Kwahiyo waliona wasirudie makosa ya Sativa wameona wamwagie na Tindikali kabisa?!
Mjini hakuna mamba wala mafisi walafi mkuu.
Hapo kuna mawili nadhani:
Yawezekana wauaji hawakupanga kumuulia mjini lakini marehemu akawaumbua.
La pili, hao wauwaji baada ya kuona wamemuua bila kukusudia wakatahayari na kukawa na mjadala wafanyeje ili kuharibu ushahidi, nd'o wakajichanganya na hiyo idea!
Lakini kwa kifo hiki sasa, Mungu ameamua waTz wote tuamke kutoka kwenye usingizini wa pono ili tumtambue adui yetu wa taifa.
Hili halina ujanja tena, sijui za kukamata mganga wa kienyeji eti naye kuua na kuzika watu wima ili kuua habari zakutekwa kwa Sativa na wale vijana wengine wa Chadema.
Safari hii mwizi katembea peku gizani lakini asubuhi wafuatiliaji wamemtambua kwa alama ya nyayo zake.
Ama mwizi wa pilau, kala kisha kasahau kunawa na kufuta mdomo, punje ya ubweche imeonekana dhahiri kidevuni pake.
Tusubiri tuone itakavyokuwa safari hii.