Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
Kitila.
kinachozungumziwa hapa ni kuwa Masau kweli amesoma udaktari Muhimbili na China lakini hajawahi kuwa daktari anayetibu watu Marekani hilo mwenyewe kasema
Sasa sisi ndio hapo tunauliza, kutokutibu America ndio kunamfanya asiwe daktari kamili? Sasa huu mtazamo si ndio wengine hapa wanauita kuwa ni ulimbukeni au siyo?
Nashangaa ile issue ya yule mgonjwa kupasuka kichwa pale THI kwa sababu aliwekewa gesi nyingi media wanajaribu kuifukia fukia
Yaani hoja zingine hapa ni vichekesho...Yani watu wameshaona ukisema umekaa marekani miaka mingi basi hiyo ndio hoja tosha!!?? Kwani ukikaa marekani basi wewe ndio unajua kila kitu? hivyi mnajua wamerikani (wazaliwa wenyewe) wengi tu ni so ignorant?
WAKATI mgogoro wa kodi ya pango kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Taasisi ya Moyo Tanzania (THI), nyaraka za kumchafua mwanzilishi wa THI Dk Ferdinand Masau zimesambazwa katika mtandao zikidai kuwa hana sifa ya kufanya upasuaji wa moyo.
Lakini Dk Masau amekanusha tuhuma hizo jana akisema ni za kubuni zenye ni ya kumchafulia jina lake kwa kuwa yeye ana sifa zote zinazostahili.
Nyaraka za kumchafua Dk huyo zilizosambazwa katika mtandao na watu wasiojulikana zinaeleza kuwa jina la Dk Masau halipo katika Bodi ya Madaktari ya Jiji la Texas nchini Marekani ambako yeye anadai alisomea.
Mwandishi wa taarifa hizo aliandika: "Nimeongea na wahusika wa Jimbo la Texas, kitengo cha Texas Medical
Board, pamoja na shule ya Dk. Masau, kitengo cha Texas Heart Institute, na nimethibitisha kwamba Dk. Masau hakuwahi kuwa mganga Houston, Texas.
"Jina lake halipo katika waganga waliowahi kuruhusiwa kutibu mtu Texas na kwamba elimu ya upasuaji moyo aliyoipata Texas Heart Institute sio "accredited program." Hata wakati anajifunza, hakuruhusiwa kugusa mgonjwa wa moyo ila kuangalia tu wanavyopasua.
Mwandishi huyo ambaye hakuweka bayana nia ya kufuatilia taarifa hizo, aliongeza kuwa, "Nimewasiliana na kampuni ya wanasheria ya Houston, Hartley Hampton P.C. kuangalia kama wanaweza kushughulikia hili suala. Wanajadili maombi yangu hadi hivi sasa tunavyozungumza,"
Dk Masau kwa upande wake, aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa ameziona tuhuma hizo kwenye mtandao na kwamba tayari amezijibu kupitia barua pepe kwenda kwa mtu aliyemuulizia kuhusu tuhuma hizo.
"Nisingependa kujiingiza kwenye malumbano au majadiliano yao na wala sipingi wao kuendelea na mijadala yao na hasa kwa vile wote siwajui na wanatumia majina ya kuficha," alisema Dk Masau.
Alisema watu kama hao ni wahuni wana lengo kumchafulia jina ingawa yeye anaamini kuwa atapigana vita hivyo mpaka mwisho bila kuchoka.
Alipoulizwa kama ana mpango wa kurudi kufanya kazi Texas na kuungana na familia yake kutokana na upinzani unaomkabili tangu alipoanzisha taasisi hiyo, alisema hana mpango wa kurudi huko kwani bado ana wito wa kuokoa maisha ya Watanzania.
Alisema Watanzania wengi wenye matatizo ya moyo wanateseka na kufa kwa kukosa huduma hiyo, hivyo ni wajibu wake kuwasaidia na ndiyo maana alirudi nchini na kwamba kama angehitaji kufanya kazi huko asingerudi kabisa.
