Majibu haya ya Lissu kwa Lema juu ya ujio wake, yananifanye niwaze kuwa kuna Power of Nature iliyo nyuma ya Lissu ambayo hata yeye mwenyewe haielewi

Majibu haya ya Lissu kwa Lema juu ya ujio wake, yananifanye niwaze kuwa kuna Power of Nature iliyo nyuma ya Lissu ambayo hata yeye mwenyewe haielewi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Nilimuuliza haugopi?akajibu siogopi!Nikamwambia,wanaweza kukupiga risasi tena au ukafungwa kwa hila,akajibu NIKO TIYARI kwa lolote.Mungu ni mwema,Kamanda Tundu Lissu kurudi nyumbani kwa mapambano tena ni muujiza wa Mungu mwenyewe.Nitakuwepo Dar es Salam kumpokea siku ya jumatatu-Godbless Lema on twitter.

Maoni yangu
:
Nikisoma katikati ya mistari,napata hisia kuwa, wasiwasi au mashaka haya ya Lema juu ya usalama wa Lissu, si tu ni mashaka ya Lema peke yake, bali pia yatakuwa ni mashaka walioyonayo viongozi wengine wa CHADEMA, na Lema kaamua kuweka wazi hili ili umma ujue kuwa Lissu kaamuaa mwenyewe kuja na si kwa kushawishiwa au kushurutishwa na viongozi wenzake katika chama(kuna watu wanaweza kuwaza hivyo).

Kwa mtazamo wangu,pengine jambo kubwa hapa ni kuwa,kuna nguvu kubwa inayomsukuma Lissu na ambayo hata Lissu mwenyewe atakuwa haielewi, na ili malengo yatimie, ni lazima Lissu apite katika hatua alizopita na pengine kuna hatua zingine atapaswa kupita kabla ya kutimia yaliyopangwa kutimia kupitia Lissu iwe ni leo,kesho,keshokuwa au vinginevyo.

Ni hisia zangu pia kuwa, hata katika ngazi ya familia, watakuwa wamejadili hili jambo, ila bado naamini ni nguvu hiyo ndio ili-prevail na ku-influence uamuzi kuwa Lissu arudi.

Hint:Tukumbuke wengi walikuwa hawaamini kama Lissu anaweza kurudi, ila ndio hivyo anarudi.

Let's wait and see how this Power works/influence things.
 
Well, mi ni pro-Magufuli kindakindaki.

Ila Lissu akirudi halafu serikali imdhuru au imkamate au imbugudhi kwa namna mmoja au nyingine nitawashangaa sana dola na nikiri wazi hii itatia doa image ya Magufuli niliyonayo kwake.
Tambue tu wewe unawakilisha wengi na hauko peke yako mwenye fikra kama hizo, na ndio maana nasema, kuna nguvu iko nyuma ya huyu mtu.
 
I really wish angebaki ulaya,labda hataki kuonekana amekua msaliti wa nchi yake kwa kubaki ulaya...anatoa sadaka usalama wake ili tu asionekane msaliti... very sad..
"anatoa sadaka usalama ili tu asionekane msaliti" haya maneno yana maana gani?. Ndani ya nchi sijaona mtu mzalendo kama Lisu, tatizo lake kubwa nikuwaeleza wakubwa ukweli huku wakiwa wanakula.
 
Kwa Ushauri wangu!!
Lisu angekadili na uongozi wa Chadema na kufikia Muafaka kuwa wasifanye shamra shamra za mapokezi kwa sababu ya Kuheshimu Uafrika wetu wakati huu wa Msiba mkubwa wa Kitaifa.

Nafikiri Lisu angesema mwenyewe kuwa anawaomba watanzania waendelee na Maombolezo ili kutoligawa taifa kihisia.
Kuepuka watu wa Tiafa moja kuwa na hali tofauti kwa wakati mmoja hawa wanashangilia na hawa wanaomboleza.

Namkubali sana Lisu.
Hekima ni Roho toka kwa Mungu. Ukikosa hekima uongozi unakua mgumu sana. Lisu atumie hekima na Busara wakati huu.
Ghasia na vurumai zikitokea wakati huu wa Maombolezo litakua ni jambo lisilo na Busara wala Hekima. Wanaweza wakamuacha wasimkamate lakini wananchi hawa hawa wanaopenda kuona mila zetu na utaifa wetu unatuunganisha watakosa imani na Lisu na kumuona kuwa ni mtu Katili asiyejali hata hisia za wanafamilia ya Mkapa. Hii itakua ni dosara kubwa. Bora hata angeahirisha mpaka Hayati B.W. Mkapa akazikwa kwa heshima.

