Majibu Kwanini Wasanii Wetu Hawaitwi Kwenye Steji Kubwa Duniani

Majibu Kwanini Wasanii Wetu Hawaitwi Kwenye Steji Kubwa Duniani

Japo kuna mibata mzinga inayoendekeza ubishi itakuja kupinga hapa, lakini ulichoandika ni facts tupu.

Kubwa zaidi kuliko yote ni kwamba wa Tanzania tunaongoza kwa chuki binafsi. Hatuna mipaka ya ushabiki na hatujui kutofautisha chuki na ushabiki.

Wanigeria hata wakiwa mahasimu kiasi gani nyumbani lakini hata siku moja huwakuti wakikandiana nje ya kwao.

Kwetu hapa Diamond akichaguliwa kipengele cha kimataifa sisi wenyewe tukiongozwa na wasanii wetu ndio tunashika bango kumpinga na kuandika upuuzi mitandaoni.
Tunarajia kuitwa na nani ikiwa sisi wenyewe hatujithamin.

Daima charity begins at home.
 
Tu washamba sana na waoga.

Fikiria hata project nyingi tu za movie za Hollwood huwa wanatamani kuja kufanyia hapa ila unakuta vikwazo kibao. wanaamua kuacha na kuchagua sehemu nyingine.

Sad indeed.
 
Hivi vitu 4 ni vya muhimu sana:-
  • Lugha
  • Mpangilio wa shairi
  • Ujumbe wa shairi
  • Mdundo wa muziki

There's more to that—native English speakers umwambie asikilize conversation in Pidgin English hawezi elewa na hata nyimbo zao huwa hawaelewi wanacheza tu. Mimi mmatumbi mwenyewe huwa sielewi wanachosema kwenye nyimbo zao.

Unapokuja kwenye swala la technicalities za music tuna wasanii wengi sana wakali, mathalani, Ali Kiba, Barnaba, FidQ, Prof J, Jay dee, Rayvanny, Rama Dee nk nk. Hawa wote wana sauti, mashairi yamesimama na midundo mikali. Wamefika walipofika.

Vp Congolese na wasanii wa West Africa wanaoimba kifaransa kabisa wamefika wapi?

Music kama tasnia zingine is a team sport, huwezi toboa peke yako. Unapoishia wewe mwenzako inabidi akupokee au akushike mkono. Kuna wanigeria wengi kwenye boardrooms za maamuzi hence wanapeana mashavu.
 
"nyie" nyingii sana......wewe mtoa mada Raia wa wapi?

Mmatumbi halisi. Ukinisoma mstari wa mwisho nimesema Dayamondi, Samatta and the likes wanaenda kwa speed ambayo wabongo wengi hatujafikia including mimi. Badala ya kuwanyoshea vidole tujiangalie sisi kwa kuwa-let down.
 
point mkuu huwezi kushindana na walio wengi,
 mkiwa wengi mnaweza pia kuwashawishi wanaowazunguka,ndo maana huwezi shangaa foreigners wanatoa support kiasi kwa wanigeria,
lugha pia kikwazo ila ukweli wabongo wengi ni very talented,

huwezi kukuta wachekeshaji wa kibongo kwenye majukwaa makubwa ya stand up comedy huwezi kukuta mbongo amejaza 02 arena UK,
sababu ni mbili> lugha na uchache wetu ughaibuni„
japo pia tumejitahidi kiasi chake maana kuna nchi zina vyote hivyo lakini wapo nyuma yetu sababu ya lack of talent

sisi tuna vipaji ila tumekosa vichache

True.
 
Japo kuna mibata mzinga inayoendekeza ubishi itakuja kupinga hapa, lakini ulichoandika ni facts tupu.

Kubwa zaidi kuliko yote ni kwamba wa Tanzania tunaongoza kwa chuki binafsi. Hatuna mipaka ya ushabiki na hatujui kutofautisha chuki na ushabiki.

