Hapa hatuzungumzii upendo au kujaliana, NO! Tunazungumzia ile tabia ya watu kujazana kwa ndugu, kaka, dada zao bila shughuli rasmi za kimaendeleo.
Hali hii imewafanya ndugu zao wanaowalea wamejikuta wanashindwa kupanga maisha yao kwa kuelemewa na gharama za ulezi wa ndugu. unakuta mtu kakaa hata miaka miwili kwa ndugu na ni kijana mwenye nguvu ila bado hajahama kujitaftia pake na wala hana shughuli za kimaendeleo.
Nyuma ya hii tabia hakukosekani visingizio vya oh tuna umoja, oh tunajaliana, oh sisi wakarimu, n.k lakini haibadilishi uhalisia wa hii tabia ya utegemezi.
Inavyotakiwa inabidi muwe na umoja lakini sio umoja wa kuanza kujazana na kuwa wategemezi. Kuna makabila hayawezagi kuvumilia mtu kuja kukaa awe tegemezi na wala si mgonjwa ama mzee.
Mfano mzuri kama wachaga, wakinga, wakurya, n.k yaani kama wewe ni mgeni ukienda kwa ndugu utapokelewa vizuri tu lakini itabidi uwe umeshatoa taarifa juu ya ujio wako, shughuli iliyokuleta, ratiba yako ikoje, upo mpaka lini, mipango yako n.k. Kama ni kusalimiana wiki 2 zinatosha, sahau kuweka kambi hapo ya kudumu.
Kimbembe kipo kuna makabila wakishaona mwezao katoboa mjini, basi ndugu zake ama ndugu wa mke huhamishia kambi huko. Wanakula na kulala hapo bila kazi maalum 😅😅
Makabila haya kwangu niliyoyaona ni kama;
. Watu wa pwani - wazaramo, wasambaa, wadigo
. Wanyakyusa - hawa huwa wanaendeleza undugu hata ule wa mbali. Yaani hata mke wa mjukuu wa baba mdogo wa babu bado anahesabiwa kama ndugu, kawaida sana kukuta mnyakyusa ana ndugu 100
. Waha, warangi na wagogo,