Makabila haya mtu ukifanikiwa jiandae kujaza ndugu tegemezi kwako ama kukuomba misaada kila mara, ukikataa unaonekana huna undugu

Nakumbuka kuna mama mmoja wa kizigua aliolewa na mtu wa huko tanga sasa yule mama alikuwa ana ndugu kama wote na mnajua maisha ya dar chumba na sebule sasa ata kubadili nguo ni changamoto sasa yule mjomba alivyoona mambo magumu akaitelekeza ile familia mpk leo hajarud kwake aliona hiki Kijiji ni shida.
 
tatizo ni ndugu tegemezi wasipenda kujishughulisha nao wajitegemee,
Wasambaa hawana hayo maisha ya utegemezi. Akienda kwa ndugu yake mjini, ni kwa ajili ya kupata hifadhi ya muda ili baadaye na yeye ajitegemee, na nyakati za sikukuu arudi nyumbani kusherehekea na wana familia wake
 
Waha ndio wanaongoza.
Hao uliowataja unawaonea tu.
 
Mbona siwaoni Wapogoro na Warangi hapo...

Kule Mbezi Mwisho kuna mtaa hadi umeitwa jina la mtaa wa Warangi, sababu ya kuitana hadi wakajaza mtaa...
 
Dah hayo maeneo uliyotaja umenikumbusha mbali sana.
Kakubilo, Nyambaya, Muharamba, Nzera, etc mananasi kama yote.
 
Watu wa Pwani ndyo zao nilikua naishi kwa brother angu dah ndugu wa mke walikua wanabadilishana tu ndugu wa mme nilikuwa mwenyewe lkn wa mwanamke walikua wanne Afrika mtu hadi atoboe kazi sana na hasa familia zetu hzi ni shida
#tujiandaekuhesabiwa#
Sasa wewe ulienda kuishi kwa kaka yako, Kufuata mila za watu wa pwani. Au wewe ndiye halali kuishi kwa mwingine.
Kilichokua kinawashinda kuja ndugu zako, ni nauli tu, ya kotoka mpiga giza mpaka Dar,
 


Weweee, acha roho mbaya!!!🤣🤣
 
wabena ndugu zenu ni wahehe,, hivi hii tabia ya kujifananisha na wakinga kwanini imeanza kushamiri baada ya wakinga kutoboa ? [emoji23][emoji23][emoji23] dah kwakweli aliewai kusema mkono mtupu haulambwi jakukoseaga
wabena umewaonea mzee.mbena hana tofauti na mhehe kuna usemi wao wanauita "Ndisina sida' manaake hawana shobo na vitu vya watu ni watu wa kujiridhikia na maisha yao.mimi sio mbena ni mtu wa visiwani huko ila nineishi huko na na nimesoma huko so nawajua vizuri
 
sina cha kusema umemaliza kila kitu well said mkuu.
 
Nadhani kutokana na utandawazi, mgawanyo wa sifa kwa makabila bado upo kidogo lakini unakwisha kwa kasi sana. Kikubwa ni aina za familia na koo tunazooa bila kujali ni za kabila gani.

Kwa mfano, mimi ni mtu ninayependa kukaa peke yangu muda mwingi, na kabla ya kuoa nilihakikisha natafuta mwanamke wa aina hiyo. Pamoja na hilo kumsisitizia zaidi nilimwambia nilivyo, na yeye akasema tunafanana.

Japo anatoka miongoni mwa makabila au jamii zinazotajwa zaidi kwenye huu uzi kwa utegemezi, ila yeye hayuko hivyo. Ninafahamu pia baadhi ambao wameoa kutoka makabila yasiyo na hizo sifa lakini wamejikuta wanashindwa kupanga maisha yao kwa kuelemewa na gharama za ulezi wa ndugu.

NB: Kinachozungumzwa sio kutosaidia ndugu, ni kutokuwalemaza wasifanye kazi wahamie kusubiri huduma kwa ndugu. Ndugu akiwa na shida atasaidiwa aliko, au akija isipite wiki awe hayupo.
 
Umetoa somo zuri sana, ukilipenda boga yakubali na majani yake, vijana wengi wanakurupuka sana kuoa na gharama ya kukurpuka wanailipa mpaka mauti wakiwa kwenye ndoa wanazojutia hawakufanya research ya kutosha zaidi ya kuangalia uzuri wa mwanamke ama shoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…