Mabulangati
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 796
- 167
Nashauri kuwa chuo kikuu chochote si sekondari, hivyo tunapoenda vyuoni tusijione sisi ni wajuaji kuliko wengine lazima kujitahidi kuwa na heshimna kwa walimu na wanafunzi wenzetu, kusoma kwa bidii, kuwahi madarasani, kujishughulisha na mambo ya kijamii, kujisomea vitabu na si madesa pekee nk. Pili tuache kudhani kuwa kudesa ndiyo kufaulu au niko UDSM au mtoto wa mjini na mambo mengine kama hayo ya kishamba.
Pili pale mwalimu anazingua mripoti haraka sana kwa head, principal/dean, DVCs au VC au zaidi ya hapo ili kupata haki yako ya msingi. Leo nimepita pale UDSM nikakuta jamaa analia kumuuliza kunanini akasema anatafakari namna atakavyojitetea kwenye seneti maana an kesi ya kujibu baada ya kukutwa anaibia kwenye mtihani. nafasi za kujitetea zipo hivyo tuzitumie vyema. Lazima tujiulize kwanini kati ya wanafunzi 1000 darasani wanafeli 30 tu kwanini isiwe wote 1000 au nusu!! Ni kweli walimu wengine ni shida uzoefu wa kufundisha hawana, wala hawasomi vya kutosha lakini nani atakusema kama sii wewe mwenyewe?