Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
- #61
MKuu, umeongea point nzuri sanam kuhusiana na VYANZO VYA MAJI, lakini sio kuhusu huduma ya maji.Kwa ujumla Serikali inafanya kazi nzuri sana hata hivyo kwa mtazamo wangu wanavyotumia Nguvu kubwa kusambaza maji; Wangetumia pia angalau robo ya hiyo Nguvu Kuhuisha vyanzo vya maji.
!
Kwa mfano, Dar kukosa maji tatizo sio vyanzo vya maji, tatizo ni watu kutokuwa makini na uzembe wa kazi. Maji yanayoingia baharini ukanda wa pwani ukilinganisha na yanayotumika kuwahudumia watu ni mengi mno! Kwa mfano, miaka ya 2000 wakati kampuni ya Songo Songo ikiweka mambomba ya gesi toka kule Somanga, iliiambia serikali kwamba nunueni mabomba ya maji ili tuwawekee pembeni ya mabomba ya gesi kutoka mto Rufiji kuja Dar, mbadilishe source ya maji Dar toka Ruvu kuja Rufiji. Unajua serikali ilikataa? Unafikiri kwa nini? Kwa sababu walijua watakosa fedha ya tenda ikiwa mabomba yangeletwa Dar kwa msaada!
Nimetoa mifano ya sehemu kama Iringa, Njombe, Tukuyu, Moshi nk. Maji yapo tele, na wala vyanzo vya maji havijaharibiwa. Na maji yanawezwa kusambazwa kwa garivity tu, lakini wapi. Angalia ramani, Tanzania tunaweza kuwa nchi inaongoza Afrika kwa kuwa na fresh water bodies nyingi na kubwa, na mito Lakini hatujaweza kutumia rasilimali hii, tunazidiwa na nchi ambazo ni jangwa kwenye huduma za maji.
Huko Mbeya, kuna wakati walipewa fungu la fedha la kununua mabomba ya maji kwa ajili ya wilaya ya Rungwe. Sasa katika ununuzi ule, injinia wa maji wa mkoa akaamua kuusimamia yeye, akanununua mabomba very low quality kwa bei poa lakini kwenye documents wakaweka bei ya juu. Walipoyafunga yalipasuka yote! Unajua hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alimfichia siri? Sasa niambie, tutafika kweli? Uzembe tu umejaa