Kuhusu elimu yake, Dk Masau alisema wakati anakwenda Taasisi ya Moyo Texas, alikuwa ameshamaliza masomo yake ya udaktari na kusajiliwa na Baraza la Madaktari Tanzania (MCT) mwaka 1995 kama mtaalamu mwenye Shahada ya Udhamiri katika upasuaji wa moyo, kifua na mishipa ya damu.
Alifafanua kuwa wakati akiwa hapa nchini aliwahi kufanyakazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) katika fani hiyo hadi alipoamua kwenda Texas mwishoni mwa mwaka 1996.
Alisema safari yake ya kwenda huko ilidhaminiwa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Jamii cha Texas Houston Januari 1997 hadi Juni 2000 na katika kipindi hicho alishiriki katika kufanya upasuaji wa moyo zaidi ya 1,800.
"Wakati nikiwa Texas sikuwa chini ya Bodi ya Madaktari wa Texas
na hivyo sikuhitaji kuwa na leseni kutoka huko na wala sijawahi kuwasiliana nayo, kwani ingekuwa na maana tu kwangu iwapo ningetaka kubaki na kufanyia kazi huko Texas. Mimi lengo langu lilikuwa ni mafunzo na kurudi nyumbani," alisema Dk Masau.
Dk Masau alisema bado anaendeleza ushirikiano mzuri na Texas Heart Institute na Texas Children's Hospital kiasi kwamba bado anashirikiana nao katika kufanya upasuaji pale anapoomba au kuhitaji na kwamba taasisi hizo mbili ni miongoni wa wafadhili wakubwa wa taasisi yake.
Kwa mujibu Dk Masau yeye ni mwanachama Chama cha Kimataiafa cha wapasuaji wa moyo ‘Society of Thoracic Surgeons' na mmoja wa wajumbe katika Kamati maalumu ya Chama hicho ‘Workforce of International Relationship of the Society of Thoracic Surgeons' tangu mwaka 2002 hadi mwaka huu.??
"Nimekuwa mwenyekiti wa Taifa ya kamati ya uandaaji wa Mkutano
Wa Tano wa kimataifa Barani Afrika unaohusu semina ya upasuaji wa moyo wa mwaka 2008 chini ya Mkurugenzi wa Mafunzo Prof Charles Yankah wa Taasisi ya Moyo Berlin, Ujerumani (BHI) na Chuo Kikuu cha Berlin pamoja na Dk. Willie Koen kutoka Christian Barnaard Memorial Hospital, Cape Town, Afrika Kusini.?
Katika hatua nyingine, alisema mwezi ujao amealikwa kuwa mgeni rasmi kushiriki katika mkutano wa ushirikiano wa nchi za Ulaya na Amerika unaohusu wataalam wa upasuaji wa kifua na mishipa ya damu unaolenga kujadili uwezekano wa kupata taarifa za awali kuhusu kuanzisha mfuko wa jamii ya wapasuaji wa kifua unaotambulika kama Mfuko wa Moyo Afrika (AHF).
Katika siku za karibuni Dk Masau amekuwa katika mgogoro na NSSF inayotaka kuhamisha wagonjwa katika taasisi yake kwa madai kwamba amekuwa halipi pango, jambo ambalo yeye analipinga na mgogoro huo bado uko mahakamani.
Yaani hoja zingine hapa ni vichekesho...Yani watu wameshaona ukisema umekaa marekani miaka mingi basi hiyo ndio hoja tosha!!?? Kwani ukikaa marekani basi wewe ndio unajua kila kitu? hivyi mnajua wamerikani (wazaliwa wenyewe) wengi tu ni so ignorant?