Wanigeria hata wakiwa mahasimu kiasi gani nyumbani lakini hata siku moja huwakuti wakikandiana nje ya kwao.

Kwetu hapa Diamond akichaguliwa kipengele cha kimataifa sisi wenyewe tukiongozwa na wasanii wetu ndio tunashika bango kumpinga na kuandika upuuzi mitandaoni.
Tunarajia kuitwa na nani ikiwa sisi wenyewe hatujithamin.

Daima charity begins at home.

I couldn't agree more mkuu. Let alone wanaija, Kenya tu hapa kila siku tunasema wakabila ila wakiwa nje wana ushirikiano wa hali ya juu. Sisi tofauti zetu ndogo tunazikuza na tunaenda nazo hadi nje.
 
Naandika huu uzi baada ya kumsoma kamikaze kwenye uzi wake: Mafanikio ya mwanamuziki Burna Boy, Nini tunajifunza!

If anything wasanii wakubwa wabongo inabidi wawalamikie watanzania wengine kwa kutokuwepo kwa wingi nje ya nchi hususani in the boardrooms.

Nigerians wapo wengi ndani na nje ya nchi yao. Unaposikia msanii wa naija kajaza ukumbi nje unakuta zaidi ya watu humo ndani ni Nigerians wenyewe. Unategemea Dayamondi ajaze ukumbi vp nje? Nyie wabongo mpo wangapi? Nani wakulalamika hapo dayamondi au nyie?

Nigeria ina timu ya basketball ambayo players wake wote wamezaliwa na wanacheza USA. Unashangaa vp msanii wa Nigeria kutumbuiza all-star game? Nyie bongo mna players wangapi NBA? Nani atawashika mkono huko NBA? Hapo wakulalamikiwa ni dayamondi au nyie wabongo wengine?

Nigeria ina hadi timu ya Bobsleigh sport, probably hujawahi usikia. Ni mchezo wa kwenye ice ila Nigeria hamna ice kabisa kama bongo tu, unadhani wanajuaje kuucheza? Players wake wote wamezaliwa na wanaishi USA. Utashangaa vp msanii wa Nigeria kuitwa kwenye function ya bobsleigh?

Bado NFL. Watu wenye asili ya Nigeria ni wengi kuliko kawaida kwenye huu mchezo. In a yr or two kuna msanii wa NG atatumbuiza kwenye superbowl believe me you. Nyie mna wachezaji wangapi NFL?

Kanu, Okocha, Ihenacho, Obi Mikel, Victor Moses na sasa Osimhen wa Napoli wote ni Nigerians, nyie wachezaji wenu wangapi wamefika UCL? Timu yenu ya taifa lini imeenda World cup? Bado unashangaa wasanii wa Nigeria kuitwa kwenye stage ya UEFA?

Viongozi wa Nigeria wamewahi na bado wanashika nyadhifa mbalimbali duniani more than any other country in Africa. Wapo kwenye boardrooms za maamuzi, nyie mpo wapi? President wa Toronto Raptors Masai Ujiri ni mnigeira, Ime Udoka aliyekuwa kocha wa Boston Celtics ni mnigeria. Unadhani wakiambiwa walete mtumbuizaji watamleta Marioo au msanii wao?

Kama you're reading btn the lines utagundua urai-pacha plays a big part as well. Wanigeria kibao wamezaliwa na kukulia nje including Burna boy mwenyewe aliyekulia UK, Davido kazaliwa US ila wanapeperusha bendera ya NG. Nyie mna uraia pacha?

If anything wasanii wetu wamefanya kazi yao, hawana deni kabisa. Dayamondi, Samatta na wasanii wengine walipofika ni juhudi zao binafsi and they can only do so much. Wanaenda kwa speed ambayo wabongo wengine hawana, we're letting them down. Hawawezi fanya kila kitu peke yao.

Nipo around mazee.
Tatizo ni bangi na umalaya ndio vinatukwamisha
 
Back
Top Bottom