Hatukatai ndugu kuja shida mtu anakuja kukaa tu yani hawazi kazi wala nini,
Inavyotakiwa inabidi muwe na umoja lakini sio umoja wa kuanza kujazana na kuwa wategemezi, Kuna makabila hayawezagi kuvumilia mtu kuja kukaa awe tegemezi na wala si mgonjwa ama mzee, mifano mizuuri kama wachaga, wakinga, wakuria, n.k yaani kama wewe ni mgeni ukienda kwa ndugu utapokelewa vizuri tu lakini itabidi uwe umeshatoa taarifa juu ya ujio wako, shughuli iliyokuleta, ratiba yako ikoje, upo mpaka lini, mipango yako, n.k. kama ni kusalimiana wiki 2 zinatosha, sahau kuweka kambi hapo ya kudumu.
Kimbembe kipo kuna makabila wakishaona mwezao katoboa mjini, basi ndugu zake ama ndugu wa mke huhamishia kambi huko ,... wanakula na kulala hapo bila kazi maalum [emoji28][emoji28]
Makabila haya kwangu niliyoyaona ni kama.
. Watu wa pwani - wazaramo, wasambaa, wadigo
. Wanyakyusa - hawa huwa wanaendeleza undugu hata ule wa mbali, hata mke wa mjukuu wa baba mdogo wa babu bado anahesabiwa kama ndugu, kawaida sana kukuta mnyakyusa ana ndugu 100
Wabena , warangi, wanyamwezi na wagogo,
Kuna ile kujificha nyuma ya kivuli cha undugu lakini inakuwa inazidi sasa, mtu anaridhika miaka inaenda yupo tu