This is a very cheap argument, maji ya kuoshea maiti yana uhusiano gani na kutokea saratani.......do you have any mechanism behind.
Labda tuseme unamaanisha kemikali inayotumika kuhifadhi maiti, mfano formalin......hivi inaingia akilini utumie formalin kwenye samaki na isilete usumbufu kwa watu wanaohusika na wateja kwa kupiga chafya au kuwashwa machoni? Hizo kemikali are very pungent ukiifungua kidogo tu hapawezi kukalika.
Kama swala ni saratani inasabbishwa na hivyo vitu kutumika kuhifadhia samaki, logic inaonyesha kwamba case za saratani zingekuwa nyingi mikoa ya mbali na Mwanza maana ndo watatumia zaidi samaki waliohifadhiwa kuliko Mwanza ambako tutategemea watu wengi wanatumia samaki fresh ambao hawajahifadjiwa na kitu chochote.
Hawa watu wanajaribu kupotosha kiini cha saratani kuwa juu huko Mwanza sijui kwa maslahi ya nani. Wafanye utafiti wenye mashiko, tatizo la saratani kuwa juu kanda ya ziwa ni kutokana na kemikali za migodini zinazoelekezwa kwenye vyanzo vya maji ikiwemo mito na kuishia ziwani. Haya ndo yaleyale ya tume ya Manyere kwamba samaki wa mto Mara walikufa kutokana na kuzidiwa na kinyesi na mikojo ya ng'ombe. Pathetic!!