Majibu ya Dr. Masau wa THI kwa maswali mbalimbali

Tumekuwa wepesi mno wa kutumia maneno na sifa ambazo sio stahili, k.m. fisadi,kigogo, kubobea. Ili mtu ahesabike kuwa amebobea katika fani fulani ni kuwa amekuwa aki'practice' kwa muda mrefu na amefanya mambo ambao peers wake wanaona ni exceptional. Kutokana na maelezo yake mwenyewe, ingawa Dr. Masau ni qualified katika upasuaji moyo nadhani bado hajafikia kiwango cha kubobea ukizingatia kuwa ameweza kusimamia na kuongoza upasuaji wa moyo tangu hapo alipoanzisha taasisi yake maana kabla ya hapo hazikuwa zikifanyika nchini. Pamoja na kusema hivi, inawezekana kabisa kuwa kuwa amebobea katika surgery ya aina nyingine.
 
Fundi Mchundo,

..hii sakata ya Dr.Masau inanikumbusha maneno niliyopata kusikia kuhusu misukosuko aliyoipata Prof.Sarungi aliporejea Muhimbili toka Hungary.

..nasikia ma Fellow wa Royal Institutes of .... walimnyanyasa sana. aliyemsaidia na kumlinda ni Medical Superintendent[there was no DG then] wa Muhimbili wakati huo.

..wote tunaelewa kwamba Dr.Sarungi alikuja kuwa DG wa Muhimbili. pia yeye ndiye aliyeleta wazo la kuanzishwa kwa taasisi ya MOI.

..nahisi huyu jamaa anaweza kuwa ni "Sarungi" mwingine. siyo vizuri kuacha ujuzi wake ukapotea hivihivi.
 
can of worms zitafunguka humu mpaka mwenyewe atajuta kwa nini aliingia kwenye huu mjadal

kitu cha ajbu ni kuwa wana JF muda wa kufanya diligence check wanao as long as hakuna atakaye kutja kutaka kudilute hii thread
 
Topic inajifia yenyewe taratiibu.

Hakuna data zaidi. Wenye chuki zilch!
 

Mkuu kitila hata huko serikalini mbona ni mbali sana hata humu barazani watu wanakuwa wanashupalia udaku sana Yaani habari zisizokuwa na uhakika
Sasa kama amemaliza muhimbili kile ni chuo kinafundisha nini ?
Ilhali ukimaliza pale unaweza kutibu sasa kibay kipo wapi ?
Chonde chonde tupendane Jamani
Mtu akipata kazi nzuri wanasema kapata ulaji mimi sijui kabisa maana yake kabisa wanasahau degree ya responsibility atakayokuwa nayo
 
naona neno "kushiriki" linawakwaza baadhi ya watu humu.
japokuwa mimi si mjuzi wa fani ya utibabu/upasuaji ninachofahamu
kuna aina ya upasuaji ambao uhusisha wataalamu wa aina mbali
mbali (timu). katika upasuaji huu huwepo kiongozi wa upasuaji na ambaye
ambaye hujulikana kama "mpasuaji". wale wengine hujulikana kama
"washiriki.

binafsi sioni kama dr masau anacheza na lugha anaposema "ameshiriki"
upasuaji.
 
Ni Vizuri hii ni web comunication maana kama ingekuwa ni uso kwa uso, baadhi ya hawa jamaa zetu wanaoondoa elimu vichwani mwa wengine, lazima ningekwisha wauliza nini wanafanya na ni wapi walipata sifa hizo.

Utashangaa kwamba huenda wana mengi ya kugushi na sasa wanadhani hata wengine wako kama wao.

Naomba Mjadala huu uhamishwe toka UWANJA WA SIASA. Tulipofikia hayahusu tena siasa, it is just personal grudges to be more precise, UMBEA.
Ukijibiwa hili unasema na lile bado. Lile likijibiwa unarudi nyuma na kudai yasiyokuwepo.
 

Kitila.
Kwa bahati nzuri nimesoma vizuri mjadala wa walimu wa Mzumbe University wenye Phd FEKI, kutoka Marekani na wewe ulichangia vizuri sana kuwapinga na elimu zao, akaja Nungwi na kusema kuwa wewe una wivu na watu wa Mzumbe ambao wamefaulu vizuri Marekani, jee ulikuwa una wivu na chuo cha Mzumbe?

kinachozungumziwa hapa ni kuwa Masau kweli amesoma udaktari Muhimbili na China lakini hajawahi kuwa daktari anayetibu watu Marekani hilo mwenyewe kasema,Watu wengi hasa Mwanakijiji wanasema tumepata mtalaam aliyekuwa akitibu Marekani kwa miaka nenda rudi huo ndio uongo hatutaki uzidishwe.
Hivi sasa watu wengi wanatengeneza CV feki kuwa walikuwa wakifanya kazi Marekani au UK kwenye shirika fulani kumbe uongo.
 
