Majanga ya Asili: Tukafanye utafiti kwa Wahadzabe na wanaofanana nao ili tufahamu jinsi wanavyotambua majanga haya kabla hayajatokea?

Namna nyingine hayo makabila yanavyojua ni uelekeo wa upepo na mvua.
Mfano: Upepo na Mvua za Arusha na mikoa ya kaskazini mara nyingi hutokea upande wa Mashariki(Ilipo Bahati ya Hindi na milima mikubwa ya Usambara, Milima ya Upare,Kilimanjaro na Meru)
Lakini kuna miaka au misimu mvua inaweza kuwa ya kutoka pande zote au pande tofauti na Mashariki, kwa waliorithishwa ancient knowledge, lazima wajiulize na kuchukua tahadhari.
Namna nyingine ni unajimu. Wanajua na kuamini unajimu kwa hali ya juu sana. Wanajua mipangilio ya nyota na mwezi zinasema nini.
Let go back to ancient knowledge. Pamoja na elimu hii ya sasa, basi hata ile ya wahenga tusipuuzie.
 
Bwana Pascal swalhumimu ktk mchango wako ambalo ungehitajika kijiuliza kabla..ni hili je tunaweza kuzuia janga kutokea?
TOfairi na je tunaweza kuzuia maafa yasitokee?
Haya ni maswali mawili tofauti na yenye majibu tofauti.
Kinachotugharimu ni kuzuia athari za majanga/maafa yasiwe makubwa katika eneo husika. Jamii yetu iko mbali sana kiuelewa hasa tukipewa tahadhari kabla.
Wengi wetu tunasubiri janga litokee ndo tunaweka mipango ya kukabili hali.
Bado sanaaaaa
 
Mlima HANANG'. Not Mlima KATESH.
Also, Hadzabe na Tindiga ni mtu moja. Ni sawa na Unasema Mbulu na Mwiraqw au Bargaig na Mang'ati au Datooga. Ni Mtu huyo huyo moja.
 
Dah, nipe details zaidi mkuu kuhusu hiyo radi na uokozi wa ng'ombe. Naziheshimu mno radi na juzi zimetoka kupifa mji wetu huu si za kawaida hadi watu na familia zao wakakimbilia chini ya kitanda.
 
Umeanza Vizuri Unakuja Kuharibu mwishoni na Uchawa wako
Magufuli Kahusika nini na Mada Hii
 
Ni maoni yako na lazima yaheshimiwe lakini siwajibiki kukubaliana nayo.
Uwe na siku nzuri.
 
Sawa, wasandawe wawekwe sensor wakianza kukimbia tujue Kuna tetemeko au volcano inakuja,
 
Tv zetu zote zinaendelea kurusha tu vipindi vya kawaida, business as usual kama vile hamna dharura ya kitaifa. Hili janga liwe ni fursa ya kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwepo na maeneo ya hifadhi. Sio kila mahali paruhusiwe kufanyika shughuli za kibinadamu. Athari za mabadiliko ya tabia nchi na athari za kimazingira zinasababishwa na sisi wenyewe kwa zaidi ya asilimia 90. Tusimsingizie Mungu.
 
Tv zetu zote zinaendelea kurusha tu vipindi vya kawaida, business as .
We jamaa,yaani waache vipindi ambavyo vimelipiwa na kudhaminiwa na watu kwa pesa kubwa warushe mafuriko ya katesh!? Anzisha na wew TV channel yako uwe unarusha matukio yakitokea ,urushe kuanzia asubuhi hadi jioni,wamiliki wanaumiza vichwa namna y kulipa wafanyakazi wao ,wewe unasema warushe matukio all over the day!!
 
Kondoo pia ukiona anapanda Hasira na kuanza kwenda huko na huko kichwa kama ana Hasira za kupigana kimbilia haraka eneo la wazi usikae karibu na miti kukiwa na mvua radi muda wowote itapiga eneo Hilo usalama wako kaa eneo wazi Wacha mvua ikutandike usithubutu kukaa chini ya mti
Pia mvua kama kubwa Ina radi epuka kukaa chini ya mti
 
mada nzuri sana

Hanang haijawahi lipuka..uliyolipuka ni Oldonyo Lengai kaskazini mwa mji wa Mto wa Mbu km za kutosha...lilipo ziwa Natron
Wafugaji walihamishwa

Huko wenzako wamebeba mabunduki na buletiprof...wako vitani...nilitegemea zile chopa za mabaka mabaka zingetimba angani na wajiolojia na kuskani mlima ...geological STATAZ ya mlima

Mlima Hanang unamatambiko mazito mazito kweli kweli..na unatisha usiku ukiuangalia kwa mbali haswa ukiwa Magharibi ya mlima...nilipanda 4 years back ni noma jomba....

Wanafunzi wa vyuo huko nje haswa ulaya hupanda huo mlima kila mwaka kama stadi tuwa ....kwao ni eneo muhimu la kujifunza zaidi ya mlima Kilìmatembo

Tukaee na hao Balise wazee chini ya huo mlima tutapata mengi ya Kusisimuwa...

cc mshana @Yercko
 
Hili taifa si limekuwa la wakata mauno

Tu kama drc sshvi

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…