Majibu ya Nape Nnauye kwa Batuli kuhusu malalamiko ya bando la simu

Majibu ya Nape Nnauye kwa Batuli kuhusu malalamiko ya bando la simu

Watoto waliokulia ushuani huwa hawataki kutanya kazi sijui ni uvivu au uzembe au ni uwezo mdogo wa kufikiri?
Nape angenyanyua simu na kumpigia mkurugenzi wa tcra na kumuamrisha atoe mmaelezo.
Sasa huyu mama Kama Yuko Babati atoke huko halafu aje Dar aanze kuzunguushwa Kama vile anakesi ya michongo.
Nnape pick up the phone and call the tcra director..
 
Afadhali mimi natamani hizo billion. Magu kachota na kulamba zaidi ya Trilliona 30 hadi master wake shetani kashangaa nakusema WTF. Ikabidi tu atwaliwe kuzimu kabla ya siku zake.
Alikufi###$$ra kabla hajafa Mana kakukaa kichwani kweli
 
Tangu gharama zipandishwe kutoka 1000 1Gb kuja 500 Mb jamaa wananyonya sana bundle ukisinzia kidogo bundle limeisha wanadai ela nyingine
 
Nina mashaka na ufahamu wa huyu waziri.
Mlalamikaji ambaye ni mtumiaji wa huduma hakumtaja Rais, anatambua wazi zipo mamlaka zinazoweza kutatua hili.

Kusema
""tukitaka yeye ndio aje kushughulikia bundles atafanya mangapi?
aidha hakuelewa ujumbe na hakutaka kujipa muda wa kutafakari, au hajui yupo nafasi hiyo kwa ajili gani.
 
Hivi ndivyo staa wa filamu, Batuli alivyotumia ukurasa wake wa Twitter kulalamika kuhusu bando lake la simu, kisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akaingilia kati na kumpa ushauri wa kwenda TCRA.

=========

Ameandika Muigizaji Batuli

Hivi Kuna Mtu Mwingine Anapitia Hii Changamoto Kutoka Airtel Tanzania Au Ni Mm Tu…!? Jana Na Leo Hiyo 🙌🏽 Na Ukiwapigia Hawakupi Ushirikiano, Soma Ya Pili Hapo Uone Maajab. Hii Ni Siku Ya 4 Leo Nataabika Na Hili Kutoka Airtel Tanzania.

Hii Ilikuwa Monday, Imagine Wiki Haijaisha Leo Ni Alhamisi, Hapo Kwangu Natumia Wi-Fi Na Ofisini Natumia Wi-Fi Jana Nimewapigia Usiku Wamejivu Shit Sana Airtel Tanzania Huu Ni Unyama Na Dhulma Kwa Wateja



Nape Mnauye Amjibu Batuli

Ushauri wangu Batuli peleka kesi TCRA watachambua swala lako kitaalamu mbele yako na kukuonyesha mwenyewe, kama kuna wizi mahali tungefurahi kuchukua hatua. Rais ameweka watu kumsaidia na ndio maana inaitwa serikali, tukitaka yeye ndio aje kushughulikia bundles atafanya mangapi?

Batuli Amjibu Nape

Nitakwenda Jumatatu TCRA_Tz Kama Ulivyotoa Ushauri Mheshimiwa, Kiongozi Malalamiko Siyo Yng Tu, Hivi Watu Wote Hadi Wa Mikoani Huko Na Vijijini Wana Uwezo Wa Kwenda TCRA…!? Tunaomba Utatuzi Wa Changamoto Hii Yenye Kutuumiza Wananchi


Pia soma: Nape: Kampuni za simu haziibi vifurushi vya intaneti vya wateja
Nape anavyojibu kuwa sio kila kitu afanye Rais..wapi Batuli amemtaja rais amsaidie?
 
Mlivyo viazi mnahisi magufuli alikuwa wa maaan. Ndungulile na magufuli ndio waliotengeneza sheria za bundle za simu ziwe under TCRA. Na wanaoiba bundle ni TCRA sio hayo makampuni ya simu.
TCRA anaiba bando la nini? Na bando linakuaje la TCRA? Lengo la kusema waende TCRa ni sababu wao ndio wenye mamlaka ya hizo kampuni za simu,
Sasa akikwambia uende kwenye kampuni za simu hutaweza siadiwa kwa kuwa wao ndio unalalamika wamekuibia.
Ni Kama ambayo bus likikudhulumu unapaswa kwenda Latra
Ila ni kweli huwa akili hamna?
 
Majibu ya huyu zero waziri Nape hayana tofauti na majibu ya yule seti tupu mwingine Makamba alivyojibu hoja za umeme za Hon. Musukuma. Hizi zero kuteuliwa uwaziri ni majanga ya taifa. Haya makosa ya kuwateuwa hawa seti tupu chief Hangaya atajuta 2025.
Tuzidi kula mtori nyama tutazikuta chini.
 
Ningekuwa Nape ningepiga hela ndefu sana kwa makampuni ya simu. Yani kila mwezi kila kampuni lazima ziniletee billion kumi kesh mezani. Natena nitazidai kwa fujo violently vitisho.
Sikia bwana mdogo,sio lazima mpaka uwe kama Nape,hata hiyo ofisi ndogo uliyopo kama utakuwa na akili kama hizi utaanza kuishi maisha ya wasiwasi na kuviziana.

Maisha haya hayajawahi kutoa nafasi kwa ukuaji wa afya ya akili.

Akili na namna hii ndiyo uleta magonjwa lukuki na hatimaye vigo vya ghafla.

Kwa hiyo usije ukaona hao viongozi wana neema sana ila wanapitia magumu sana na wanapambana na mengi.

Tafuta pesa halali ishi maisha yako.
 
Nimesikia TTCL wameanzisha unlimited bundle,ila usikivu na net kwa sisi tulio mbwinde sina hakika.
 
huyo nape kajitoa mhanga wa kusafisha makampuni lkn ukweli wanaujua.
mm nilimtumia mtu salio toka tigo kwenda airtel ile salio halikufika na wala kwangu halikurud.anaposema tupeke ushadi ni watu wangapi wa wanatunza hizo kumbukumbu? basi mitandao iwe unatutumia voice note wanazorekodi tukiwapigia simu.
 
GB 11 atumie yeye na wateja kwenye ofisi yake kama Wifi na anataka zisiishe??😿😿😿😿😿😿😿
 
Watoto waliokulia ushuani huwa hawataki kutanya kazi sijui ni uvivu au uzembe au ni uwezo mdogo wa kufikiri?
Nape angenyanyua simu na kumpigia mkurugenzi wa tcra na kumuamrisha atoe mmaelezo.
Sasa huyu mama Kama Yuko Babati atoke huko halafu aje Dar aanze kuzunguushwa Kama vile anakesi ya michongo.
Nnape pick up the phone and call the tcra director..

Nape atakua ananyanyua Simu kwa kila mwenye malalamiko kwenda kwa Mkurugenzi TCRA wewe ungeweza ?

Waache wafate utaribu mh waziri afanye kazi nyingine
 
Back
Top Bottom