Majina ya sura zote 114 za Quran Tukufu kwa Kiswahili

Jini sio kiumbe Cha kuonekana Kwa macho.
Mtume alionana nao vipi
Majini wanaishi kama tunavyoishi sisi, wanazaliana na kufa pia. Wana dini na lugha kama hivi tunavyozungumza.

wapo Majini Waislam
Wapo Majini wakristo
Wapo majini wanaofata dini ya kiyahudi.
Wapo majini wanaofata ubudha na umajusi n.k

Alikutana nao wengi tu...wengi walikuwa wakija kusoma dini kwake. Kiuhalisia majini ni wengi kuliko sisi wanaadamu. Tunapoishi wapo..wao wanatuona sisi hatuwezi kuwaona kwa macho haya.
Kwako walishakuja kusoma chochote. Ulishawahi kukutana na Jini la dini gani na wapi? Au yanakutana na waislam spesho tu
 
Alikutana nao wapi? Na je, ni majini yote au kikundi kidogo?

Mtume (S.A.W) alikutana na kikundi kidogo tu cha majini (idadi yao inatajwa kuwa kati ya 3 hadi 9). Tukio la kwanza kabisa lilitokea katika bonde linaloitwa Wadi Nakhla (lipo kati ya Makkah na Ta'if) wakati Mtume akisali usiku mara baada ya kufukuzwa na kupigwa mawe na wakazi wa mji wa Taif.

Baadaye, kulitokea mikutano mingine rasmi ndani ya mji wa Makkah (sehemu inayojulikana leo kama Masjid al-Jinn au Msikiti wa Jinn).

Kwa hiyo, hawakuwa majini yote duniani, bali lilikuwa ni kundi dogo ambalo baada ya kusilimu, lilirudi kuwaalika na kuwalingania majini wenzao duniani kote
Umejibu vizuri kwa nukuu safi sana. Mkuu nimependa. Hiyo mikutano mingine na majini ina aya zake pia?
Kbal ya ubudha, Yesu na Mohammada yalikuwa na dini gani.

Majini ya kizaa mtoto tuseme watoto wa majini ya miaka ya 2000 wanasilimishwaje? Na nani anawasilimisha.
Kwa nini majini wasiwe na misikiti name hekalu na makanisa yao hadi waje wajibane huku kwa wanadamu mkuu.
 
Kabla ya kukutana nao walikuwa na dini gani au waliamini nini?

Majini wana hiari (freewill) kama binadamu—kuna wema na wabaya. Kabla ya kukutana na Mtume, majini waligawanyika:
  • Wapo waliokuwa Mayahudi na Wakristo (kama Quran inavyoashiria katika Surah Al-Ahqaf aya ya 30, ambapo majini walisema wamesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa).
  • Wapo waliokuwa Washirikina au makafiri (waasi waliokuwa wakimfuata Ibilisi).
Kabla ya mayahudi na wakristo maana wayahudi walianza baada ya Utumwa huko Misri na wakristo miaka 2000 iliyopita. Au dini zao zinafuata harakati za binadamu wao wanadandia kwetu
 
Wewe kama muislam umewahi kukutana nao. Na je uliokutana nao ni wale waliosilimu au waasi.
Mtume alionana nao vipi kama hawaonekani kwa macho?

Mwanadamu wa kawaida hawezi amwona jini katika umbo lake halisi la asili (kama Quran inavyosema: "Hakika yeye (Ibilisi) na qabila yake wanakuoneni, na nyinyi hamuoni" - Al-A'raf: 27).

Hata hivyo, Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa na uwezo huo kama Muujiza (Miracle) aliopewa na Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye alitumwa kuwa Mtume wa watu na majini yote (Thaqalayn). Pia, majini yana uwezo wa kujigeuza kuwa maumbo ya viumbe wengine (kama watu au wanyama), na katika hali hiyo wanaweza kuonekana.

Kutoka kwa Abu al-Darda (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema

"Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama kuswali, tukamsikia akisema: 'Najilinda kwa Allah kutoka kwako'. Kisha akasema: 'Nakulaani kwa laana ya Allah' mara tatu, na akanyosha mkono wake kama mtu anayetafuta kukamata kitu.

Tulipomaliza kuswali, tukamwambia: 'Ewe Mtume wa Allah! Tumekusikia ukisema maneno katika swala yako ambayo hatujawahi kukusikia ukiyasema kabla ya leo, na tumekuona ukinyosha mkono wako.'

