Maji ni huduma ambayo Serikali inafeli vibaya mno, uhaba na mgao karibu kila mkoa japo mabilioni yanatumika. Rais Samia anashindwa wapi?

Kwa ujumla Serikali inafanya kazi nzuri sana hata hivyo kwa mtazamo wangu wanavyotumia Nguvu kubwa kusambaza maji; Wangetumia pia angalau robo ya hiyo Nguvu Kuhuisha vyanzo vya maji.

!
MKuu, umeongea point nzuri sanam kuhusiana na VYANZO VYA MAJI, lakini sio kuhusu huduma ya maji.

Kwa mfano, Dar kukosa maji tatizo sio vyanzo vya maji, tatizo ni watu kutokuwa makini na uzembe wa kazi. Maji yanayoingia baharini ukanda wa pwani ukilinganisha na yanayotumika kuwahudumia watu ni mengi mno! Kwa mfano, miaka ya 2000 wakati kampuni ya Songo Songo ikiweka mambomba ya gesi toka kule Somanga, iliiambia serikali kwamba nunueni mabomba ya maji ili tuwawekee pembeni ya mabomba ya gesi kutoka mto Rufiji kuja Dar, mbadilishe source ya maji Dar toka Ruvu kuja Rufiji. Unajua serikali ilikataa? Unafikiri kwa nini? Kwa sababu walijua watakosa fedha ya tenda ikiwa mabomba yangeletwa Dar kwa msaada!

Nimetoa mifano ya sehemu kama Iringa, Njombe, Tukuyu, Moshi nk. Maji yapo tele, na wala vyanzo vya maji havijaharibiwa. Na maji yanawezwa kusambazwa kwa garivity tu, lakini wapi. Angalia ramani, Tanzania tunaweza kuwa nchi inaongoza Afrika kwa kuwa na fresh water bodies nyingi na kubwa, na mito Lakini hatujaweza kutumia rasilimali hii, tunazidiwa na nchi ambazo ni jangwa kwenye huduma za maji.

Huko Mbeya, kuna wakati walipewa fungu la fedha la kununua mabomba ya maji kwa ajili ya wilaya ya Rungwe. Sasa katika ununuzi ule, injinia wa maji wa mkoa akaamua kuusimamia yeye, akanununua mabomba very low quality kwa bei poa lakini kwenye documents wakaweka bei ya juu. Walipoyafunga yalipasuka yote! Unajua hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alimfichia siri? Sasa niambie, tutafika kweli? Uzembe tu umejaa
 
Kweli kabisa. Yaani kuna uzembe upande wa huduma za maji nchini sijapata kuona. Sijui hawa watu wana akili za namna gani. Wanajiita viongozi lakini vitu vya msingi na rahisi kama kufikisha maji kwa wananchi vinawashinda. Bibi yangu alipata shida ya maji. Mama yangu pia, mke wangu pia, na sasa binti yangu atapata shinda ya maji. Hadi lini? Utafikiri tunaongelea kila mwananchi kununuliwa gari na serikalim hapanam ni kufikisha huduma ya maji ya uhakika kwa wananchi tu!
 
Huku Morogoro kuanzia kihonda kelekea mkundi, tungi ni balaa tuu!! Na akina side hata uwezo wa kuchimba kisima hatunaa!! Tunasubiriii maboza yalete ndoo moja shilingi mia Tano[emoji20][emoji20][emoji20] na familia ni shiidaa!!! Tunasubiriii mvua zikinyesha ndio nafuu yetuu!! Na mvua nazo ndio hazijii[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Maji na umeme ni huduma zisizo na kikomo yaani kuna wamasai na wahadzabe ukiwapelekea maji na umeme wanahama wanaenda mbali kuanzisha makazi mapya huko sasa tatizo haliwezi kuisha kwa style hyo
Fikirisha ubongo huo..

Hapo juu wametajwa hao watu?mimi nipo Dar hapo Mbezi kwenye stand kuu na maji hamna mimi ni mhadzabe useme nimeyakimbia hayo maji?
 
