Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Endapo jamii itaelewesha kuhusu imani na namna ya kuishi na imani zao basi mambo mengi sana yatapungua. Wengi wetu sasa hivi wanaamini mtu kuliko walichotakiwa kuamini.
Nani atafanya kazi hiyo nzito?
 
Ngoja RC waje hapa,
Dini yao inajitetea yenyewe, hizi nyingine ndio wanatetea kwa upanga.

In short dini zimeletwa na wakoloni.
ARAB--
LUTHER-LUTHERAN
USA-TAG
CATHOLIC-WAITALIANO
UINGEREZA-ANGLICAN.
 
Kwa bulldozer maji sio lazima ununue hata ya nyumbani na mafuta ya nyumbani hujalazimishwa kununua ni kuwa na imani tu.

kwahiyo mkuu maji ya chimbwe yatibiwe yawe na ubora wafanyakazi walipwe mabobo yatengenezwe , usafiri umeme, label halafu upewe bure.

Yeye atakuwa analima wapi hizo hela.
Hueleweki mara unasema hayauzwi sio lazima ununue,mara yanauzwa kwakuwa kuna gharama sijui mabomba sijui nini,au upo kwa mwamsposa umeanza kupandisha pepo
 
Wote waongo tu.
Hapana, siyo wote waongo. Maadhimisho ya ibada ya RC ni maudhui yatokanayo na dhima nzima ya kumwabudu Mungu wetu.

Tunafanya kama Kristo Yesu alivyofanya kumwabudu Mungu. Wote tunajua ya kuwa Yesu Kristo alipokuwapo duniani, aliingia hekaluni kwa ajili ya kuabudu, nasi tunaingia makanisani kwa ajili ya kuabudu.

Adhimisho la ekaristi takatifu ni tukio lililofanyika siku ya Alhamisi Kuu, ambapo alimega mkate na akawapa wanafunzi wake, na kuwaambia, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

Wakati fulani imani inaiingiliana na saikolojia. Watu huweza kupindisha ukweli na kufanya jambo linaloelekeana na jambo la msingi, hapo ni jukumu la walengwa kung'amua ukweli ulivyo.
 
Wote waongo kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Kama unabisha, nakuuliza swali rahisi tu, thibitisha huyo Mungu yupo.
 
Endapo jamii itaelewesha kuhusu imani na namna ya kuishi na imani zao basi mambo mengi sana yatapungua. Wengi wetu sasa hivi wanaamini mtu kuliko walichotakiwa kuamini.
Ukiwa mvivu wa kuyajua maandiko bure utakayajua kwa kuyalipia
 
Kuna utofauti mkubwa sana Bwaaa shekhe.

1. Maji ya Baraka hayauzwi ili hali yale ya upako yanauzwa.

2. Maji ya Baraka sio mali ya mtu, ili hali yale ya upako ni mali ya Mwamposa.

3. Maji ya Baraka yana nguvu ya Mungu, ili hali yale ya Upako hayana nguvu ya Mungu bali binadamu na ndio Maana yanauzwa.

Kuhusu Sakramenti na vimikate vingine.

1. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni mwili kweli na damu kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo, ili hali Mikate hiyo mingine ni Mikate tu kama Mikate.

2. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu inatupa Uzima wa Milele, Wakati Mikate hiyo mingine haina uwezo huo.

3. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni Kwaajili ya Wakristo Wakatoliki, tena waliojiandaa yaani wamejitakasa kwa toba na matendo mema, ili hali Mikate hiyo mingine inaliwa na yeyote bila kujali dini yake wala hali yake Kiroho.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
😅😅 Nicheke nikalale ......ehee uzima wa milele ni upi
 
Maji yetu Katoliki na hayo ya Mwamposa plna Tonny Kapola hayana shida ila tatizo linakuja pale Mtu anapoacha kumwabudu Mungu anabaki na Maria
Maria ni mwanadamu tu na baada ya kumzaa Yesu aliendelea na masiha kawaida na bwana ake na alipata watoto wengine: Kuendelea kumuita bikra ni uongo.
Lakini walokole kama TAG nawakubali kwakuwa hawana mambo ya sanamu wala maji ya upako.
Kwani Pana dhehebu linaabudu sanamu
 
Wote waongo kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Kama unabisha, nakuuliza swali rahisi tu, thibitisha huyo Mungu yupo.
Kuthibitisha kuwa Mungu yupo ni rahisi (kama ulivyouliza swali rahisi). Tutabase zaidi kwenye logic; wewe kuwepo duniani, chanzo ni wazazi wako, ukifuatilia mlolongo huo, mwisho wa siku utakuja kuona chanzo cha binadamu ni Adam na Hawa. Sasa hebu niambie, chanzo cha Adam na Hawa ni nani? Did they come from vacuum?
 
Logical non sequitur.

Kwanza hujathibitisha kuwa kulikuwapo na Adam na Hawa.

Pili, hata ukithibitisha kuwa Adam na Hawa walikuwapo, hujathibitisha kwamba waliumbwa na Mungu.

Yani ni hivi, hata ikiwa watu wa kwanza hawakutoka kwenye vacuum, huo si uthibitisho kwamba wameumbwa na Mungu.

Na kama unaona swali la "wametoka wapi, wametoka kwenye vacuum" ni muhimu, hata huyo Mungu naye naweza kukuuliza "Mungu naye katoka wapi, katoka kwenye vacuum"?
 
Back
Top Bottom