Mtume akajibu: 'Hakika adui wa Allah, Iblis, alikuja na kijinga cha moto (flame of fire) ili akipenyeze/akiweke usoni kwangu. Nikasema mara tatu: "Najilinda kwa Allah kutoka kwako." Kisha nikasema: "Nakulaani kwa laana kamili ya Allah," lakini hakurudi nyuma mara zote hizo tatu.
Baadaye nikataka kumkamata. Na walahi (naapa kwa Allah), kama si kwa ajili ya dua ya ndugu yetu (Nabii) Sulaiman, asubuhi ya leo angekuwa amefungwa hapa kwenye nguzo ya msikiti na watoto wa watu wa Madina wangekuwa wanachezea naye."

(sahih muslim)

Mimi binafsi sijawahi kumuona Jinn katika umbile lake halisi ila nishawahi kumuona katika umbile la paka mweusi. Pia nishashuhudia wakiwa wameingia katika miili ya watu na nilipata wasaa wa kuhojiana nao.
 
Kuna muingoliano wowote kati ya majini na watu? Au unaushahidi wowote wa muingiliano wa majini na watu?
Kuhusu Muingiliano, katika Uislamu imekatazwa binadamu kufanya urafiki, kushirikiana au kufanya biashara na majini (mambo ya ramli, uchawi n.k). Ushahidi wa uwepo wao na mwingiliano wao na wanadamu upo wa aina mbili:
  • Ushahidi wa Kidini (Maandiko):
    Quran na Hadithi zilizothibiti zinaeleza uwepo wao.
*Ushahidi wa Kiuhalisia (Kijamii):
Kuingia kwa majini mwilini mwa binadamu (possession), maradhi yasiyoonekana hospitali, na matukio ya kichawi ni mambo yanayotokea kwenye jamii nyingi duniani (hata kwa wasio Waislamu) na ni ushahidi kwamba viumbe hawa wanajipenyeza kwenye ulimwengu wetu.
 
Je majini na haya tunayoyaita mapepo au mashetwain yanayuhusiano wowote?
Hivi vyote ni viumbe vya aina moja (vimeumbwa kwa moto), tofauti ipo kwenye tabia na majina ya kiutamaduni
  • Jini (Jinn): Hili ndilo jina la jumla la kiumbe huyu (kama neno "Binadamu"). Jini anaweza kuwa Muislamu mwema au kafiri.
  • Shetani (Shaytan): Huyu ni jini yeyote mwasi na mkaidi anayemfuata Ibilisi kufanya maovu. Hakuna shetani mzuri.
  • Mapepo/Subiani/Mahaba /maimuna / Makata n.k: Haya ni majina ya Kiswahili na ya kiutamaduni wanayopewa wale majini wabaya (mashetani) wanaowasumbua au kuwaingia watu na kusababisha maradhi au mambo ya kishirikina.
 
Uko serious kabisa? Hii huwa tunasoma for fun tu mkuu hamna wongofu humo.

Yesu alisema: “Tafuteni, nanyi mtapata” (Mathayo 7:7), na “Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Basi isome Qur’an kwa nia ya kuijua, si kuisoma kwa fun. Kisha tujadili aya kwa aya. 🤝
 
Mtume alionana nao vipi

Kwako walishakuja kusoma chochote. Ulishawahi kukutana na Jini la dini gani na wapi? Au yanakutana na waislam spesho tu
Huwezi kuwaona katika umbile lao halisi bali unaweza kuwaona endapo watavaa umbo la mnyama, mdudu ama mwanadamu.

Kila mwanadamu anapozaliwa huwa na rafiki wa kijini...unaambatana nae mpaka pale utakapokufa. Hata wewe unayeniuliza pia unae. Wapobwengi sana ni vile tu tumenyimwa uwezo wa kuwaona.

Makazi yao yapo kwenye majumba ya watu, miti mikubwa, misituni, kwenye majalala ya taka, vyooni, majangwani, baharini n.k
 
Mtume alionana nao vipi kama hawaonekani kwa macho?

Mwanadamu wa kawaida hawezi amwona jini katika umbo lake halisi la asili (kama Quran inavyosema: "Hakika yeye (Ibilisi) na qabila yake wanakuoneni, na nyinyi hamuoni" - Al-A'raf: 27).

Hata hivyo, Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa na uwezo huo kama Muujiza (Miracle) aliopewa na Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye alitumwa kuwa Mtume wa watu na majini yote (Thaqalayn). Pia, majini yana uwezo wa kujigeuza kuwa maumbo ya viumbe wengine (kama watu au wanyama), na katika hali hiyo wanaweza kuonekana.

Kutoka kwa Abu al-Darda (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema

"Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama kuswali, tukamsikia akisema: 'Najilinda kwa Allah kutoka kwako'. Kisha akasema: 'Nakulaani kwa laana ya Allah' mara tatu, na akanyosha mkono wake kama mtu anayetafuta kukamata kitu.