Quote:- Kuhani
1. Chochote alichosomea huko muhimbili na kwingine hakikuwa upasua moyo. Yeye mwenyewe anasema kwenye website yake kwamba kajifunza upasua moyo Marekani. Tatizo ni kwamba waliomfundisha Marekani wanasema huwezi kujifunza upasua moyo kwa kutazama tu.
2. Upasua moyo huwa ni residency ya miaka minne. Unapasua mioyo ya watu kwa miaka minne mafunzoni. Dk. Masau hakuwahi kugusa mgonjwa mafunzoni. Yani mafunzo yake hayakubaliki huko katika nchi aliyosomea.
3. Sasa kama hafai kupasua moyo wa watu wa huko alikosomea sisi ndio kuku wa yeye kujifunzia ?
4. Kuhusu success rate yake, data niliyoipata ni ya zamani. Alikuwa ana success rate ya 62% mwaka 2003. Na hiyo ni data aliyoitoa mwenyewe. Inaweza ikawa chini ya hapo, kwenye hamsini na.
5. Yani kwa wastani alikuwa akigusa wagonjwa wawili mmoja lazima afe!
Mkuu sizunguki mbuyu, wewe huna hoja hapa ila una kiroja, check this out, nimesema hivi mimi nimewahi kuishi USA miaka 20, kwa kutumia hiyo experience nikasema kuwa Kuhani ni muongo na ukweli umethibitishwa na Dr. Masau mwenyewe kuwa Kuhani ni muongo na mzushi kama nilivyosema kwa kutumia experience yangu ya kuishi USA miaka 20,
Kuhani amesema uzushi kwa kutumia gear ya kuishi USA, nimemwambia kuwa huko USA, alipokwenda alitukuta tayari tupo na tunayajua ya huko kuliko yeye aluyeenda majuzi tu, ukweli umejitokeza wazi kuwa ni mzushi na muongo,
Sasa hapa exactly, anayechekesha hasa ni nani kati yangu, wewe na Kuhani?
Upasuaji wa moyo kwa sasa unaweza kufanywa kwa kuangalia tu TV sembuse ambaye anashuhudia live kama alivyofanya Dr. Masau. Nchi ambayo inaongoza sasa hivi kwa upasuaji wa moyo ni India na wataalamu wake wanaheshimika sana nchini Marekani. Hii inatokana na uzoefu wao wa kushughulikia wagonjwa wengi kwa wakati moja na daktari moja kwenye hospitali kuu ya India anaweza kushiriki kwenye upasuaji wa moyo kwa wagonjwa zaidi ya ishirini kwa siku moja. Kwa mfano Marehemu Dr. N. V. Mandke aliyekuwa bingwa wa upasuaji moyo India, aliweza kupewa tuzo ya pekee chini Marekani ambayo madaktari wengi hawana na alikuwa akiwa US anakuwa mgeni wa Surgeon-general (cardio) US.
BP Biscuit Mane
Re: Dr. Masau ajibu hoja za Ndg. Kuhani
Quote:
Inatosha baba! Naona jinsi ulivyomkalia kooni Mzee Kuhani inaonyesha wazi una personal vendetta dhidi yake. Kumbuka kwamba Mzee Kuhani ni binadamu pia na anaweza kukosea kama ulivyo wewe! Utakumbuka jinsi ulivyopotosha wana JF mara kadhaa humu ndani lakini watu hatukuchuulia kama "big deal" au siyo? Mfano mzuri ni jinsi ulivyothibitisha tena kwa "Breaking News" kulingana na "dataz" unazozijua mwenyewe eti Mohamed Mpakanjia kafariki dunia wakati si kweli. Ama kweli Nyani haoni ku....
Kuhani Kuhani has no status. JF Senior & Premium Member Join Date: Wed Apr 2008
1. Bodi, shule ya Dr. Masau: Cheti chake hakimruhusu kupasua watu
2. Nimeongea na wahusika wa jimbo la Texas, kitengo cha Texas Medical Board, pamoja na "shule" ya Dr. Masau, kitengo cha Texas Heart Institute, na nimethibitisha kwamba:
1 ) Dr. Masau hakuwahi kuwa mganga Houston, Texas. Jina lake halipo katika waganga waliowahi kuruhusiwa kutibu mtu Texas.