Ningekua ni Mimi Lisu , ambaye kwa kiwango Kikubwa nimewahi kufanyiwa ubaya na roho mbaya sana na binadam kuliko hata wanyama wa mwituni ningefanya yafuatayo :-
Ama ningesogeza Mbele tarehe ya kurejea nchini mpaka Mazishi ya Hayati Mkapa yapite au Ningekuja lakini ningewaomba watanzani wenye mapenzi mema na Taifa letu wasifanye mapokezi yoyote na shamra shamra kubwa za mapokezi.
Baada ya kutua Air Port ningekwenda moja kwa moja mpaka kwa Hayati Benjamin Mkapa kumpa Mkono wa Pole Mjane wa Marehemu mama ana Mkapa.
Hii ingemjengea heshima kubwa sana kitaifa na kimataifa na kuwafundisha vijana wadogo hasa wa miaka ya 82 na wazee ndani ya mavyama ya siasa kuwa Chuku haiondolewi kwa Chuki Bali huondolewa kwa Upendo. Giza linaondolewa na NURU.
Kwenda Moja kwa moja kwenye msiba ingempa nafasi kubwa ya kuonana na watu wengi,miongoni mwao ni Wale walioshangilia mateso yake. Hii pia italeta hisia na imani kubwa kwa Watanzania kuamini kuwa Lisu sio mtu wa visasi zaidi ya amani.

Ni ushauri wangu tu kwa kuwa Sijawahi kumwona Lisu akiwa na ubaya na mtu zaidi ya kupambana kwa hoja za kisiasa.

Lakini pia kuna jambo naliona dhahiri toka kwa Mbowe na wenyeviti wengine wa vyama; wanatamani Jambo lingine baya zaidi limpate Lisu ili iwe ndiyo kafara yao kisiasa wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi lakini kwa hakika hawana nia njema na Lisu zaidi ya kutaka kuona serikali inakosea kwa kumkamata Lisu na kuibua Tafrani ili eti Mabeberu ya huko Gomora yaibuke na kuiwekea serikali vikwazo vikali kwa kutoheshimu haki za binadam.
Ikumbukwe kuwa endapo Lisu atafanya jambo litakalofanya akamatwe basi ni dhahiri kuwa yeye ndiye atakayebebeshwa lawama kubwa kuwa amejitakia na akitiwa Gerezani ni dhahiri kuwa hataachiwa mpaka uchaguzi upite, jambo litakalomnyima fursa ya kufanya kampeni kwenye mikutano ya hadhara.
Lakini kwenda kwenye msiba kimya kimya na kushikana mikono na watu kama Waheshimiwa Ma Spika wa zamani na Mzee Joseph Warioba na wengine kutaleta hisia kubwa za utaifa. Endapo Lisu atatangaza hadharani kuwa wapenzi na mashabiki wake watulie kipindi hiki kigumu kwa familia ya Mkapa na taifa kwa ujumla litakua ni jambo litakaloifanya serikali ikose sababu za kumtendea Lisu ubaya.

Pia naishauri Serikali iepuke kumkamata Lisu wakati huu wa Maonbolezo makubwa ya Taifa na pia kuelekea uchaguzi Mkuu.
Tuiache asili na mila za kiafrika zihukumu endapo Lisu na Mbowe watahamasisha kufanyika kwa mapokezi na shamra shamra zifanyike wakati huu wa Msiba.
Watanzania na waafrika watasikitika sana kuona Lisu akishindwa kuheshimu mila na Desturi za kiafrika wakati wa msiba.
Lisu atajipunguzia maksi yeye Mwenyewe.

Huu ndio wakati wa Serikali na Tundu wa kuonyesha Hekima,Busara na maarifa makubwa kuhusiana na Ishu ya Lisu.
 
Kama haogopi kwanini ameomba kulindwa? Kwanini anajisemesha semesha ili watu wamsikie?
Ukweli ni kwamba anahofia kifo pia kwa sasa hanapesa za kuendelea kuishi huko. Ina maana hana namna nyingine zaidi ya kurudi.
 
Nilimuuliza haugopi?akajibu siogopi!Nikamwambia,wanaweza kukupiga risasi tena au ukafungwa kwa hila,akajibu NIKO TIYARI kwa lolote.Mungu ni mwema,Kamanda Tundu Lissu kurudi nyumbani kwa mapambano tena ni muujiza wa Mungu mwenyewe.Nitakuwepo Dar es Salam kumpokea siku ya jumatatu-Godbless Lema on twitter.

Maoni yangu
:
Nikisoma katikati ya mistari,napata hisia kuwa, wasiwasi au mashaka haya ya Lema juu ya usalama wa Lissu, si tu ni mashaka ya Lema peke yake,bali pia yatakuwa pia ni mashaka walioyonayo viongozi wengine wa CHADEMA, na Lema kaamua kuweka wazi hili ili umma ujue kuwa Lissu kaamuaa mwenyewe kuja na si kwa kushawishiwa au kushurutishwa na viongozi wenzake katika chama(kuna watu wanaweza kuwaza hivyo).

