Makabila haya mtu ukifanikiwa jiandae kujaza ndugu tegemezi kwako ama kukuomba misaada kila mara, ukikataa unaonekana huna undugu

Makabila haya mtu ukifanikiwa jiandae kujaza ndugu tegemezi kwako ama kukuomba misaada kila mara, ukikataa unaonekana huna undugu

kama haujawaweka wanaSingida na wamburu bas utafiti wako ni hewa. Singida on top wale watu kiasili wapo ivyo.
 
Makabila ya watu wakarimu yote wanajali sana undugu, huwa hawajali sana vitu kama msosi, sijui maisha magumu wao ndugu akija nyumbani kwake anafurahi tuu wala haoni tabu.
kwakwel hii hali nimeikuta kwa wasambaa, mwaka 2016 niliwahi kwenda usambaani uko lushoto kijiji cha kileti jirani na lukozi, yaan wale watu ni wakalimu adi unaogopa, mgeni haujihis mpweke kabisa yan. misosi kwao sio tatizo ata kidogo wanamoyo wa kutoa, siku naondoka icho kiPASSO kilijaa viazi adi spring zikawa zinagonga
 
Ukonga Mombasa hii hii nnayoijua mimi au Mombasa ipi mkuu?
Bwana bure wewe jiandae tu utapakuliwa pilau wakati unasubiria vingine.
Mombasa ya Ruto ndio kwenye hivyo vya bure ukipenda na mtaa ni mwembe basha.
 
Kwa wasambaa nimeishi nao hili nakubali [emoji3] dingi yangu mkubwa alioa huko. Mzigo anao kiaina basi ndugu hawakauki hasa dada wa mkewe na nahisi wengine aliwagonga [emoji23][emoji23][emoji23] maana mzee wangu baharia yule!
Alijilipa sio
 
Ambao nina uhakika nao kujazana kwa ndugu:
-Wasambaa
-Wazaramo
-Watu wa kusini

Ukioa huko jiandae kisaikolojia 😂😂😂
Ukisema Watu wa kusini huja-specify but ume-overgeneralize na kiuhalisia mpaka naondoka Tanzania watu wa mtwara na masasi hawana hizo shobo sijawahi kuziona abadani labda watu wa Lindi 😂
 
Umewasahau wasukuma..

#MaendeleoHayanaChama
Wasukuma sio kweli,sema wao wanaweza kuja hata watano kwa mkupuo yaani baba na Mama mkwe,shemeji zako kama watatu na watoto wao kama watatu,hawajui watalalaje hiyo haiwahusu na watakaa si zaidi ya siku 3/5 na ninachowafurahia Wasukuma watakuja kwako baada ya mavuno kule kwao means wanakuja kwako huku wamebeba vyakula vya kutosha,so utakuta wamekuja na 100kgs za mchele,debe 5 za udaga, nanasi,mihogo mibichi na manumbu plus maharage, nk. Huu ndo ugeni wa Kisukuma ambao haukupi kinyongo,halafu raha nyingine kati ya ugeni huo km kuna shem wa maana unaweza pita nae bila noma.Aisee mimi nina uzoefu na hii jamii kwani nimeoa huko hawajawahi kunichosha.Hata waje 10 nitawapokea Kwan mara zote msukuma akija kwako anakuja kwa upendo na ni watu wa kazi km una mashamba hawezi kukubali uamke asubuhi umuache ndani amelala wewe uende shamba,atawajibika nawe shambani mpk siku anaondoka unaona kabisa kuwa huyu ndo mgeni haswa
 
Mimi ni mzaramu na kitu kuhusu wazaramu ni karibu wote wamezaliwa mjini yaani Dar es salaam na hakuna mji mwingine ambao unaweza kuitwa mji zaidi ya Dar es salaam.
Nimezaliwa kariakoo na ndugu wote wamesambaa Dar nzima na kila mtu anaishi kwake.

sasa sijui ni "kutoboa mjini" kwa aina gani unakoongelea mpaka mtu atoke kwake ambako ni mjini aende kwa ndugu ambaye anaishi mjini hapohapo.
That's what I know for sure about my tribe, hayo makabila mengine siwezi ongelea sababu mtu mwenye akili timamu hawezi kuongelea kitu ambacho hakijui.
 
Wasambaa kupendana na kubebana sana haswa mijini wacha kusema kujazana wanabeba na wanapenda kujitafutia katika umri mdogo sana
 
Ila kuna Wahaya jamani[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwanza kitendo cha kuja kwake bila taarifa,umekwishaaa!!!Hawanaga aibu,chakula kwa mhaya kinamuumiza sana ni heri kidogo mhaya wa kijijini anaweza kukuvumilia coz utakula vinavyotoka shambani but jichanganye eti unaenda kwa Mhaya aishie town na hasa Dar! !Ukibahatika sana utakaa 3 dayz tena za kupewa makavu live kila siku,ukiondoka hapo kamwe hutokuja ukanyage pale tena
 
Msukuma aache kuchunga ng'ombe aje kwako!!!
Hapo kwa wasukuma katuongopea jamii inayopenda kujazana kwa ndugu ni Ile jamii yenye njaa, msukuma Hana njaa na ndio maaana wasukuma wengi wapo masham huubani kwao uko hawajakimbia jamii zao nakuja jazana mjini kwa kazi za kuunga unga kama waha kutoka kigoma,au wakulya kutoka musoma

Pili mnyamwezi ukiona yupo kwa ndugu basi ni dada yake au kaka yake mnyamwezi Akai kwa ndugu wa kuunga unga wale watu Wana umaskini jeuri sana yupo radhi arudi kwao akalale chini siyo kukaa kwa ndugu anayemsimanga au mtesa kwanza wavivu kwaiyo kukaa kwa ndugu wa kuunga unga hawezi

Mnyakyusa yeye hana aibu kujipendekeza kisa tu boss furani au yule mnyakyusa pamoja na ukabila ni watu wasiojua kusaidiana wanatabia ya kujisnitch wao kwa wao ndio maana suala la kaka kutembea na mke wa mdogo wake au dogo kutembea na mke wa kaka yake ni kawaida kwao au ndugu kwa ndugu kujihusisha na mahusiano kwao kawaida
 
Wanyakyusa wanaupa undugu uzito mkubwa sana hata uwe ule ambao ni wa kizazi cha babu zake,,,, yani hata mjukuu wa mke wa baba mdogo wa babu si ajabu undugu ukawa unaendelea hapo, wanyakyusa wameendekeza sana undgugu, hii inapelekea hata kujazana kwenye nyumba
Kweli kabisa. Kwa Wanyakyusa Umepatia.
 
Back
Top Bottom