Ukiwa na leseni ya udereva ya Tanzania huwezi kuendesha UK au Marekani bila kuwa na leseni au kupewa baraka za bodi zinazohusika na mambo hayo za UK au Marekani.

yaaani unazidi kujichoma ndani ya shimo la chooni, wewe omba radhi kwa Dr. Masau, ili yaishe maana haya unayosema sasa ni kusadikika, aibuuu tupu kwa mfano haya juu hapo nani aliyekuambia kuwa ni kweli?
 

Mkuu Kieleweke,

Heshima mbele, uliyosema hapa ndio yanayotakiwa kwenye kuweka heshima ya hii forum inapotaliwa, huyu mtu asitubabaishe na rangi zake 50 hapa, wewe umeshikwa kubali tu hapa JF hatuna peremende hapa tuna mawe ya ukweli umekosea muombe radhi Dr. Masau na uache hizi tabia za kurukia majina ya watu usiowajua, kila kukicha hapa matusi tu kwa watu leo yamekukuta aibuu kubwa ingekuwa ni mtaani tungekuzomea na kukupa singi za usoni, hilooooooo!

mzushi mkubwa wewe, mwanaume mzima kuja kusutwa mbele ya jamii huna hata aibu, huyu Doctor ukweli ni kwamba humjui na wala hujui lolote linalomhusu, hapa umejaribu sana kuharibu jina la Mwanakijiji, pamoja na Dr. Masau, kwa makusudi kabisa knowingly kuwa humjui na wala hujui kabisa habari zake, halafu huna hata aibu kujaribu kujifanya unajua sana kumbe nonesense tupu, ni ayako ni kuiharibu hii forum huna lolote,

Uache huu mchezo, Mkuu MMJ naomba umuombe radhi Dr. Masau kwa niaba yetu wote hapa JF kwa kumkosea adabu, mwambie ndio matatizo ya PHD za online kama za Nchimbi, unakuwa na muruwe ruwe tu kichwani huwezi kufikiri right, hujali wengine unajijali wewe tu, kila mtu mwingine ni mjinga, wenye akili ni wewe tu sasa unakuja kuwa humbled na masikini dokta wa watu, can you imagine wewe ungekuwa na power bongo, si ungeshamfukuza kazi huyu masikini wa Mungu, Dr. Masau?

Kwa mara ya kwanza I am ashamed kuwa forum moja na wewe mkuu, maana this is the worst aibu toka nijiumnge na hii forum, sasa niambie hivi Dr. Masau atasema nini kuhusu hii forum kokote anakokwenda? Halafu unajaribu kupindisha ukweli kama vile sisi ni watoto wadogo huna hata haya?

Muombe radh Dr. Masau, kama huwezi nyamaza kuna watu hapa watakuombea, lakini next time usilete matusi kwa watu bila ya kuwa na ukweli, maana hii uliyoifanya ni aibu yetu wote hapa JF. A spade is a spade akiongea uongo akisema uongo ni muongo tu hakuna neno tofauti hapa!

You are nothing but a cheap liar!
 

Haya ni maneno umeyasema mwenyewe, hakuna anayekusingizia hapa na hao wanaojaribu kukutetea uongo wako shame on them, hapa hukusema leseni ulkiyoyasema ni hayo juu yako very clear, kwamba ni uongo tena wa mchana na ni uzushi!

Muombe radhi Dr. Masau na wana forum wote kwa kumchafua jina kwa makusudi mzee wa watu.
 
Nina imani na daktari aliyemaliza na kupata shahada yake ya kwanza chini na hasa Muhimbili kuliko vilaza wanaoshindwa kuendelea na shule nchini wakazamia majuu na kurudi na misururu ya madigri. Mimi binafsi nawajua wengi tu walioshindwa hata kumaliza hiyo "O level" lakini wakaweza kuibuka baadaye na maPhd baada ya kukaa marekani miaka nenda rudi. Hakuna ubishi kuwa Dr. Masau alisoma Muhimbili na hili kwangu linatosha kumkubali.

