Girland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2016
- 2,489
- 4,253
- Thread starter
- #121
Kiranga anapinga uwepo wa Mungu, lakini atakubaliana nami kuwa kuna kanuni zinazoendesha ulimwengu.Mfano kani ya uvutano na mambo mengine mengi.Logical non sequitur.
Kwanza hujathibitisha kuwa kulikuwapo na Adam na Hawa.
Pili, hata ukithibitisha kuwa Adam na Hawa walikuwapo, hujathibitisha kwamba waliumbwa na Mungu.
Yani ni hivi, hata ikiwa watu wa kwanza hawakutoka kwenye vacuum, huo si uthibitisho kwamba wameumbwa na Mungu.
Na kama unaona swali la "wametoka wapi, wametoka kwenye vacuum" ni muhimu, hata huyo Mungu naye naweza kukuuliza "Mungu naye katoka wapi, katoka kwenye vacuum"?
Sayansi inazieleza vizuri kanuni hizi bila kutuambia zimetoka wapi?Suala la kuamini au kutokuamini uwepo wa Mungu linabaki kuwa maamuzi binafsi.
Baba wa Sayansi Kama Isaac Newton aliamini uwepo wa Mungu halafu mtu mmoja alnapinga?!
Mwenye masikio na asikie