Majimbo ya Ubunge yaliyosimamisha wagombea wa CCM bila wagombea wa Upinzani
Najiuliza tu "HIVI KUNA SEHEMU WA UPINZANI ATAPITA BILA KUPINGWA?"
HIVI HAWA WA CCM WANA UWEZO WA KUJAZA FOMU KULIKO WENGINE!?
Wqnajaziwana NEC...

Wewe ungekuwa ndiye mkurungenzi kisha chama chako kikaja na wamekosea sehemu uta kidisqualify?

Mimi ningewapitisha.
 
Wadau mpaka sasa nasikia CCM imeshachukua majimbo nane, namaanisha wamepita bila kupingwa. Yaani kabla ya hata ya kitufe kubonyezwa majimbo yafuatayo wapinzani wamenyanyua mikono na CCM wanayachukua.

CCM imepita bila kupingwa katika majimbo haya:
1. Misungwi,
2. Ruangwa,
3. Ushetu,
4. Morogoro Mjini,
5. Mvomero....
Hakika kwa utaratibu huu Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na tume huru ya uchaguzi inayojumuisha vyama vyote na taasisi za kidini ili kuwe na usawa katika utoaji wa elimu juu ya ujazwaji wa fomu kwa wagombea na uchaguzi kwa ujumla.Bado najiuliza tafsiri ya neno demockrasia na dhana nzima ya uchaguzi wa demockrasia na viashiria vyake.
 
Watanzania mazwazwa kweli kweli, hivi mnaamini na kukubali kabisa kuwa wapinzani wameshindwa kujaza na CCM wameweza? Hata habari za kutekwa na kunyang'anywa fomu hamjazisikia? Na wale waliowekwa ndani na policeccm hamna habari? Zero kabisa CCM!
 
Kwa hali hii Tz itaendelea kuwa nchi ya kilofa sana
 
Wadau mpaka sasa nasikia CCM imeshachukua majimbo nane, namaanisha wamepita bila kupingwa. Yaani kabla ya hata ya kitufe kubonyezwa majimbo yafuatayo wapinzani wamenyanyua mikono na CCM wanayachukua.

CCM imepita bila kupingwa katika majimbo haya:
1. Misungwi,
2. Ruangwa,
3. Ushetu,
4. Morogoro Mjini,
5. Mvomero,
6. Kilosa,
7. Mtama,
8. Gairo
9.Kongwa
10. Namtumbo
11. Kavuu
12. Katavi
13. Morogoro Kusini
14. Chamwino
15. Kondoa
16. Mpwapwa
17. Vwawa
18. Dodoma Mjini

Karibuni tuweke kumbukumbu za clean sheets hapa.

Updates

1. Mkoa wa Morogoro

Mkoa wa Morogoro una Majimbo 11 hadi sasa CCM Imepita bila kupingwa 6
- Jimbo la Kilosa
(Prof Kabudi)

- Jimbo la Gairo
(Ahmed Shabiby)

- Jimbo la Mvomero
(Jonas Vanzland)

- Jimbo la Morogoro kusini
(Innocent Kalogeris)

- Jimbo la Morogoro kusini mashariki
Hamis Tale Tale (Babu Tale)

- Jimbo Morogoro Mjini
( AbdulAziz Abood)

2. Mkoa wa Katavi
- Jimbo la Kavuu

Geophrei Mizengo Pinda

3. Mkoa wa Mwanza
- Jimbo la Misungwi

Alexander Mnyeti

4. Mkoa wa Lindi
- Jimbo la Ruangwa
Kassim Majaliwa

- Jimbo la Mtama
Nape Nnauye

5. Mkoa wa Shinyanga
- Jimbo la Ushetu

Elias Kwandikwa

6. Mkoa wa Dodoma
- Jimbo la Kongwa

Job Ndugai

- Jimbo la Chamwino
Deo Dejembi

- Jimbo la Kondoa mji
Ally Juma Makoa

7. Mkoa wa Ruvuma
- Jimbo la Namtumbo

Vita Kawawa
20
 
Hakuna resources wala nini
Mfano mtu anarudisha fomu mkurugenzi hayupo,mtu anaporwa fomu,
Hapo Tume/wasimamizi wanakosea Sana.. huwezi kumfanyia MTU unyama wa namna hiyo, watu wametumia resources na muda wao kwenye mchakato alafu unawafungia ofisi..huo si utu..hao wakurugenzi kwakweli wakifanyiwa Jambo Baya na watu wenye hasira hakuna atakayewaonea huruma
 
