Majirani zetu kutoka 'dona kantri', mnahitajika hapa kwa dharula. Hii nayo imepitiliza, ukizingatia zile mbwembwe za 'tunajenga kwa hela zetu'. Sijui tutaiitaje hii, hali mbovu ya mazingira ya kazi na huduma msingi kwa wananchi au ni utepetevu na ujeuri tu wa viongozi? Mbaya zaidi ni kwamba hawa ni watumishi wa umma ambao wapo karibu sana na chama tawala. Nimezoea kuona 'barracks' mbovu za polisi kutoka kwa nchi mbali mbali za Afrika. Ama 'police posts' ambazo huwa ni temporary wakati wa vurugu na ukosefu wa usalama. Ila kituo cha polisi, kama hiki, ambacho ndio sura ya serikali ni aibu kubwa. Sio kwa nchi ya Tz pekee yake, bali kwa ukanda huu na bara hili la Afrika kwa ujumla. Huu wimbo hapa, Run away- Gentleman una ujumbe kuntu sana, kwenu nyinyi wanakwaya kwenye jukwaa hili.
How long you a go run away, from yourself.