Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma


Ingekuwa vizuri kama ungekuwa unafanya research kabla ya kuropoka ili usipotoshe wenzio...mwaka 2004 Riz1 bado alikuwa darasani,na amemaliza 2005.. Uwakili hatufanyi mitihani kama unavyofikiria!!!bali ni oral interview;sasa cjui hao IMMa waliingia nae kwenye panel ile na kumsemea/kumjibia maswal kama unavyodanganya hapa???tuache ushabiki maandazi,haulipwi..utapiga domo wewe wenzio wanakula maisha..
 
Mara chache mwl Nyerere alizungumzia sababu za yeye kutopata daraja la kwanza(First Class) alipokuwa Chuo kikuu. Mwl Nyerere alisema mimi nilipokuwa Chuo kikuu nilikuwa na akili na uwezo wa kupata daraja la kwanza lakini niliamua kufanya siasa na uanaharakati huku ninasoma na kuamua kuwa tayari kupata alama za kawaida darasani. Nilifanya uchaguzi mwenyewe lakini uwezo nilikuwa nao. Hii ni kwa sababu niliona harakati za kuleta mabadiliko zilikuwa muhimu kuliko mimi kusoma kwa bidii na kupata harakati.

Maelezo ya John Mnyika

Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi.

Wote walikuwa wanaendesha harakati huku wakiwa wanasoma,
Wote waliona kuendesha harakati ni muhimu kuliko alama za darasani,
Wote wana akili ya kuzaliwa ambayo iko very sharp,
Wote ni wanasiasa wanaopambana na mifumo iliyopo madarakani (Nyerere vs wakoloni na Mnyika Vs CCM mafisadi)

Tofauti ndogo tu ni kwamba Nyerere alihitimu na degree ya kawaida na J Mnyika alimaliza miaka mitatu Chuo kikuu akiahirisha mitihani ya mwisho kutokana na harakati zake. Na harakati hizo sasa zimekwamisha juhudi zake za kurejea darasani na hakuna dalili ya kupewa associate graduate kama ilivyo ktk nchi zingine.

Hongera Mnyika.
Kama Nyerere alifika Ikulu, who knows wewe utafika wapi!!
 
MORIAH,

Tupo karne ya ishirini na moja (21st Century).
 
Last edited by a moderator:
Kamanda Mnyika umefanya jambo la muhimu sana kueleza yote sasa naamini itakuwa ni fundisho kwa wote pale wanapopewa shutuma wawe wanajibu sio kuwa kimya ....hiyo ya kuwa kimya inafanya tuamini ni kweli yasemwayo na mwisho inakuwa story mtaani sio kwenye JF tu
 

Ameona ni relevant 2 ans nw, in orda 2 stop ur nuinsense! I realy hate grapeveins za kijinga! Instead of doing smthng constructive, nape na riz u end up kufatilia maisha ya wa2! Acheni ujinga jaman!
 
nape moses nauye form 4 mwaka1997 nsumba sec matokeo ya mtihani division 3 point 22 combination hazikukubali, halikwenda high school kwa sababu ya nafasi ya mzee,form six mwenge sec singida matokeo div zero,je anao uhalali wa kuhoji elimu ya mnyika kweli
 

Hana uhalali si unaona anavoona aibu kuleta matokeo yake?
 
Nakushauri harakati zako uzitengenezee kitabu, nimefarajika kusoma hii historia yako ya elimu
 
Hongera mnyika kwa kuyazima hayo mavuvuzela ya ccm?? Sasa na sisi wananchi tunawataka waweke matokeo yao hapa jf kuanzia form 4 hadi chuo kikuu,msipotuwekea tutajua nyie ndio vihiyo na degree za favour
 
Nape na ridhiwani na nyie tupeni kiwango chenu cha elimu,mmelikoroga sasa mlinywe
 
Heko Mnyika. Nimeishiwa maneno. Ila wewe ni noma.
 
Elimu ni uadilifu siyo makabrasha pekee yangelikuwa ni hayo tu nchi hii ingelikuwa Tokyo ya dunia.........wezi na wabadhirifu wakubwa wana makaratasi lakini hayana manufaa kwa umma............
 
Ameona ni relevant 2 ans nw, in orda 2 stop ur nuinsense! I realy hate grapeveins za kijinga! Instead of doing smthng constructive, nape na riz u end up kufatilia maisha ya wa2! Acheni ujinga jaman!

Kama ni za kijinga kwanini amekuja kujibu?! Kama umepewa hoja za kijinga, na wewe unafahamu kuwa ni za kijinga na bado ukaja kuujibu ujinga huo; basi wote ni wajinga kinyume chake angepuuzia na kuona wote walioleta hoja ni wapuuzi tu!
 
Tuna watu wa ajabu sana nchi hii,wenye attitude za ajabu!!sasa umeandika u..tu.mb.o gani hapa?-mnyika kaaelezea vizuuri hapa lakini wapi!attitude!
shukrani kwako mnyika na shukrani saana kwa Ridhiwan kwa ustaarabu mkubwa uloonesha hapa!
By the way,what matters to us is what you deliver,your impact kwenye society inayokuzunguka na sio utitiri wa vyeti!
Hakuacha chuo kwa sababu ya matokeo mabaya...so whats the point?hicho cheti cha BBA ambacho angepata kama angemalizia chuo kingetusaidia nini wananchi wa ubungo??
 
Kwa walio wahi kupita shule (sekodari) wanaelewa inahitaji uwezo wa juu kiasi gani kupata A 9. Hii ni zaidi ya kipaji maalumu. Nachelea kusema mheshimiwa Mnyika ndiye Mbunge Pekee katika bunge la sasa aliyefaulu sekoari kuliko wote
 
Muda unapotea kujadili A Tisa za mnyika...na yeye kutomaliza degree yake...? Hiyo degree akiamua ku carry credits Ana uwezo wa kuimaliza hata mwaka huu Akitaka....na ndani ya miaka mitano akaafanya kabisa na masters hadi phd......

Tungetumia Muda huu kujadili devision Zero ...260'000 ......ndani zikiwemo F za hesabu 300,000 na ushe na kati ya hizo F......160,000 wakipata Alama Kati ya 0 hadi 9 ......Matokeo mabaya kabisa kwenye historia ya Tanzania ( source NECTA )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…