Hicho ndio kinashangaza sana siku zote ni upinzani tu ndio hawajui kujaza fomu kama sio kuendeleza uhuni wa kijinga ni nn? Waachie wananchi tuchague tunaowataka sio kutuletea wanaowataka wao
hivi ni wagombea wa upinzani tuu ndio wakosa vigezo?
NEC hili taifa tunalipenda sana maana hakuna sehemu nyingine nzuri kwa watanzania ispokuwa tanzania.
Acheni ngiriba za kupendelea chama kimoja dhidi ya vyama vingine.
mtenda haki hulipenda taifa
 
Mwenyekiti wako kajaribu kumuengua Lissu kimizengwe ila usalama wamemuambia asicheze na Lissu nchi itapinduka juu-chini
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Lisu aliwaambia jazeni vizuri ili yasitokee yale ya selikali za mtaa.

Naona hamkuelewa.
 
Inavyoonekana kujaza form ya NEC kwa usahihi ni vigumu sana kuliko kufaulu mtihani wa APPLIED MATHEMATICS hasa kama ulisoma BAM tu.
Wala si shida bali ni kujifanya wajanja. Sidhani kama mgombea Urais anazunguka kutafuta wathamini mikoani lakini haelewi kanuni zinataka wadhani kuhakikiwa na tume kwenye eneo husika? Ameipa kazi Tume yaTaifa Kuhakikia majina Dodoma siku ya kururisha fomu!!!
 
Haya sasa mpaka sasa ni majimbo 23 yamepita bila kupingwa.Upinzani hamkujifunza kabisa serikali za mitaa mmekalia kulalamika tu kila siku.
Mmeshindwa kudai Tume huru ya uchaguzi mnaingia kwenye uchaguzi mnasimamiwa na wakurugenzi ambao Magufuli anawachagua?

Hiyo "sasa basi " yenu iko wapi? Ninyi tulieni tu mkajipange upya.Tunaliona bunge jipya likiwa limejaa kijani tupu
 
Wqnajaziwana NEC...

Wewe ungekuwa ndiye mkurungenzi kisha chama chako kikaja na wamekosea sehemu uta kidisqualify?

Mimi ningewapitisha.
Ukiwapitisha ww sio final authority final authority ni NEC ndiyo wenye appelate jurisdiction
 
Watanzania mazwazwa kweli kweli, hivi mnaamini na kukubali kabisa kuwa wapinzani wameshindwa kujaza na CCM wameweza? Hata habari za kutekwa na kunyang'anywa fomu hamjazisikia? Na wale waliowekwa ndani na policeccm hamna habari? Zero kabisa CCM!
Usiwasemee watanzania wote, tupo ambao tumefurahi hao wa ccm kupita bila kupingwa kwenye hayo majimbolo
 
Hao wakurugenzi wapuuzi wa CCM wala hatuwasikilizi. Narudia tena hakuna muhuni yeyote yule kuanzia waziri mkuu mpaka muhuni wa mwisho kupita kihuni kama walivyofanya. Tutaimba nao kuanzia kesho!
Utafanyaje wewe?

Lisu aliwambia jazeni vizuri ili yasitokee yale ya selikali za mtaa nyie hamkuelewa
 
Ukiwapitisha ww sio final authority final authority ni NEC ndiyo wenye appelate jurisdiction
Nimeuliza kwa mfano wewe ndiye msimamizi wa uchaguzi hapo Morogoro.

Na chama chako ndicho chama tawala. Kisha mgombea wa upande wako akaja na fomu yenye makosa.

Je, ungemtoa kwenye uteuzi?
 
Back
Top Bottom