Tulipomaliza kuswali, tukamwambia: 'Ewe Mtume wa Allah! Tumekusikia ukisema maneno katika swala yako ambayo hatujawahi kukusikia ukiyasema kabla ya leo, na tumekuona ukinyosha mkono wako.'

Mtume akajibu: 'Hakika adui wa Allah, Iblis, alikuja na kijinga cha moto (flame of fire) ili akipenyeze/akiweke usoni kwangu. Nikasema mara tatu: "Najilinda kwa Allah kutoka kwako." Kisha nikasema: "Nakulaani kwa laana kamili ya Allah," lakini hakurudi nyuma mara zote hizo tatu.
Baadaye nikataka kumkamata. Na walahi (naapa kwa Allah), kama si kwa ajili ya dua ya ndugu yetu (Nabii) Sulaiman, asubuhi ya leo angekuwa amefungwa hapa kwenye nguzo ya msikiti na watoto wa watu wa Madina wangekuwa wanachezea naye."

(sahih muslim)

Mimi binafsi sijawahi kumuona Jinn katika umbile lake halisi ila nishawahi kumuona katika umbile la paka mweusi. Pia nishashuhudia wakiwa wameingia katika miili ya watu na nilipata wasaa wa kuhojiana nao.
Kwani Jini ni Ibrisi kwa aya hiyo?
 
Huwezi kuwaona katika umbile lao halisi bali unaweza kuwaona endapo watavaa umbo la mnyama, mdudu ama mwanadamu.

Kila mwanadamu anapozaliwa huwa na rafiki wa kijini...unaambatana nae mpaka pale utakapokufa. Hata wewe unayeniuliza pia unae. Wapobwengi sana ni vile tu tumenyimwa uwezo wa kuwaona.

Makazi yao yapo kwenye majumba ya watu, miti mikubwa, misituni, kwenye majalala ya taka, vyooni, majangwani, baharini n.k
Haya maelezo yanaaya yake kuwa kila mwanadamu anajini. Mimi naamini kila mwanadamu anamalaika sio jini.

Kama vitu havionekani kwa nini tunajihusisha navyo wakati haunaushahidi. Mimi sioni mtu mfano alafu namwambia kuwa muislam anasema nimekuwa kesho nitajuaje kama ni yeye au sio yeye au ananidanganya. Kwa nini tushughulike na vitu ambavyo hatunaushahidi na uthibitisho wa maamuzi yao?
 
Kuhusu Muingiliano, katika Uislamu imekatazwa binadamu kufanya urafiki, kushirikiana au kufanya biashara na majini (mambo ya ramli, uchawi n.k). Ushahidi wa uwepo wao na mwingiliano wao na wanadamu upo wa aina mbili:
  • Ushahidi wa Kidini (Maandiko):
    Quran na Hadithi zilizothibiti zinaeleza uwepo wao.
*Ushahidi wa Kiuhalisia (Kijamii):
Kuingia kwa majini mwilini mwa binadamu (possession), maradhi yasiyoonekana hospitali, na matukio ya kichawi ni mambo yanayotokea kwenye jamii nyingi duniani (hata kwa wasio Waislamu) na ni ushahidi kwamba viumbe hawa wanajipenyeza kwenye ulimwengu wetu.
Kwa nini Mungu akataze kuingiliana na majini wakati Quran inasema wamesilimu wengine. Sasa kwa nini Mungu abague waumini kwa misingi ya asili yao?
 
Yesu alisema: “Tafuteni, nanyi mtapata” (Mathayo 7:7), na “Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Basi isome Qur’an kwa nia ya kuijua, si kuisoma kwa fun. Kisha tujadili aya kwa aya. 🤝
Quran inaturudisha kwenye biblia kama kuna sehemu huelewi pia.

Sura ya Yunus 10:94
"Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka." [1]

Fafanuzi baadhi zinasema hao ji Manasara ( au thenashara au wafuasi wa Yesuau wakristo) na Wayahudi.

Na sisi iko wazi
Hakuna majini bali ni Malaika wasafi wa Mungu na Malaika wachafu wa shetwain ambao ndio majini,mapepo, mashetani.

Ndio maana kumtetea jini msafi kidini ni kazi ngumu sana ambayo hata shetani mwenyewe hawezi. Maelezo ya Surat jin ni mazuri ila yanaacha maswali mengi ambayo hakuna wa kuyajibu bila kuacha shaka.
 
Hiyo quran 10.94 wasomao kitabu hawapo tena , walikuwepo siku hizo ilipoteremshwa hiyo Aya , kwani hicho kitabu si biblia
 
Back
Top Bottom