Makala maalumu ya historia ya Tundu Lissu: Ni hasa huyu mtu? Mambo saba (7) usiyoyajua kumhusu

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
4,249
Reaction score
11,592
MAMBO SABA USIYO YAJUA KUHUSU TUNDU LISSU.
-
Courtesy: BBCSwahili.com​
Katika historia ya siasa za Tanzania, ni vigumu kutaja majina ya wanasiasa walioteka hisia za watu kwa hoja, ujasiri na misimamo bila kumtaja Tundu Antiphas Lissu.

Kwa wengi, yeye ni alama ya mapambano ya haki, demokrasia na uwajibikaji wa serikali. Kwa wengine, ni mpinzani mkorofi anayependa kugonganisha fikra na utawala.

Lakini kwa wengi, Tundu Lissu ni sauti isiyotetereka katika mapambano ya haki, uwajibikaji na utawala wa sheria.

Hivi sasa, akiwa amewekwa rumande kwa tuhuma za uhaini ambazo kwa sheria za Tanzania hazina dhamana, jina la kiongozi huyu wa chama kikuu cha upinzani limerudi tena kwenye vichwa vya habari kitaifa na kimataifa, lakini hii si mara ya kwanza kwani Lissu ni mtu wa historia ndefu sana toka miaka 1990s

Ili kumuelewa kwa undani Lissu ni muhimu kumtazama kwa jicho pana: ni nani hasa huyu mtu? Haya hapa ni mambo saba muhimu yanayomtambulisha.

01. Msomi aliyelelewa kwenye taaluma na tafakuri ya sheria.

Tundu Lissu ni msomi wa sheria mwenye taaluma pana na ya kina wa kiwango cha shahada mbili (Masters), aliyezaliwa katika kijiji cha Mahambe wilayani Ikungi, mkoa wa Singida - Tanzania na kusoma sekondari ya awali (O'Level) katika Shule ya Sekondari ya Ilboru, Arusha (shule ya wanafunzi wenye vipaji maalumu kiakili) na baadaye Elimu ya juu ya sekondari (A'Level), Shule ya Sekondari Galanos iliyoko Tanga

Alipata Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1994, mojawapo ya taasisi kongwe na zenye heshima kubwa Afrika Mashariki na baadaye kufanya shahada yake ya pili ya sheria nchini Uingereza

Hapa ndipo alipoweka msingi wa uelewa wake wa kisheria, hasa kuhusu haki za binadamu, utawala wa sheria na uwajibikaji wa taasisi za dola.

02. Lissu alianza kujitambulisha kama mwanaharakati kabla hajavaa rasmi koti la kisiasa.

Tangu miaka ya 1990, alikuwa mstari wa mbele katika kutetea wananchi waliokuwa wakinyanyaswa na mfumo wa sheria usio wa haki.

Aliwahi kuwa mshauri wa kisheria wa mashirika kama vile Legal and Human Rights Centre Environmental Law Alliance Worldwide na pia alikuwa mjumbe wa Bodi ya International Federation for Human Rights.

Kazi hizi zilimuwezesha kushughulika na kesi zinazohusu mazingira, haki za binadamu, ardhi na uwajibikaji wa makampuni ya kimataifa barani Afrika.

Kama wakili alitoa msaada wa kisheria kwa watu wanaoishi katika mazingira ya uchimbaji madini walioathiriwa na ufukuzwaji ktk ardhi zao lakini wasio na uwezo wa kugharamia huduma hizo na hivyo kujijengea jina kama mtetezi wa wanyonge

03. Mwanasiasa mshawishi na mwalimu wa kujenga hoja.

Akiwa bungeni, Lissu alitokea kuwa mmoja wa wabunge wenye ushawishi mkubwa.

Alijijengea heshima kubwa kama mzungumzaji mahiri, mwenye uwezo wa kutoa hoja nzito zenye mashiko ya kisheria na kitaalamu.

Alipewa nafasi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambapo aliongoza mijadala mizito kuhusu bajeti, sheria kandamizi, masuala ya madini na mikataba mibovu ya serikali.

Alijulikana kwa kutumia takwimu, nyaraka na vielelezo thabiti katika kuibua hoja, jambo lililowafanya wabunge na wananchi kumheshimu hata kama hawakukubaliana naye.

04. King'ang'anizi mwenye matumaini na asiyekata tamaa

Mojawapo ya sifa kuu inayomtambulisha Tundu Lissu ni kuwa mtu mwenye matumaini yasiyotikisika na kutokata tamaa, hata katika mazingira ya hatari au kukataliwa na kukimbiwa na wenzake.