2 ) Elimu ya upasuaji moyo aliyoipata Texas Heart Institute sio "accredited program." Hata wakati anajifunza , hakuruhusiwa kugusa mgonjwa wa moyo ila kuangalia tu wanavyopasua.
3. Ofisa wa hospitali aliyejitambulisha kama Dianne ameniambia "now, I don't know how much you can learn by looking..." Nikamwomba yeye ndio aniambie unaweza vipi kujifunza upasuaji kwa kutazama.
4. Akasema "He obtained a certificate from an unaccredited program ...... now I don't know how much good that certificate can do him in Tanzania,
5. but it's no good in Texas." Program hiyo inaitwaje, akasema "visiting physician in Cardiovascual Surgery" akizidi kurudia rudia kunitahadharisha kwamba ni unaccredited program, kama ambavyo tovuti yao inabainisha wazi.
6. SOURCES :
Texas Medical Board
Public Verification,
Licensure Verification
(512) 305-7030 au 1-800-248-4062.
http://www.tmb.state.tx.us/consumers...rification.php
7. Texas Heart Institute
Cardiovascular Anesthesiology Residency and Fellowship Programs
832-355-2666
http://www.texasheartinstitute.org/E...in/postdoc.cfm
8. Umuhimu wake ni nini?
Kwenye website yake, Dr. Masau anatangaza kwamba hapa Texas Heart Institute ndio amejifunza upasuaji mioyo. Lakini waliomfundisha, hawakumruhusu asogelee vifua vya wagonjwa wao, achilia mbali kwamba shule yenyewe haiko accredited. Hii ni hatari kwa wagonjwa wa Tanzania Heart Institute.
Cha pili, credibility ya Dr. Masau sio impeccable. Siku alipoulizwa kama mambo yakizidi kuwa na vikwazo ataondoka kurudi kufanya kazi Texas, alimjibu mwanahabari wa KLH News "ikibidi itabidi iwe hivyo." Wakati alijua vyema kwamba, sio tu hawezi kuachwa peke yake kwenye chumba cha kupasua moyo, ila haruhusiwi kumpa ushauri mkazi yeyote wa Texas anaejisikia mafua!
Unless, tumezoea kufa kufa na magonjwa na hatujijali tena, Dr. Masau hatakiwi apasue mtu moyo - waliomfundisha, officially, hawaruhusiwi kufundisha na hawakumruhusu!
Kama nilivyohofia, hili linaweza kueleza ni kwa nini hawakumpa koti jeupe siku ya kumbukumbu.
The Following 11 Users Say Thank You to Kuhani For This Useful Post:
Augustoons (2nd August 2008), GAME THEORY (2nd August 2008), Insurgent (4th August 2008), Juakali (1st August 2008), Masatu (2nd August 2008), Mauza uza (2nd August 2008), Mtuwamungu (2nd August 2008), Mzee Mwanakijiji (1st August 2008), Nyama Hatari (2nd August 2008), SteveD (1st August 2008), tzengo (2nd August 2008)
Narudia tena, kuhoji credentials ni wajibu wetu. Neno Kihiyo halikutoka hewani. Alikuweko. Sasa kama huyu mkuu ana'load' CV yake ni lazima aulizwe. Hii kukimbilia kila siku kumtetea mtu kwa vile tu ni mzalendo mwenzetu kutatufikisha kubaya.
I'm so done. Swali la msingi limeshabijiwa. Kuhamisha magoli kwa lengo la kukwepa kufungwa haisaidii. Wote tunakosea, wakati mwingine tunaandika vitu kwa jazba au tukiamini ni kweli. Na nina uhakika hata huko mbeleni tutakosea hapa na pale au tutatoa ripoti ambayo si sahihi.