Kwa mtazamo wangu,pengine jambo kubwa hapa ni kuwa,kuna nguvu kubwa inayomsukuma Lissu na ambayo hata Lissu mwenyewe atakuwa haielewi, na ili malengo yatimie,ni lazima Lissu apite katika hatua alizopita na pengine kuna hatua zingine atapaswa kupita kabla ya kutimia yaliyopangwa kutimia kupitia Lissu iwe ni leo,kesho,keshokuwa au vinginevyo.

Ni hisia zangu pia kuwa, hata katika ngazi ya familia, watakuwa wamejadili hili jambo, ila bado naamini ni nguvu hiyo ndio ili-prevail na ku-influence uamuzi kuwa Lissu arudi.

Hint:Tukumbuke wengi walikuwa hawaamini kama Lissu anaweza kurudi, ila ndio hivyo anarudi.

Let's wait and see how this Power works/influence things.
Haya nayo ni maajabu.

Lissu asirudi nyumbani kwa sababu zipi hasa?

Aogope kurudi nchini kwake, abaki huko uhamishoni kwa sababu zipi? Kuitwa msaliti na kuachia mbwa wammalize? Ndiyo iwe sababu ya yeye kurudi nyumbani?

Mbona mnawapa vichwa sana hawa watesi wenu, na ndio wanapozidi kukaza kamba wakijua nyinyi ni waoga.

Lisu anavunjiwa haki zake, halafu ndiye awe mwoga kama mharifu? Hii ni kitu gani hii?

Haya mnayoyaweka hapa ndiyo yanayowapa nguvu wanaowaonea. Wanajua mmekwishaingiwa na hofu.

Haya mnayoweka hapa ndio sababu zitakazofanya kazi yenu ya kuwaondoa iwe ngumu zaidi, kwa sababu hao mnaowagwaya wanachoweza kufanya ni kitoa mfano mdogo tu tena ili kuwasambaratisha kabisa. Wakiua mmoja au wawili kati yenu wanajua wamemaliza kazi na kwa hao wawili wanajua hali haitawawia mbaya sana.

Watakuwa wamewaogopesha, na wala dunia haitastuka sana kwa vifo vya hao wawili na vilema kadhaa, na mahabusu, n.k.

Kumbuka, wao hata kama ni vichaa, lakini bado wanazo akili za kutosha za kuwaonyesha kwamba Lissu sasa yupo kwenye ngazi tofauti kabisa na ile aliyokuwepo kabla ya yale yaliyompata mwanzo.

Hawatakiwi kumgusa tena kwa njia zile walizotumia mwanzo. Akili ya kuwafahamisha hivyo wanayo sana.

Na hata kama si hivyo, na haya maigizo ya kuwa wafuata dini je?
Wao wataona wanaowaigizia bado wana amini maigizo hayo?
 
Kama haogopi kwanini ameomba kulindwa? Kwanini anjisemesha semesha ili watu wamsikie?
Ukweli ni kwamba anahofia kifo pia kwa sasa hanapesa za kuendelea kuishi huko. Ina maana hana namna nyingine zaidi ya kurudi.
Mbona hajaomba achangiwe pesa?

Nina hakika wapo wengi ambao wangeweza kujitolea kuchanga ili aendelee kuishi huko.

Au, hivi mkuu, wewe unaelewaje watu kuishi mahali kokote duniani. Yeye Lissu hawezi kuishi kwa njia hizo hizo wengine wanazotumia kuishi huko?

Mbona wewe unalindwa, unaogopa nini. Au hujui kwamba unalindwa usidhurike?
 
Mbona hajaomba achangiwe pesa?

Nina hakika wapo wengi ambao wangeweza kujitolea kuchanga ili aendelee kuishi huko.

Au, hivi mkuu, wewe unaelewaje watu kuishi mahali kokote duniani. Yeye Lissu hawezi kuishi kwa njia hizo hizo wengine wanazotumia kuishi huko?

Mbona wewe unalindwa, unaogopa nini. Au hujui kwamba unalindwa usidhurike?
Hongera sana ndugu kwa majibu murua. Kwa kifupi ni kwamba Lissu haogopi na watanzania sasa hatuogopi. Enough is Enough, Lissu anarudi na anapambana kwa hoja sie watanzania tukimuunga mkono.

Lolote watakalomfanya Lissu watakuwa wame endorse nchi kutumbukia kwenye shida kubwa na kwa hatua tuliyofikia watanzania enough is enough watuue wote kama wataweza.

No hate No fear
 
Kama haogopi kwanini ameomba kulindwa? Kwanini anjisemesha semesha ili watu wamsikie?
Ukweli ni kwamba anahofia kifo pia kwa sasa hanapesa za kuendelea kuishi huko. Ina maana hana namna nyingine zaidi ya kurudi.
Endeleeni tu na propaganda zenu uchwara
 
Back
Top Bottom