Lissu amekuwa mstari wa mbele katika kudai Katiba mpya ya Tanzania kwa zaidi ya muongo mmoja, akiitazama kama msingi wa haki, uwajibikaji wa watawala, na ujenzi wa taifa lenye misingi ya demokrasia ya kweli.

Alianza kampeni hii akiwa bado Mbunge na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, akihudumu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete 2005 - 2015

Wakati baadhi ya wanasiasa walijitoa au kukata tamaa kutokana na changamoto zilizokumba mchakato huo, Lissu aliendelea kusimama imara hata baada ya Bunge hilo kuvunjika bila kufikia muafaka wa kitaifa.

Katika kila jukwaa la kisiasa, iwe ndani ya nchi au akiwa uhamishoni baada ya jaribio la mauaji, Lissu ameendelea kuhubiri umuhimu wa Katiba mpya.

Hata katika kampeni yake ya urais mwaka 2020, suala la Katiba mpya lilikuwa mojawapo ya nguzo kuu ya ajenda yake.

Alikuwa akirudia mara kwa mara kuwa, "Katiba ya mwaka 1977 ni Katiba ya chama kimoja, haikidhi mahitaji ya taifa la vyama vingi," akisisitiza kuwa bila mabadiliko ya msingi ya kikatiba, uchaguzi wowote hauwezi kuwa huru na wa haki.

Hadi leo, anapokumbwa na kesi nzito ya uhaini kutokana na msimamo wake wa "No Reform, No Election", anaendelea kusisitiza kuwa Tanzania haiwezi kusonga mbele bila katiba mpya ya wananchi.

Kwa Lissu, unaweza kumuita king'ang'anizi anapolitaka jambo lake, na muhimu zaidi ni kuwa, matumaini, imani itendayo kazi, uelewa wa maarifa mapana aliyonayo ktk mambo anayosimamia ndizo silaha zake za hatari na muhimu ambazo huangusha mlima wowote ulio mbele yake. Haamini katika kukata tamaa wala kushindwa kwa jambo lililo haki, bali katika kusimama imara hadi haki ipatikane.

Katika kampeni ya No reform no election ambayo sasa inaongozwa na Makamu mwenyekiti wake chadema, Ndugu John Heche, imekuwa ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa Tume huru ya uchaguzi, siasa safi, na uongozi bora na mengine mengi.

05. Mpambanaji, Jasiri na mkosoaji asiyetishwa na chochote, na yeyote

Haijawahi kuwa rahisi kumtisha Lissu. Ana historia ya kusema kile anachokiamini bila kujali nafasi ya anayekisema. Katika kipindi chake bungeni, Lissu aliibua mijadala mikubwa kama sakata la akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 300 zilichotwa kwa njia ya utata.

Aliwataja wahusika kwa majina na kuwasilisha ushahidi wa maandishi, hatua ambayo ilionyesha kiwango cha ujasiri na weledi wake. Pia aliongoza mijadala kuhusu matumizi ya fedha za umma, sheria za uchaguzi na udhaifu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akionyesha namna mfumo ulivyoegemea upande mmoja kwa faida ya chama tawala. Kwa Lissu, ukweli ama anachokiamini ni silaha yake kuu, hata kama inamgharimu maisha.

Alikosoa waziwazi serikali ya Mkapa na serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, hasa kuhusu haki za wachimbaji wadogo na rushwa katika sekta ya madini na mikataba isiyofaa kwa taifa.

Alipofika awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, Lissu hakusita kusema wazi kwamba serikali imegeuka ya kiimla, kifamilia na kikabila na ilitumia vyombo vya dola kuwakandamiza wapinzani, hali iliyowafanya baadhi ya viongozi wa upinzani kukimbilia nje ya nchi.

Katika moja ya hotuba zake kati ya mwaka 2016 na 2017, Lissu alisema "Naibu Waziri Kalemani (Medard, alikuwa Naibu wa Wizara ya Madini wakati huo), mtoto wa dada sijui wa kaka, wote Chato( Kanda ya Ziwa anakotokea Magufuli)". Hapa alikuwa akizungumzia kufukuzwa kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kuachwa Naibu wake (Kalemani), kwa tuhuma ambazo aliamini Lissu kwamba zilipaswa kumfukuzisha pia na Kalemani, lakini alidai alilindwa kindugu.

