Majibu Kwanini Wasanii Wetu Hawaitwi Kwenye Steji Kubwa Duniani

Majibu Kwanini Wasanii Wetu Hawaitwi Kwenye Steji Kubwa Duniani

Anakuja EBM kuwastua fursa za nje hata mjue greencard lottery ni nini mkapambane mchukue dola za USA na kurudisha nyumbani bado mnamkamata kama mwizi mnajidai mara ni jasusi, mnashindwa kuelewa volume ya diaspora huchangia sana mambo kama hayo, mmelala usingizi wa pono leo mnaona makongamano makubwa kigali mnatoa macho wakati wenzenu wana urai pacha na wako wengi huko duniani

Umemaliza mkuu. Asante
 
Naandika huu uzi baada ya kumsoma kamikaze kwenye uzi wake: Mafanikio ya mwanamuziki Burna Boy, Nini tunajifunza!

If anything wasanii wabongo inabidi walalamikie ufinyu wa watanzania wengine nje ya nchi hususani in the boardrooms.

Nigerians wapo wengi ndani na nje ya nchi yao. Unaposikia msanii wa naija kajaza ukumbi nje unakuta zaidi ya watu humo ndani ni Nigerians wenyewe. Unategemea Dayamondi ajaze ukumbi vp nje? Nyie wabongo mpo wangapi? Nani wakulalamika hapo dayamondi au nyie?

Nigeria ina timu ya basketball ambayo players wake wote wamezaliwa na wanacheza USA. Unashangaa vp msanii wa Nigeria kutumbuiza all-star game? Nyie bongo mna players wangapi NBA? Nani atawashika mkono huko NBA? Hapo wakulalamikiwa ni dayamondi au nyie wabongo wengine?

Nigeria ina hadi timu ya Bobsleigh sport, probably hujawahi usikia. Ni mchezo wa kwenye ice ila Nigeria hamna ice kabisa kama bongo tu, unadhani wanajuaje kuucheza? Players wake wote wamezaliwa na wanaishi USA. Utashangaa vp msanii wa Nigeria kuitwa kwenye function ya bobsleigh?

Bado NFL. Watu wenye asili ya Nigeria ni wengi kuliko kawaida kwenye huu mchezo. In a yr or two kuna msanii wa NG atatumbuiza kwenye superbowl believe me you. Nyie mna wachezaji wangapi NFL?

Kanu, Okocha, Ihenacho, Obi Mikel, Victor Moses na sasa Osimhen wa Napoli wote ni Nigerians, nyie wachezaji wenu wangapi wamefika UCL? Timu yenu ya taifa lini imeenda World cup? Bado unashangaa wasanii wa Nigeria kuitwa kwenye stage ya UEFA?

Viongozi wa Nigeria wamewahi na bado wanashika nyadhifa mbalimbali duniani more than any other country in Africa. Wapo kwenye boardrooms za maamuzi, nyie mpo wapi? President wa Toronto Raptors Masai Ujiri ni mnigeira, Ime Udoka aliyekuwa kocha wa Boston Celtics ni mnigeria. Unadhani wakiambiwa walete mtumbuizaji watamleta Marioo au msanii wao?

Kama you're reading btn the lines utagundua uraia-pacha plays a big part as well. Wanigeria kibao wamezaliwa na kukulia nje including Burna boy mwenyewe aliyekulia UK, Davido kazaliwa US ila wanapeperusha bendera ya NG. Nyie mna uraia pacha?

If anything wasanii wetu wamefanya kazi yao, hawana deni kabisa. Dayamondi, Samatta na wasanii wengine walipofika ni juhudi zao binafsi and they can only do so much. Wanaenda kwa speed ambayo wabongo wengine hawana, we're letting them down. Samaki ndani ya aquarium hawezi kuwa mkubwa zaidi ya aquarium yenyewe.

Nipo around mazee.
Hata msanii wao mkubwa kacheza kwenye series moja kubwa tu US ya POWER. Shemeji yetu
 
Kwenye hizo hizo nyimbo unazoponda Zimemfanya diamond aitwe big brother kuperform, kuperform tuzo za mwanasoka wa Africa ile aliyochukua Mane, kuperform karibia nchi zote ukanda wa west Africa, kuwa dominated kwenye Tuzo ya BET pia kuperform kwenye platform ya Grammer wewe ujaelewa somo la mtoa mada Diamond mafanikio mengi aliyopata ni kwasababu ya juhudi binafsi ndio anachozungumzia kilichokosekana ni network ya nchi yake abroad ukilinganisha na nguvu waliyonayo Nigeria abroad sijui unachoponda ni nini
Hujaelewa Comment yangu, Rudi kasome tena au urudi shule? Uchague moja.
 
Siukatai Uloko wao... Ila Basi waimbe Kiswahili Fasaha. Nyimbo zinazoharibu Lugha yetu binafsi sizipendi.

Mkuu I don't condone nyimbo zisizo tumia Kiswahili fasaha ila mziki wa nchi yeyote ile una vionjo vya namna hiyo. Ni kwa sababu Nigeria hamuelewi vizuri lugha yao ila lazima na wao wanamatumizi yasiyo sahihi ya lugha.

Leo rappers wa US ukisikiliza mziki wao kuna muda hutoki na kitu hawa kina Lil Lil something ila ndo wanasikiizwa zaidi.
 
List the shows. List the venues. List the dates okoa nguvu na muda.

Singeli ni mziki wa wapi na umefika wapi?

Vp tasnia zingine wabongo mpo wangapi au napo hamna identity yetu? Nimelist soka players na NBA players kwenye uzi wangu, nitajie wabongo. Bado finance and technology

If you can't name the names I rest my case.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Strong argument, bravo.
 
Nikufikirishe kidogo...South Africa ambayo ina wazungu kibao..wa south kibao wapo nje..Tajiri no 1 dunian ana asili ya south..mboma wasanii wao hawa hit kama wa Nigeria? Au hawaimbi kingereza wanaimba kizulu[emoji849]?
Kwamba maeehemu aka

Casper nyovest

Costa Tec

Na wengine wengi Wote hawa wanaimba kizulu
 
Kwamba maeehemu aka

Casper nyovest

Costa Tec

Na wengine wengi Wote hawa wanaimba kizulu

Kama wanaimba kingereza kwanini hawajafika UEFA, WC, Grammys etc etc.. hapo ndo unagundua mziki sio lugha tu there's more to it. Ukiacha nchi kadhaa kama bongo na Kenya zinazoshobokea amapiano huko duniani mziki wao haupo kabisa. Hao wasanii inawezekana Dayamondi kawaacha mbali pamoja na kwamba anaimba Kiswahili tu.
 
Wasanii wenyewe ndio hawa kina Harmonize wako busy na matako?
 
Wasanii wenyewe ndio hawa kina Harmonize wako busy na matako?

TZ msanii ni Harmonize tu?

Vp enzi za Fella Kuti wa NG na kina Marijani bongo au the 2000s era maana hii tofauti haijaanza leo.

Nigeria hawapendi matako? Msemo wa Nyash ni wa nchi gani?
 
Kitu kingine
Watanzania tunapenda comfort zone yani mtu hata kwenda Kenya kutembea na kujaribu maisha hataki
Kila ukikutana na ndugu anakushauri uache kazi private uhakikishe unapata kazi serikalini
 
Kitu kingine
Watanzania tunapenda comfort zone yani mtu hata kwenda Kenya kutembea na kujaribu maisha hataki
Kila ukikutana na ndugu anakushauri uache kazi private uhakikishe unapata kazi serikalini

Kweli mkuu 🤣
 
Back
Top Bottom