DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa saratani wamekuwa wakitokea kanda ya ziwa jambo ambalo linapelekea serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini kanda ya ziwa...
Naomba kuuliza,haya maji ya kuuoshea maiti,ni maji Dawa au ni yale maji yanyokusanywa baada kuoshea maiti na kuhifadhiwa?
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa saratani wamekuwa wakitokea kanda ya ziwa jambo ambalo linapelekea serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini kanda ya ziwa...
Ungesema Dawa za kuhifadhia maiti na siyo maji,mwanza samaki waliohifadhiwa kwenye majokofu hazina wateja,Sababu ni jirani na ziwa hivyo wateja hupenda kununua samaki asubuhi na jioni waliotoka kuvuliwa mida hiyo hiyo.

Hivyo waadhirika wakubwa ni wateja wa mikoani.
 
Story za vijiweni zinamsumbua
 
O.K
Screenshot_20220914-080936_Google.jpg
 
KIla MTU anataka kuwa tajiri kwa kutumia njia zozote zile !! Hata kama kwa njia haramu !! Sijui ni akina nani walitufundisha hivi !!
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa saratani wamekuwa wakitokea kanda ya ziwa jambo ambalo linapelekea serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini kanda ya ziwa...
Hii kitu kama ni kweli tutakufa wengi,wapo baadhi ya watu pindi wakila samaki familia yote inaona madhara kwenye ngozi, majipu yasiyoeleweka,pengine najaribu kukuelewa pamoja tatizo la Kansas kuwa kubwa Kwa baadhi ya maeneo.
 
Haya yote ni matokeo ya ujinga na upumbavu kwenye jamii.

Elimu rasmi na isiyo rasmi iendelee kutolewa kwa nguvu zaidi.

Muingiliano na jamii nyingine zilizostaarabika pia utapunguza kama siyo kuondoa kabisa tatizo.
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa saratani wamekuwa wakitokea kanda ya ziwa jambo ambalo linapelekea serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini kanda ya ziwa...
Utakuwa huelewi kinachofanyika! Ukweli ni kwamba hawatumii maji ya kuoshea maiti bali wanatumia formalin kuhifadhia samaki ili wasichine!
 
Utakuwa huelewi kinachofanyika! Ukweli ni kwamba hawatumii maji ya kuoshea maiti bali wanatumia formalin kuhifadhia samaki ili wasichine!
Sasa mkuu kama wanatumia formalin kuhifadhi samaki, kwa nini tatizo lisiwe kubwa huku Dar na mikoa mingine iliyo mbali na kanda ya ziwa ambako ndo tunategemea watumie samaki waliohifadhiwa?
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa saratani wamekuwa wakitokea kanda ya ziwa jambo ambalo linapelekea serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini kanda ya ziwa...
Kama wateja wa hiyo ni wenye maduka ya dawa za asili,na waza kuwa huenda Kuna walakini pia kwenye dawa za maumivu ya meno japo zinasifika kuwa ni nzuri,ila upo uwezekano wa hii kitu kuwa Moja ya malighafi ya kuzitengenezea.
 
Baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Phillip Mpango amesema ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani katika mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na baadhi ya watu kutumia maji ya yanayotumika kuoshea maiti pamoja na dawa aina ya Cloroform inayotumika kuhifadhi samaki.

DK. Mpango alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa saratani katika huspitali ya rufani ya kanda Bugando jijini Mwanza, jengo ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.6.

Baada ya kauli hiyo, inadaiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jana jioni ilianza kugawa fedha kwa waandishi wa habari kuzuia stori hiyo isitoke kwenye vyombo vya habari.

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa zinadai, fedha hizo zilikuwa zikitolewa na Katibu wa mkuu wa mkoa, bwana Matia Levi.

Inaelezwa zaidi ya waandishi 20 walipokea mshiko huo ili habari hiyo isiandikwe, lakini waandishi walipokea na kutoa habari hiyo.

Hata hivyo Leo mchana, Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa hiyo na inaelezwa wamesikitishwa na kauli ya Makamu wa Rais.

IMG-20220914-WA0043.jpg
 
Back
Top Bottom