Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Endapo jamii itaelewesha kuhusu imani na namna ya kuishi na imani zao basi mambo mengi sana yatapungua. Wengi wetu sasa hivi wanaamini mtu kuliko walichotakiwa kuamini.
Nani atafanya kazi hiyo nzito?
 
Ngoja RC waje hapa,
Dini yao inajitetea yenyewe, hizi nyingine ndio wanatetea kwa upanga.

In short dini zimeletwa na wakoloni.
ARAB--
LUTHER-LUTHERAN
USA-TAG
CATHOLIC-WAITALIANO
UINGEREZA-ANGLICAN.
 
Hueleweki mara unasema hayauzwi sio lazima ununue,mara yanauzwa kwakuwa kuna gharama sijui mabomba sijui nini,au upo kwa mwamsposa umeanza kupandisha pepo
 
Wote waongo tu.
Hapana, siyo wote waongo. Maadhimisho ya ibada ya RC ni maudhui yatokanayo na dhima nzima ya kumwabudu Mungu wetu.

Tunafanya kama Kristo Yesu alivyofanya kumwabudu Mungu. Wote tunajua ya kuwa Yesu Kristo alipokuwapo duniani, aliingia hekaluni kwa ajili ya kuabudu, nasi tunaingia makanisani kwa ajili ya kuabudu.

Adhimisho la ekaristi takatifu ni tukio lililofanyika siku ya Alhamisi Kuu, ambapo alimega mkate na akawapa wanafunzi wake, na kuwaambia, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

Wakati fulani imani inaiingiliana na saikolojia. Watu huweza kupindisha ukweli na kufanya jambo linaloelekeana na jambo la msingi, hapo ni jukumu la walengwa kung'amua ukweli ulivyo.
 
Wote waongo kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Kama unabisha, nakuuliza swali rahisi tu, thibitisha huyo Mungu yupo.
 
Endapo jamii itaelewesha kuhusu imani na namna ya kuishi na imani zao basi mambo mengi sana yatapungua. Wengi wetu sasa hivi wanaamini mtu kuliko walichotakiwa kuamini.
Ukiwa mvivu wa kuyajua maandiko bure utakayajua kwa kuyalipia
 
πŸ˜…πŸ˜… Nicheke nikalale ......ehee uzima wa milele ni upi
 
Kwani Pana dhehebu linaabudu sanamu
 
Wote waongo kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Kama unabisha, nakuuliza swali rahisi tu, thibitisha huyo Mungu yupo.
Kuthibitisha kuwa Mungu yupo ni rahisi (kama ulivyouliza swali rahisi). Tutabase zaidi kwenye logic; wewe kuwepo duniani, chanzo ni wazazi wako, ukifuatilia mlolongo huo, mwisho wa siku utakuja kuona chanzo cha binadamu ni Adam na Hawa. Sasa hebu niambie, chanzo cha Adam na Hawa ni nani? Did they come from vacuum?
 
Logical non sequitur.

Kwanza hujathibitisha kuwa kulikuwapo na Adam na Hawa.

Pili, hata ukithibitisha kuwa Adam na Hawa walikuwapo, hujathibitisha kwamba waliumbwa na Mungu.

Yani ni hivi, hata ikiwa watu wa kwanza hawakutoka kwenye vacuum, huo si uthibitisho kwamba wameumbwa na Mungu.

Na kama unaona swali la "wametoka wapi, wametoka kwenye vacuum" ni muhimu, hata huyo Mungu naye naweza kukuuliza "Mungu naye katoka wapi, katoka kwenye vacuum"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…