Majeshi yote yana askari na majeshi yote yana Wanajeshi

Kwann anaitwa raia mkakamavu?je kwnn rais upendelea kuvaa combat na c idara zngine za ulinzi?
Ndo ujue kuwa Jeshi ndiyo chombo cha ulinzi kinachowakilisha uimara wa kiulinzi ndani ya taifa lolote ikiwemo Tanzania.

 
Mkuu kama sijakosea umesema mrakibu wa jeshi la polisi, jeshini rank yake ni Chini ya captain
 
Hapana hapo Chini nakupinga sisi tuliopita JKT tunaelewa... Huwez linganisha coarse ya Askari wa polisi na JWTZ[emoji23][emoji23][emoji23]... Mkuu hapo haupo sahihi Askari polisi anaishia kupata mafunzo Machache Sana ya kimedani na utumiaji silaha... Kuna silaha tukizipeleka polisi za kivita watashindwa kabisa kuzitumia..kwene course ya upolisi hufundishwi Sana mafunzo ya kimedani.... Na kaa ukijua hakuna jeshi lenye uweledi kimafunzo, kikamavu, kimkakati, na rasilimali zaidi ya jeshi la ulinzi
 
Kuna silaha ziko jeshi la Us zikiletwa jwtz hamuwezi kuzitumia,,,Je! Tuseme jwtz ni dhaifu kwa kutokujua silaha flani!!?Kwani JKT mlijifunza nini zaidi ya AK-47,SMG,LMG na tuliopita zamani jkt tuligusa RPG na G3 pia, hizi silaha ukienda polisi wanajifunza pia
 
G3,Ak47 zipo kundi la SMG" sub machine gun". Usichanganye mambo, silaha kipolisi zinahifadhiwa na kutumika kwa level ya kituo,wilaya,mkoa Kisha makao makuu. Hivyo tusiweke mambo yote hapa. Jua kua askali wa kipolisi hufundishwa mwisho Lmg/Rpg kwasababu hizo Ni silaha za msaada ngazi ya Section mpaka platoon.

Na kuanzia ngazi ya Combania kipolisi hawana changamoto za namna hyo Tena hiyo ni kwa wale Crises response team. Nenda Mtwala,Kigoma,Katavi,Lukwa na Kagera ndio utaelewa hii. Ila usidanganye watu hapa.

Ile mizinga ya masafa mafupi tusiiingize hapa, Lengo Ni kukuelewesha usichanganye mambo.
Hivyo tunaelewa kuwa Polisi wapo kudeal na changamoto ndogo dogo za kiusalama. Walau wapambane na kikundi Cha watu 20_35 hivi lakini we Ni shuhuda. Huwa wakikutana na changamoto kubwa wanawahi kulipoti kwa wakuu wa kamati za ulinzi na usalama kwaajili ya rainfocement ya wavunja vyungu vya uyoga kutoka napalia mbele nyuma pajakawa.

Kaka nikuambietu. Hiyo platoon unayo izarau wewe inauwezo wa kuingia msituni na kutangaza uasi na Polisi mkashindwa kbsa kwa nyenzo zote kuikabili. Ebwana usifanye mchezo ati.

Usiwapime Polisi kulinganisha na jeshi kwa kuua na kukamata majambazi ambao wanavamia Huku wanaogopa kujulikana,kukamatwa pia wakijua kabisa hawana backup Tena wanapambana huku wakihakikisha hawajulikani na wakijua kabisa adui yao kawazidi kisilaha idadi na ile Hali ya uhalali huwa inanguvu fulani hivi.Usitolee Tena mfano wa majambazi ambao wanakuja kuvamia na silaha zilizo katwa kitako na magazine yenye lisasi Saba. Huku wenzao wakiwa na mpaka za akiba
 
Kwakua sio ligi na nilichohitaji ukifaham umekifaham Basi hapo hakuna jipya.