Aliongeza kuhusu ukabila akimuhusiha Rais Magufuli ambaye alikuwa Msukuma kutoka kanda ya Ziwa na viongozi waliopewa nafasi mbalimbali serikalini; "Mkuu wa Majeshi Msukuma, (anatoka) Kanda ya Ziwa, Mkuu wa Polisi Kanda ya Ziwa, Mwanasheria Mkuu, Kanda ya Ziwa, Mwendesha Mashtaka Kanda ya Ziwa, Kaimu Jajim Mkuu, Kanda ya Ziwa, Mlipaji Mkuu wa Serikali, Kanda ya Ziwa, nani asiyejua, tupaosema nchi imeingia kwenye Udikteta ndiyo hivi".

Msemaji wa serikali wakati huo, Hassan Abbas alijibu matamshi ya Lissu wiki hiyo hiyo alipoyatoa akikanusha Serikali kuegemea ukabila, undugu ama ujamaa na kwamba serikali haitakubali mtu ama kundi la watu kutumia vibaya uhuru wa kujieleza.

Kumkosoa kwa kumuita Rais Magufuli 'Dikteta Uchwara", kulizua mijadala sana mwaka 2016 mpaka 2017 kabla ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana na kusurika kifo. Alitumia zaidi nafasi yake kama Mbunge na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupata majukwaa ya kumkoa Magufuli na kuikosoa serikali kwa kina.

06. Mwanasiasa mwenye misimamo mikali, asiyeogopa "kumlipua yeyote" na kwa sababu hiyo baadhi humuona kama 'Mropokaji'

Kwa tukio la kushambuliwa risasi na kunusurika kufa, kwa mtu mwingine asiye imara na misiamo, asingeweza kurejea kwenye siasa, uanaharakati ama shughuli yoyote inayoweza kuleta uadui hata mdogo. Lakini Lissu wala hajatetereka mpaka leo.

Kwa misimamo yake, amekuwa akikataa pia kushiriki mazungumzo ya maridhiano na Chama Cha Mapinduzi, CCM, akiyaita "mazungumzo hewa yasiyo na dhamira ya kweli."

Baada kurejea nchini mwaka 2020, na kugombea urais, Lissu alirejesha nguvu ya upinzani katika siasa za Tanzania, iliyoanza kudorora, baada ya mikutano ya kisiasa kufungwa. Akaendelea kukosoa mfumo wa uchaguzi Tanzania, akionyesha unaipendelea chama tawala, CCM, jambo ambalo Mamlaka na CCM wenyewe wanapinga.

Disemba 2024 Chadema chini ya mwenyekiti aliyepita, Freeman Mbowe, kilipitisha 'No Reforms, No Election', ambao ni msimamo wa kisera wa chama hicho unaotaka mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa na uhuru wa mikutano ya hadhara kabla ya kushiriki uchaguzi.

Lissu amekuwa msitari wa mbele kutetea msimamo huu tangu awe mwenyekiti Januari, 2025, akisisitiza kuwa kushiriki uchaguzi bila marekebisho ni kushiriki udanganyifu. Hata pale baadhi ya wanachama wa CHADEMA walipoanza kuyumba kwenye msimamo huo, Lissu alibaki imara.

Kuanzia kwenye uchaguzi wa ndani wa chama, ambapo alipokataa kukaa pembeni na kumpisha Mbowe agombee uenyekiti, mpaka kupigia debe msimamo wa "No Reforms, No Election', Lissu alisemwa kama mropokaji.

Lakini yeye ameendelea kusimamia hilo na kuendelea kuhubiri kwa wananchi ili wamuunge mkono, msimamo ambao sasa unamgharimu sasa, amekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhaini.

07. Mtu wa kesi 'lukuki'

Aprili 09, 2025, Lissu alikamatwa akiwa mkoani Ruvuma baada ya kufanya mkutano wa hadhara kupigia debe msimamo wa "No Reforms, No Election'. April 10, 2025 akafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam na akafunguliwa mashitaka ya uhaini, kosa ambalo linahusishwa na kutishia usalama wa taifa.

Kosa hili halina dhamana, na hivyo Lissu anasubiri hatma yake akiwa rumande. Hii si kesi ya kwanza, Lissu amekuwa na kesi nyingi, na nyingi zikiwa za uchochezi kwa maneno aliyoongea kwenye majukwa ya siasa, ama majukwaa mengine yanayohusisha ukosoaji wake.

"Hafungwi mtu hapa....., sikilizeni niwaambie nina kesi sita Kisutu (Mahakama), na zote za uchochezi', alisema Lissu wakati wa harakati za uchaguzi Mkuu wa 2020, akiwatoa hofu wanachama wa Chadema kwamba kesi hizo hazitamzuia kugombea Urais.

