Itapendeza kama umeme hautakuwa wa luku....
Nikija Dar, natumai itakuwa tayari niipande mpaka Kigoma nikumbUKE nostalgia ya reli ya kati miaka ileeeee...una safiri na waranti yaa uanafunzi...
Nipite Morogoro, kutoka Moro mpaka Kilosa ni viunga vya misitu ya Uluguru ya ukijani na ukungu wa kutosha, mara tunaingia Kilosa, hatukai sana tunaitafuta Kongwa, mara Dom hii hapa, nishuke niende Wimpy's nikapate msosi, nirudi na kushushia karanga za kuchemsha, tuitafute Manyoni, sijui yale marashi na sabuni za ulaya walikuwa wanatoa wapi wale wauzaji wa Manyoni, mara Honi ya treni ikilia unaliacha liaanze kuondoka ili ulikimbize na kudandia na ujione VanDamme, hapo tunaitafuta Itigi ni Mandhari ya kutosha huku umechungungulia dirisha maeneo ya mlangoni, na nakumbuka ikifika Tabora, unatakiwa uwe macho juu na mizigo yako maana hapo ni wezi wako juu ya treni inaeenda wananing'inia na kuchomoa mabegi,
aaahh naona hivyo vituo nimechanganya madawa....nitarudi nikiwa sober...