Nikukumbushe uwezo wa kijeshi upimwa kwa mission/silaha nk, je! Magereza ili wawe wakali waende field na kundi linalo kinzana nalo kijeshi. Mfungwa muweke pembeni.
Nitarudi
hujui lolote.unaongea mambo ya vijiweni.
 
Chunguza tena alivyokuwa kavaa hizo gwanda!

Angalia kola na kofia ndiyo utapata jibu, kwamba kuvaa nembo ya ikulu kwene kofia yake ndiyo alama hiyo ya amiri jeshi mkuu.

Hizo nyota nyota unazotaka kusema zinavaliwa na ma kada wa jeshi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ungelitupatia ulinganifu wa hivyo vyeo kwa mtiririko, kwa mfano inspector wa Polisi ama SP akishikizwa jeshini atavishwa rank gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

"Afisa wa jeshi ni mwanajeshi, lakini siyo askari. Ni afisa au mwanajeshi.
Mwanajeshi anaweza kuwa askari lakini askari hawezi kuwa mwanajeshi"...why!

Contradiction kubwa sana hii!

Ninadhani katika ku distinguish kati ya Jwtz na polisi, magereza na idara zingine zinazohudumu katika wizara ya mambo ya ndani tungelisema hivi:

Inavyoeleweka kwa sasa, ukisema mwanajeshi ama jeshi, ni jina la jumla la maafisa na askari wa majeshi ya ulizi yaani Jwtz.

Katika majeshi hayo ya ulinzi, kuna makundi mawili ya vyeo, kuna kundi la maafisa wa vyeo mbali mbali na kuna kundi la askari wa vyeo mbali mbali.

Kwa hiyo hiyo dhana ya kusema askari hawezi kuwa mwanajeshi halipo.

Kuanzia askari hadi afisa wa cheo cha mwisho juu ni mwanajeshi.

Tukija kwenye idara za polisi, magereza na wengineo katika wizara ya mambo ya ndani:

Jina la jumla la polisi ama magereza huitwa maafisa wa Polisi, maafisa wa magereza, maafisa wa zimamoto ama maafisa wa uhamiaji nk.

Katika idara hizo pia kuna makundi mawili ya vyeo, kuna kundi la maafisa na kuna kundi la skari.

Sheria za majeshi ya ulizi (NDA) zimewataja polisi nk, kama civilian police, prison etc.

Hapa nimechangia kifupi sana kutoa mwanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo hiyo dhana ya kusema askari hawezi kuwa mwanajeshi halipo.

Majeshi ya kipolisi hayawezi kua na mwanajeshi,Ni suala la kulazimishatu. Ila hicho kitu hakipo.

Ukishajua mwanajeshi ninani,majukumu yake,wajibu wake na anapaswa kuwa wapi. Itatufanya tumalize ubishi. Pia ukifahamu wajibu na majukumu ya kipolisi. Hapo ndio utakua mwisho wa mabishano. Nani Mwanajeshi Nani Polisi. Mi ninacho kipinga ni kutokujua kua yeyote mwenye kushika silaha kwa kiswahili huitwa askali au kamanda haijalishi ni nani. Ona kwenye lugha za wenzetu hata mgambo atatambulika hivyotu kua yeye Ni mgambo (Militia). Askali wanyama poli the same (Ranger). Kwahyo nadharia ya askali kwa kiswahili ni kwa kila askali haijalishi ni nani. Ila Sasa kwenye majukumu ndio tunawatenganisha, nisieleweke vibaya.
 
Naona umemsifia kijana wa JKT na kumdharau KMKM, FFU na kuendelea kummwagia sifa Mpaka security guard wa SUMA JKT
Unasahau hao Watuliza ghasia gerezani na mtaani wote wamepita kwenye ujana wa JKT.
Hata huyo kijana wa JKT unaemsifia akiajiriwa tu upande usioupenda basi atapoteza hizo sifa unazompa.

Muache kudharauliana, serikali inatambua kila mmoja ni mtaalam kwenye majukumu yake.
 
