Majibu ya damu yagundua mwanaume ana matatizo ya ugumba akiwa kwenye ndoa na watoto wanne

Majibu ya damu yagundua mwanaume ana matatizo ya ugumba akiwa kwenye ndoa na watoto wanne

Wakati unapigania maisha kuna dawa ni lazima waangalie allergy reaction kabla hawajakupa na katika kupima wakakuta jamaa ana rare condition kwenye damu, walichoshangaa watu wenye matatizo hayo huwa ni wagumba.
Dr mwenye akili huwa hasemi yasiyomhusu... especially kama halihusiani na matibabu.
Sasa hyo dawa na kutozaa ingehusiana vp
 
Sasa ilijulikane Kama watoto Ni wa houseboy baada ya hiyo ajali?
 
nao walikuwa wanatafuta nini hadi kwenda kugundua mambo ya ugumba?
Wanasayansi ni watafiti, walitaka kujua iweje huyu bwana amepata watoto akiwa na matatizo hayo, au kuna wengine wanaweza kupata watoto kwahiyo tafiti za awali zinaweza kutenguliwa.
 
Baba zao walikua maswaiba, katika kulinda mali za familia zao walipanga kuwaoza watoto wao. Binti hakuwahi kumkubali jamaa lakini kwake pia aliona ile ndoa ni life opportunity. Familia ya mume ilikua matawi ya juu.

Baada ya harusi mke alileta house boy nyumbani. Ni kijana mdogo ndiyo kwanza amemaliza kidato cha nne. Houseboy alipewa servants quarter na furniture zote alinunuliwa.

Kitu cha heshima alichofanya bibi yule ni kuto mruhusu houseboy kuingia kwenye matrimonial bedroom anayolala na mume wake. Lakini jamaa akiwa kwenye mihangaiko mama anakua kwenye servants quarter na houseboy. Lengo na madhumuni ni kupata watoto wenye sura nzuri kwani sura ya mume wake hakukubaliana nayo.

Mtoto wa kwanza alizaliwa na wa pili na watatu mpaka wakafika wanne. Katika kipindi chote hiki, mke alimhakikishia mume wake kuwa yeye ndiye Managing Director wa nyumbani kama alivyo mume katika biashara zake na wasiingiliane. Houseboy alifundishwa udereva na akawa anawapeleka watoto shule na kuwachukua. Jioni alicheza nao mpira na kuwafundisha shughuli nyingi kama kutunza bustani na kupanda maua na mboga mboga.

Maisha yalikua mazuri sana, ni zile familia ukiziona kwenye Range Rover yao ya 2021 unatamani maisha yao.

Mid term walipanga kwenda kupumzika Dubai, mume alikua na mkutano muhimu Morogoro, katika kukamilisha taratibu za uwekezaji huko. Alijijua asipofanya hima atachelewa ndege, hivyo kutoka Morogoro akiiimbiza Range, aliishia kupata ajali mbaya sana.

Mungu ni mwema alinusurika na kifo. Lakini wakati wa matibabu madaktari walichukua damu kwa vipimo vingi, ndipo walipogundua ana rare condition na wanaume wenye hii condition huwa ni wagumba sasa yeye ni baba wa watoto wa nne inakuwaje?

Uchunguzi ulianzia hapa, na wahenga walisema hakuna siri chini ya jua.
I don't buy this, Mtu anapoenda Hospitalini anapimwa magonjwa Mengi hasa Yale yanayoambukizwa Kwa Njia ya Damu lakini Majibu yanakua Siri ya Hospital unless mgonjwa amefanya Inquiry ya Majibu.

Sasa Kwa case ya Hii story Daktari anawezaje kumwambia mgonjwa ana rare condition na yawezekana ana Ugumba bila Mgonjwa kuuliza?

Sana sana hpo wataangalia kama dam imepungua, watampima Blood Group ili aweze kuongezewa, mifupa na sehem yyte nyingine ambayo pengine anaweza kua amedhurika.
 
I don't buy this, Mtu anapoenda Hospitalini anapimwa magonjwa Mengi hasa Yale yanayoambukizwa Kwa Njia ya Damu lakini Majibu yanakua Siri ya Hospital unless mgonjwa amefanya Inquiry ya Majibu.

Sasa Kwa case ya Hii story Daktari anawezaje kumwambia mgonjwa ana rare condition na yawezekana ana Ugumba bila Mgonjwa kuuliza?

Sana sana hpo wataangalia kama dam imepungua, watampima Blood Group ili aweze kuongezewa, mifupa na sehem yyte nyingine ambayo pengine anaweza kua amedhurika.
Inawezekana pia mmoja wa madaktari akawa mwanafamilia au kuwa na ujuzi wa kidaktari akaweza kuuliza maswali zaidi na akawa anajua madhara ya hiyo condition kwa wanaume.
 
Hivi stori ni za kwenye vitabu au ni za kweli maana naona unaleta story za aina hii mara nyingi au unachangamsha jukwaa
 
Back
Top Bottom