Majina ya sura zote 114 za Quran Tukufu kwa Kiswahili

Wewe unaweza kusilimisha jini?
Mfano haya yaliyozaliwa kipindi chako baada ya mtume?
Utajuaje kama limesilimu kweli au limedanganya?
Wao katika majini wapo waislam Wana silimishana wao Kwa wao ila hata Mimi naweza kumsilimisha jini ambaye amemuingia mtu akapandisha
 
Kumbuka mudy alikuwa kila siku anaulizwa aoneshe majini anashindwa , anawapiga soundi tu

Kuna siku aliwadanganya wenzake kwamba alikuwa na shetani kamfunga kamba
Yesu alivyotoa mapepo ambao ni majini waovu aliwaonesha?
 
Ukiwa muislamu automatically unakuwa mwendawazimu 😂
 
Haya yote yanatokea wewe ulikuwepo , ukishuhudia kwa mifumo Yako ya ufahamu ?
 

SURAT BIKRA 72
 
Wao katika majini wapo waislam Wana silimishana wao Kwa wao ila hata Mimi naweza kumsilimisha jini ambaye amemuingia mtu akapandisha
Kwa nini usilimishe jini aliyemuingia mtu. Kwa nini usimtafute yeye akiwa independent kama unavyosilimisha wakiwa independent.

Kwanza nikitaka kuonana na majini yakiwa yenyewe bila kumuingia mtu nayapata wapi kwa tanzania. Mfano nayaka kuyasilimisha.
 
Jini sio kiumbe Cha kuonekana Kwa macho.
 
Hadi sasa bado yanasilimu au ni kipindi kilekile cha Mohammad tu. Na je alikutana na majini yote duniani au machache ya hapo middle east. Jazia kidogo
Majini wanaishi kama tunavyoishi sisi, wanazaliana na kufa pia. Wana dini na lugha kama hivi tunavyozungumza.

wapo Majini Waislam
Wapo Majini wakristo
Wapo majini wanaofata dini ya kiyahudi.
Wapo majini wanaofata ubudha na umajusi n.k

Alikutana nao wengi tu...wengi walikuwa wakija kusoma dini kwake. Kiuhalisia majini ni wengi kuliko sisi wanaadamu. Tunapoishi wapo..wao wanatuona sisi hatuwezi kuwaona kwa macho haya.
 
Inasema alikutana na kikundi cha majini. Wapi? Na je ni majini yote duniani au ni kakindi kadogo huko alikokutana nao.
Alikutana nao wapi? Na je, ni majini yote au kikundi kidogo?

Mtume (S.A.W) alikutana na kikundi kidogo tu cha majini (idadi yao inatajwa kuwa kati ya 3 hadi 9). Tukio la kwanza kabisa lilitokea katika bonde linaloitwa Wadi Nakhla (lipo kati ya Makkah na Ta'if) wakati Mtume akisali usiku mara baada ya kufukuzwa na kupigwa mawe na wakazi wa mji wa Taif.

Baadaye, kulitokea mikutano mingine rasmi ndani ya mji wa Makkah (sehemu inayojulikana leo kama Masjid al-Jinn au Msikiti wa Jinn).

Kwa hiyo, hawakuwa majini yote duniani, bali lilikuwa ni kundi dogo ambalo baada ya kusilimu, lilirudi kuwaalika na kuwalingania majini wenzao duniani kote
 
Hao majini kabla ya kukutana nao walikuwa wanadini gani au walikuwa wanaamini nini
Kabla ya kukutana nao walikuwa na dini gani au waliamini nini?

Majini wana hiari (freewill) kama binadamu—kuna wema na wabaya. Kabla ya kukutana na Mtume, majini waligawanyika:
  • Wapo waliokuwa Mayahudi na Wakristo (kama Quran inavyoashiria katika Surah Al-Ahqaf aya ya 30, ambapo majini walisema wamesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa).
  • Wapo waliokuwa Washirikina au makafiri (waasi waliokuwa wakimfuata Ibilisi).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…