Majibu ya Postmoterm yaonyesha kwamba Hayati Ali Kibao alipigwa sana na kumwagiwa Tindikali

So sad
 
True
 
Unataka kusemaje? Kwamba your president alikuwa mtakatifu!?
 
RIP Mzee Kibao.
 
Hivi kwa matukio kama haya raisi Samia na wateule wake wnawezaje kupokea mishahara inayo toka kwenye kodi za wananchi na kwenda kufurahi na familia zao, huku walipa kodi hao wakiwa wanatekwa na kuuwaa na watu wanao paswa kuwalinda? Hii nchi imefikia kiwango cha kuongozwa na wendawazimu wa kiwango hiki? Ambao hawana hata akili ya kujuwa majukumu ya kazi zao . hawajari tena viapo vya kazi zao. Yaani tuna watu wameajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi ambao wanafikiri kazi yao ni kulinda watawala na sio wananchi? Hii nchi imefika mahali pabaya sana. Kwa hali hii tutegemee kuwa na madakitari wanao amini kazi ya udakitari ni kutafuta pesa kwa Wagojwa. Sasa mahospitalini tutaanza kusikia watu wameibiwa Figo kwaajiri ya kuuzia wenye hela. Tujiandae kuwa na walimu watakau pasisha wanafuzi kwa kuwa wametowa hela na sio kwa kuelewa masomo.
 
Magufuli ndio muasisi wa unyama huu. Kwa sasa ni muendelezo wa alichokuwa anafanya.
 
Swali ambalo linahitaji kujibiwa ni:
Ni sababu zipi hasa zilizo wakasirisha hao watu kiasi cha kuwa na unyama kama ule kwake. Alitukana viongozi? Alikuwa ni tishio kubwa sana kwa CCM?

Kwa nini akawa yeye?

Mbona alikuwa hafahamiki kwa watu wengi, hadi CHADEMA wenyewe walipo towa habari za yeye kutekwa!

Kulikuwepo na sababu nyinginezo mbali ya siasa?
 
Kwahiyo waliona wasirudie makosa ya Sativa wameona wamwagie na Tindikali kabisa?!
Mjini hakuna mamba wala mafisi walafi mkuu.

Hapo kuna mawili nadhani:
Yawezekana wauaji hawakupanga kumuulia mjini lakini marehemu akawaumbua.

La pili, hao wauwaji baada ya kuona wamemuua bila kukusudia wakatahayari na kukawa na mjadala wafanyeje ili kuharibu ushahidi, nd'o wakajichanganya na hiyo idea!

Lakini kwa kifo hiki sasa, Mungu ameamua waTz wote tuamke kutoka kwenye usingizini wa pono ili tumtambue adui yetu wa taifa.

Hili halina ujanja tena, sijui za kukamata mganga wa kienyeji eti naye kuua na kuzika watu wima ili kuua habari zakutekwa kwa Sativa na wale vijana wengine wa Chadema.

Safari hii mwizi katembea peku gizani lakini asubuhi wafuatiliaji wamemtambua kwa alama ya nyayo zake.

Ama mwizi wa pilau, kala kisha kasahau kunawa na kufuta mdomo, punje ya ubweche imeonekana dhahiri kidevuni pake.

Tusubiri tuone itakavyokuwa safari hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…