Majimbo ya Ubunge yaliyosimamisha wagombea wa CCM bila wagombea wa Upinzani
Nimeuliza kwa mfano wewe ndiye msimamizi wa uchaguzi hapo Morogoro.

Na chama chako ndicho chama tawala. Kisha mgombea wa upande wako akaja na fomu yenye makosa.

Je, ungemtoa kwenye uteuzi?
Siwezi kufanya upendeleo kwa sababu mimi siyo mchumia tumbo
Kwa mujibu wa taratibu za Tume, na ile kesi ya Bob Chacha wangwe ya kuhoji uhalali wa wakurugenzi kusimamia uchaguzi, walisema kwamba hao wakurugenzi wanakula viapo vya kujivua uanachama wa vyama vyao ndiyo wafanye hiyo kazi ya usimamizi
pili, mamlaka ya rufaa ipo ambayo ni Tume.
 
teh teh teh
Hamjiulizi, Mbona Halima Mdee, Sugu, Lema, Msigwa, Mwamba fomu zao hazijakosewa? kwa nini hao?
Biashara mkuu, wameshachukua chao mapema.
Kabla ya mapingamizi, wachunguzeni wagombea wenu kwanza
Hata ungekuwa wewe mkuu, ukijiangalia huna hata mia ya kukuwezesha kuzunguka jimbo zima kupiga kamoeni, sasa kwanini usichukulie zako milion 5 uendelee kula maisha kuliko kusubiri aibu ya kushindwa?
 
1. Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro una Majimbo 11 hadi sasa CCM Imepita bila kupingwa 6
- Jimbo la Kilosa
(Prof Kabudi)

- Jimbo la Gairo
(Ahmed Shabiby)

- Jimbo la Mvomero
(Jonas Vanzland)

- Jimbo la Morogoro kusini
(Innocent Kalogeris)

- Jimbo la Morogoro kusini mashariki
Hamis Tale Tale (Babu Tale)

- Jimbo Morogoro Mjini
( AbdulAziz Abood)
Hati wamepita bila kupingwa-majimbo 6 mkoa mmoja. Inafikirisha, nafikiri ni yale yale ya serikali za mtaa. CDM waweke mapingamizi tu. Bado ushenzi unatuandama.
 
Tutashuhudia mengi mwaka huu. Maana hata Tundu Lissu atapata kura chache sana
Kwani anauwezo wa kupata nyingi????? Kazi ndiyo imeanza atulie akiporomosha mitusi yake NEC inamhusu na jeshi la polisi.Eti kafurahia kupitishwa, hiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Nimechunguza kwa makini majimbo CCM waliopita bila kupingwa, ni kama vile kuna ufanano mkubwa sana.

Mengi ya haya majimbo ni ya watu masikini sana na wasioelewa kutetea haki zao.

Nilitegemea kwamba kipindi hichi ndicho ambacho wangesimama kidedea kuhakikisha wanakuwa na watetezi wenye maoni ya mbadala ya hawa viongozi wao waliokuwepo kwa sasa.

Matokeo yake, wapinzani wamekatwa na hamna kitu hawa raia wamefanya.

Inatia huzuni na hasira sana. Watu wamezidi unyonge sana mbele ya CCM na ndo mana wanazidi kutuchezea akili.

Wananchi tubadilike, tuache unyonge kwa wakoloni weusi wenye roho mbaya kushinda wazungu.

EgSV-1vWoAEAW8M.jpeg
 
Ha ha inashangaza sana.
Kwanini NEC wasitoe mafunzo maalumu ya ujazaji hizo form kabla ya zoezi wa ujazaji kuanza kwa uwazi na haki kabisa?
Mbona lissu kajazA??? Wagombea wenu majanga wanatia aibuuuuu
 
Siwezi kufanya upendeleo kwa sababu mimi siyo mchumia tumbo
Kwa mujibu wa taratibu za Tume, na ile kesi ya Bob Chacha wangwe ya kuhoji uhalali wa wakurugenzi kusimamia uchaguzi, walisema kwamba hao wakurugenzi wanakula viapo vya kujivua uanachama wa vyama vyao ndiyo wafanye hiyo kazi ya usimamizi
pili, mamlaka ya rufaa ipo ambayo ni Tume.
Wewe unaamini wakishaapishwa huwa wanauvua uanachama?
 
Yaani utafikiri lengo ni kupata mjazaji fomu bora, jamii inahitaji zaidi ya mjazaji fomu.

Wengine wanatekwa, wengine wanabambikwa kesi na wengine wanakataliwa kurudisha fomu, wengine wanapokea vitisho ili tu chama fulani kishinde.

Kisha utamsikia mwenyekiti wao, 'tutamngulize Mungu kwa kila jambo'. Naona wanambeep Mungu kwa kulitumia jina lake kufunika maovu yao, wacha tuone..

Bado tuna safari ndefu kama taifa, kujificha kwenye hila za kipuuzi namna ile then watu wanaamini hiyo serikali ina nia ya dhati ya kulipeleka taifa mbele.
Usisahau wasaliti wengi wameuza mchezo.Ni kawaida ndio maanake walikuwa wanazunguka na maform kufika bei.Upinzani wa kweli bado sana.
 
Huwezi kushiriki uchaguzi Kwa muda mrefu kama CCM walivyoshiriki na ukashindwa kujaza form, nadhani CCM Wana resources na experience kubwa compared to other parties ambazo to be honest vingine ata ofisi ya kujazia hizo forms hawana..kile kigezo cha kujua KUSOMA na KUANDIKA kitawaangusha wengi Sana..but I still believe NEC wako strictly Sana Kwa wapinzani kuliko wagombea wa CCM but still sio excuse ya wapinzani kuwa reckless katika kufuata maelekezo... Mpinzani kushinda have to be really on point bila dosari yoyote. Wanahitaji kuwa na usaidizi Mpana WA wanasheria ambao unfortunately they don't come cheap especially kipindi hiki.

Resources tunaona wote zinavotumika kuteka watu na kuwanyang’anya fomu ndiyo uzoefu huo wa muda mrefu. Watanzania wanaona kila kitu tumeona yaliyokuwa yanaendelea huku luangwa ili kupita bila kupingwa.
 
Morogoro na Dodoma mnatutia aibu taifa. Wananchi mmezidi unyonge. Siku mkiondoa huo unyonge hata maendeleo tutaanza kuyaona.

Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya unyonge na umasikini.

Acheni unyonge.

Mbona Mara hakuna aliyepita bila kupingwa? Jifunzeni humo.

Mnaaibisha
 
Back
Top Bottom