Safiii mkuu naongezea Happ na ndo maana huitwa ASKARI JESHI - JW
ASKARI POLISI
ASKARI MAGEREZA n.k
 
Mfumo wa kiusalama wa marekani ni tofauti na Tanzania, Marekani wana Police Departments katika mfumo wa eneo husika, usilinganishe na Hapa kwetu ambapo polisi wamepewa hadhi ya Jeshi.
 
Hiyo dhana haipo mkuu, nakumbuka mara ya kwanza kumuona Mtu mmoja kamanda ilikuwa katika mavazi ya Askari jesh lakini baadae nikmuona akivaa sare za Askari polisi nafikiri kwasasa yupo usalama barabarani
 
Sasa ungelitupatia ulinganifu wa hivyo vyeo kwa mtiririko, kwa mfano inspector wa Polisi ama SP akishikizwa jeshini atavishwa rank gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi kushikizwa jeshini, Tena ni
rahisi kwa raia wa kawaida kuitwa jeshini kushiriki Jambo fulani kuliko askali kutoka hizo idara za kipolisi. Na ukiona wanajeshi wapo na Polisi basi ujue ni joint operation ambayo wao Polisi ndio wameomba, ikiwa jeshi linataka kufanya operation uraiani Basi jukumu la kipolisi wanalichukua Polisi wa Jeshi. Na Polisi hawato luhusiwa kuingilia operation hyo. Japo inakua imeingilia majukumu yao.

Suala la renk. Inafatwa seniority nani katangulia kupewa kamishenj. Ila sisi Tanzania tumepenyezewa siasa hadi huko kwenye vombo vya ulinzi na usalama. Ndiomaana CDF,IGP,DG,CGP,nk Wanaudhulia mikutano ya kisiasa Tena simpletu hata hawana stress alafu wanatudanganya hawafungamani na chama chechote.

Hivyo kwakua kipolisi huwa wanapewa kamisheni na kukabidhiwa majukumu makubwa. Yaani wanapewa kamisheni na kukabidhiwa labda kuongoza ukurugenzi wa makosa ya jinai ndipo hapo huwa wanapewa heshima Kama wateule wa Rais ngazi ya Kati chini. Mnielewe hivyohivyo hakuna namna. Sasa huyo unamringanisha na Nani jeshini nikua hatumlinganishi na afisa yeyote yule,Bali tunamchukulia Kama mteule wa Mh Rais kwenye hiyo ngazi. Na watu pekee wanao wajibishwa kijeshi katika kutokutii wakubwa wao. Ni wale NCO'S Pekee hakuna afisa yeyote yule kuanzia insign kwenda mbele. Rabda tu awe kamtangulia kupata commission kwa hivyo 2Lt to Commissioner..
Sasa kuanzia hao ASCP/I kuja mpaka kwa inspector msaidizi, jeshi haliwatambui Kama Ni maofisa hivyo wakienda jeshini watapigwa refresher course Kisha watakua wanajeshi wakawaida Hilo ni swala ambalo hata wao hawawezi kukubali.

Haya mengine unayo yaona yanaendelea ni kujalibu kuondoa migogoro isiyo na maana.
 
Hiyo dhana haipo mkuu, nakumbuka mara ya kwanza kumuona Mtu mmoja kamanda ilikuwa katika mavazi ya Askari jesh lakini baadae nikmuona akivaa sare za Askari polisi nafikiri kwasasa yupo usalama barabarani
Kwahiyo Kaka unafikiri huyo atakua Polisi mwanajeshi?. Mtu pekee anayeweza kuvaa vazi la idara nyingine ni Mwanajeshitu. Na hao wengine wakivaa wanahakikisha hawaingii mikononi mwa jeshi. Hivyo yaweza kua ulimuona kavaa lakini alikua kaziiba pahala. Maana Polisi ni in charge wa wenzao wengine wa mambo ya ndani Sasa hawezi kujihusisha na mambo yeyote ya jeshi la ulizi.
 
Hakuna Afisa/Askari anaeweza kuvaa vazi la Jeshi Jingine.

Acheni kulishana upropaganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…