Naamini Kuhani ameona hilo na sidhani kuna haja ya kumlazimisha aombe radhi kama hayuko tayari kufanya hivyo. Akiona ipo haja ya kufuta kauli yake ya kwamba Dr. Masau hajasomea upasuaji wa moyo (kumbuka ilikuwa ni blank statement, akiamini kuwa upasuaji wa moyo ni lazima kuwa angekuwa amesomea Marekani wakati amekuja). Jibu limepatikana.
Kilichonishtua binafsi ni ushauri wake alioutoa kwa mtu na kumwambia amuondoe mgonjwa mikononi mwa daktari halali na mwenye uwezo wote. Hilo lilinitisha na siamini kama Kuhani ana qualification ya kutoa ushauri wa kitabibu based on hearsay.
Mambo ya leseni na mengineyo natumaini yatarudi kwenye mada kuu, lakini suala la elimu ya Dr. Masau natumaini limeekuwa settled once and for all.
Nawashukuru kwa michango yenu mingi ambayo miingine kwa hakika imekuwa too personal and bordered on personality and character attacks. Tuendelee kukumbuka hoja hujibiwa kwa hoja, siyo vioja.
Na ninamshukuru Dr. Masau kwa kutumia muda kujibu hoja zetu kitu ambacho viongozi wetu wengine inakuwa mbinde. Leo hii tukimuuliza Nchimbi au Mkullo kuhusu elimu zao watakuwa tayari kutoa majibu yao kwa kina? I hope so. Vinginevyo, Dr. Masau amekubali kuja kwenye tanuru la moto na ametoka mzima.
Kwa upande mwingine namshukuru Kuhani kwa changamoto yake ambayo sidhani kama alitarajia ingeturn out this way lakini ametusaidia at least to establish ukweli kuwa mjadala wa Dr. Masau ubakie kwenye masuala ya Kodi.
Na hata hilo, tutashindwa kujadili sana kwa sababu kuna mchakato wa kisheria unaoendelea. Ingawa kuna watu wanataka alipe "kodi" alimradi mahakama ya chini imeamua bado kuna kesi zinaendelea mahakamani na ni vizuri tunapojadili tuache sheria zifuate tusije kujikuta kama ilivyotukuta kwenye mjadala wa Dr. Mwakyembe pale ambapo baadhi ya wanachama wenzetu walitaka tu "alipe" alichozushiwa kuwa anadaiwa asichafue jina lake.
Hadi mahakama ya mwisho kabisa itakapotoa hukumu, Dr. Masau ana haki zote za kuendelea kufanya shughuli zake na kupinga kitu chochote ambacho anaamini kuwa hatendewi haki yeye na THI.
m.m.
Leo mtahangaika sana, hiyo Breaking newss aliyeitoa sio mimi, ilitolewa na mtu mwingine, na unaweza kuitafuta uiweke hapa, maana hapa hakuna mate bro tuna wino tu, huwezi kuchukulia big deal habari ambayo sikuianzisha, sina vendetta na mtu yoyote hapa ila kama kawaida ninasimamia ukweli tena kiroho mbaya, kukosea ni one thing na kuzusha ni another thing, huyu amezusha kwa sababu alikuwa na nafasi nyingi sana za kubadili habari yake lakini akaendelea kutoa uzushi zaidi,
Kwenye ukweli nimesema siku zote simuogopi mtu, mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kumwambia kuwa huwezi kupiga simu Texas Medical Board ukapewa habari za mwanafunzi, lakini akajifanya much know sana, hebu tizama maneno yake hapa chini, haya sio ya kukosea haya ni uzushi wa makusudi, hivi umeshawahi kuifikiria familia ya Dr. Masau ambayo inaishi kwa kutegemea kazi ya huyu mzee aliyezushiwa, hebu soma hapa chini halafu uniambie kuwa ni kukosea:-