kubeba jukumu la kulea familia peke yake akiwa mjane.

Baraka alikuwa na ndoto kubwa sana maishani. Ndoto zake zimekatishwa kikatili na watu wenye tamaa ya mali ambayo hawakuitafuta kwa jasho lao.

Nitaenda Rombo kumzika rafiki yangu Baraka. Nitaenda hadi Useri kuomboleza pamoja na familia yake. Nimeambiwa Macho hakupata majeraha makubwa, aliumia kidogo tu na tayari ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Majambazi nawachukia sana. Mmeua kijana mdogo mwenye ndoto zake. Bora hata mngemchukulia pikipiki, lakini uhai wake mkamuachia.

Inawezekana katika watu wa karibu alioowaambia Mipango yake Huko kwao Kilimanjaro ndo wamem time, sio rahisi sana haya mambo ya wire bila Malengo
 
Halafu unakuta kuna mjinga akiona mnataka kumuua mwizi au jambazi anajifanya ana huruma sana heti msimuue mpelekeni polisi,kama vile yeye ataenda kutoa ushaidi mahakamani....

Hao washenzi ni wakuua tu na wao.
 
Kabisa tena auawe kwa amteso makali ajutie makosa yake na iwe mfano kwa wana tasnia wenzake
 
Pole dalali,, rafiki yako apumzike kwa amani.
Nakupa tip.
Kama unataka kujua kuwa ni na kulipiza kisasi ,, marehemu akishaoshwa pale unapomuangalia na kumuoga kwa mara ya mwisho.
Chukua fimbo ndogo iwe mbichi mchape huku unamuuliza amekufanye na waliomfanyia ni nani??? Unamchapa kidogo tu huku unamwambia ahakikishe analipa kisasi akimaliza kulipa kisasi alale atulie...... Mkishazika majibu utaleta hapa.
 
1)Kwanini marehemu alitembea na kadi ya pikipiki
2)hilo eneo lina historia ya matukio hayo au ndo limetokea tu kwa marehemu
3)kwanini wampige mapanga marehemu peke yake
Safari ndefu hivyo kadi ni Muhimu kw usalama wake ikiwa itahitajika, Historia kwa mujibu wa wadau kuna historia swala la kwanini wampige marehemu mapanga peke yake sijajua kabisa
 
Pole dalali,, urafiki yako apumzike kwa amani.
Nakupa tip.
Kama unataka kujua kuwa ni na kulipiza kisasi ,, marehemu akishaoshwa pale unapomuangalia na kumuoga kwa mara ya mwisho.
Chukua fimbo ndogo iwe mbichi mchape huku unamuuliza amekufanye na waliomfanyia ni nani??? Unamchapa kidogo tu huku unamwambia ahakikishe analipa kisasi akimaliza kulipa kisasi alale atulie...... Mkishazika majibu utaleta hapa.
Shukran sana
 
Pole kwa wafiwa.

Na mini nilikuwa najiuliza hivihivi, nikafikiri labda ni mimi tu.
Huyu unakuta wamemchukua pengine ana mda ajaenda kwao alafu anataka kwenda na pikpik shehee kwa wachaga hata msata hufiki..mizmu lazima ipite na wewe kwa njia yoyote
 
Hapa ndo huwa siyaelewi mavibaka ya Tanganyika, hayana akili, hapo yakiulizwa baada ya kuanguka kwanini hamkuchukua pikipiki mkaondoka badala yake mkamkata mapanga unaweza usiamini yatakachojibu kama ni akili ya binadamu au mnyama.
Itakuwa marehemu alibisha na kujaribu kupambana nao.
 
Back
Top Bottom