Upasuaji wa moyo kwa sasa unaweza kufanywa kwa kuangalia tu TV sembuse ambaye anashuhudia live kama alivyofanya Dr. Masau. Nchi ambayo inaongoza sasa hivi kwa upasuaji wa moyo ni India na wataalamu wake wanaheshimika sana nchini Marekani. Hii inatokana na uzoefu wao wa kushughulikia wagonjwa wengi kwa wakati moja na daktari moja kwenye hospitali kuu ya India anaweza kushiriki kwenye upasuaji wa moyo kwa wagonjwa zaidi ya ishirini kwa siku moja. Kwa mfano Marehemu Dr. N. V. Mandke aliyekuwa bingwa wa upasuaji moyo India, aliweza kupewa tuzo ya pekee chini Marekani ambayo madaktari wengi hawana na alikuwa akiwa US anakuwa mgeni wa Surgeon-general (cardio) US.

Kuhani, game theory, maumau na wengineo ama nyie ni kama hao vilaza ninaoongelea au mna lenu hapa. Niliwahi kusoma kwenye shule moja ya ufundi marekani na nikaongoza darasa kwa theory na vitendo kwa kipindi chote. Cha ajabu wakati naongoza idara moja nchini nililetewa bosi mpya mzungu kutoka marekani - alikuwa si mwingine bali ni moja wa wanafunzi niliosoma nao darasa moja. Siku hiyo hiyo baada ya kumkabidhi ofisi nilitoa notisi ya kujiuzulu ya masaa 24 na huyo rafiki yangu pamoja na kushangaa alibaki anajiuliza kulikoni. Ukweli mchungu ni kuwa serikalini wamejaa hawa second grade material wakati vipanga wanasota kwingineko.

Bottom line - wataalamu wetu tunawanyanyasa mtindo moja.
 

Uzushi mtupu na ni aibu kubwa sana kwa mtu mzima, sasa muombe radhi Dr. Masau ili yaishe.
 

Wewe si mjanja wa maneno, sasa yabadilishe haya nayo umeyasema mwenyewe haya, na yote ni uongo mtupu tena wa mchana, shame on you kwa kumsingizia mzee wa watu, Mungu akubariki Dr. Masau uendelee na kazi yako ya kusaidia wananchi, kuna tunao heshimu sana kazi yako!
 

.......well said FMES...............hii forum tumetoka nayo mbali mkuu........heshima yake JF ni kitu muhimu sana......na huu upuuzi hauna budi kulaaniwa kwa nguvu zote.......
 


Tizama ulivyomchafua mzee wa watu, maneno mazito kama vile una ukweli kumbe ni majungu matupu na uzushi wa bila mfano, omba radhi tu kwa mzee wa watu Dr. Masau.
 
Halafu kila siku kulaumu vyombo vya habari vya Bongo, kwamba ni vitupu, yeye mwenyewe alipojaribu kutafuta habari, kashindwa hata kumuuliza mhusika mkuu, sasa sijui madai yake ana yabase katika kitu gani!

tulishamuonya, logic bila data wakati mwingine haitoshi, sasa anabaki kucheza na maneno
mara ooh dk Masau kasoma kwa kutazama tu, ghafla anakataa, eti mtu hawezi kusoma upasua moyo kwa kutizama, sasa sijui wale madenti pale muhimbili wanaohudhuria operation za wakufunzi wao pale wanakuwa hawasomi?.

labda wataalamu wa ufundishaji mtueleze kuna njia zipi zaidi za kusoma?
mimi ninazozijua

1:kusikiliza 2:kusoma vitabu 3:kutizama 4:kujadiliana 5:kutenda

kwa hiyo utaona hapo katika njia nilizozitaja upasuaji moyo utacombine hizo zote, sasa sijui kuhani anakataa kwamba kutazama dk anavyopasua yaweza kuwa ni njia mojawapo ya kusoma upasuaji vizuri zaidi kwa mtu anayeongeza ujuzi wake?
 
Nashangaa ile issue ya yule mgonjwa kupasuka kichwa pale THI kwa sababu aliwekewa gesi nyingi media wanajaribu kuifukia fukia
 
Haka kajamaa mau mau kana bore sana....mkuu mau mau kama umekosea kaa kimya tu ndio JF tulivyo au kubali yaishe......unarudia rudia kile kile mkuu.....
 
Haka kajamaa mau mau kana bore sana....mkuu mau mau kama umekosea kaa kimya tu ndio JF tulivyo au kubali yaishe......unarudia rudia kile kile mkuu.....

Yaani kwa sababu kauliza maswali ambayo huyapendi ndio anyamaze?

acha hizo...kila mtu humu yuko huru kuzungumza hata kama tunatofautiana kimawazo au ile WE DARE TALK OPENLY HUIELEWI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…