Dodoma mjini Nako nilishanga kukutwa mgao wa maji eti,huku nkuhungu yanatoka kwa wiki Mara 2 kaahh
Hivi hii nchi kuna mkoa ambao maji huwa yanatoka mfululizo mwezi mzima kweli?
 
Wasambazie watanzania wenzako wanunue walau ndoo sh 100 mkuu Mungu atakuongezea..
 
Wasambazie watanzania wenzako wanunue walau ndoo sh 100 mkuu Mungu atakuongezea..
Hata bure ningewapa Watanzania wenzangu tatizo mtaji wa mabomba ila kama mtu akitia timu hata aje na mapipa.
 
Huku Morogoro kuanzia kihonda kelekea mkundi, tungi ni balaa tuu!! Na akina side hata uwezo wa kuchimba kisima hatunaa!!
Changeni pesa mje mchimbiwe kisima Borehole.
 
Mkuu GT kuna kodi unalipa ukichimba kisima?
 
Mkuu GT kuna kodi unalipa ukichimba kisima?
Sijui, na kwasababu siyafanyii Biashara ni kwa ajili ya,domestic use.

Ila sitoshangaa wakija maafsaa na vitambi vyao na kuanza kudai serivce charge wakati hawajaingiza senti.

Wakidai nakifukia chap chap😁 just kiddin
 
Sijui nianze kufuga organic Sato ambao ni clean wasiokuwa na kemikali za kuhifadhia maiti?
 
Umenikumbusha Rungwe, sisi pale shuleni maji yalikuwa gravity..ikitokea yamekatika bas ni chamber zimeziba huko mliman, tunaenda kuzibua basi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Underground water bila chumvi. Lol! Kama mzaha vile.
 
Umenikumbusha Rungwe, sisi pale shuleni maji yalikuwa gravity..ikitokea yamekatika bas ni chamber zimeziba huko mliman, tunaenda kuzibua basi.



Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa watu wa Rngwe wameshindwa kufanya hilo kwa ajili ya wilaya yote? Hao ndipo utapoona labda Chadema wako right wanaposema wanataka utawala wa majimbo. Mnaletewa Mkuu na Mkurugenzi wa wilaya ambao hawajali maendeleo ya eneo kwa kuwa sio watu wa hapo. Wapo hapo kwa ajili ya kazi na mshahara, sio maslahi na upendo wa eneo kwa sababu ni wazaliwa wa hapo
 
Sijui, na kwasababu siyafanyii Biashara ni kwa ajili ya,domestic use.

Ila sitoshangaa wakija maafsaa na vitambi vyao na kuanza kudai serivce charge wakati hawajaingiza senti.

Wakidai nakifukia chap chap😁 just kiddin
MKuu kama bado hawajaja nashangaa, tena wanaweza kukufungulia mashitaka. Wanasema maji ni rasilimali ya taifa huwezi kuyatumia lazima uwe na kibali, hata kama ni borehole
 
MKuu kama bado hawajaja nashangaa, tena wanaweza kukufungulia mashitaka. Wanasema maji ni rasilimali ya taifa huwezi kuyatumia lazima uwe na kibali, hata kama ni borehole
Huwa naenda kuogelea Baharini mara kwa mara tena bure sasa kama Maji ni rasilimali ya Taifa mbona huwa siwaoni wakinisubiri na taulo langu?

Najua nchi hii inavisheria kandamizi vingivingi sana ambavyo huwa havifutwi ambavyo vingine tumetoka navyo kwa Mkoloni.

Au tulipewa Uhuru wa Bendera?

Mfumo wangu wa kuvuna Maji ya Mvua pia wataniuliza Kibali.

Au yule Mpenzi wangu kutoka Kagera mwenye "Maji" mengi pia watauliza Permit?

Wakija maswali watayakimbia.
 
Nadhani kuna tozo pia ikiwa unavuna maji ya mvua utafikiri yametoka serikalini 🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…