Hata hivyo, kesi ya sasa ya uhaini ni kubwa na ya aina yake. Akikutwa na hatia adhabu yake ni kifo kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Lakini kwa Lissu mwenyewe labda kwa sababu ni mbobevu wa sheria, haonyeshi usoni ukubwa wa kesi hiyo zaidi ya kuendelea na ari yake ya kisiasa.

"Msiogope hii ndiyo njia ya kwenda Ikulu kama Mandela (Nelson Mandela, Rais wa zamani wa Afrika Kusini)", anasema Lissu kuwatoa hofu wafuasi wa chama chake, waliofika Mahakamani.

Kwa wafuasi wake, wanaiona kesi hii ni kama muendelezo wa uonevu kwa wanasiasa wa upinzani. Kwa Serikali, huenda kesi hii ni jaribio la kudhibiti kile wanachokiona kama uchochezi na usalama wa taifa. Lakini kwa wachambuzi wa siasa na haki za binadamu, kesi hii ni kipimo cha hali ya uhuru wa kisiasa na demokrasia ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Kesi yake inaweza kuwa mojawapo ya matukio muhimu zaidi katika historia ya kisasa ya Tanzania. Kama atapatikana na hatia, inaweza kubadilisha sura ya siasa ya upinzani nchini. Kama atashinda vita hii ya kisheria, huenda akawa alama hai ya ushindi wa haki dhidi ya woga.

Mwisho, Asanteni​
 
Amos Makala ni kama maji, hata kama humpendi kuna mahali utamuandika tu
 
Ni mmoja ya raia bora sana kwenye nchi yetu,nakumbuka kipindi anasimamia kesi migodi mkoani Mara,wakati wa bunge la katiba kuhusu serikali tatu bila kusahau kesi ya richmond.

Kipekee sana,namshukuru Mungu kwa maisha ya huyu kiumbe,ametuonyesha ni kwa namna gani sisi watanzania wengi tulivyo waoga katika kutafuta haki zetu.
Mungu aendelee kumlinda na kumkirimia neema zake zaidi na zaidi.
 
Moderator tafadhali, rekebisha kwenye title ya makala hii palipoandikwa "Ni hasa mtu huyu" usahihi inapaswa isomeke "NI NANI HASA MTU HUYU?"
 
Amos Makala ni kama maji, hata kama humpendi kuna mahali utamuandika tu
Asante kwa maoni yako

Lakini kama ni kumhusu Amos Makala, nadhani wewe uko kwenye nafasi nzuri kumwandikia wasifu wa makala yake ndefu

Kumbuka, ukiandika usisahau kuweka ule uzushi wake kuwa CHADEMA wanataka kuzuia uchaguzi kwa kuwa wameenda madukani kununua virusi vya Ebola na M-POX wavisambaze hapa nchini
 
Ni mmoja ya raia bora sana kwenye nchi yetu,nakumbuka kipindi anasimamia kesi migodi mkoani Mara,wakati wa bunge la katiba kuhusu serikali tatu bila kusahau kesi ya richmond.

Kipekee sana,namshukuru Mungu kwa maisha ya huyu kiumbe,ametuonyesha ni kwa namna gani sisi watanzania wengi tulivyo waoga katika kutafuta haki zetu.
Mungu aendelee kumlinda na kumkirimia neema zake zaidi na zaidi.
Wakati wa ubunge wake kule Jimbo la Singida Mashariki, alielimisha wananchi wake wote na kujenga awareness kubwa wa kisheria juu ya haki na wajibu wao...

Ndio maana kule, CCM ni kama haipo kabisa na ukifanyika uchaguzi wa kawaida huru na haki, CCM wanaweza kuambulia kura 5 tu

Huyu ni mwanasiasa na mwanaharakati wa haki za binadamu asiyeyumba wala kuyumbishwa na chochote
 
MAMBO SABA USIYO YAJUA KUHUSU TUNDU LISSU.
-
Courtesy: BBCSwahili.com​
Katika historia ya siasa za Tanzania, ni vigumu kutaja majina ya wanasiasa walioteka hisia za watu kwa hoja, ujasiri na misimamo bila kumtaja Tundu Antiphas Lissu.

Kwa wengi, yeye ni alama ya mapambano ya haki, demokrasia na uwajibikaji wa serikali. Kwa wengine, ni mpinzani mkorofi anayependa kugonganisha fikra na utawala.

Lakini kwa wengi, Tundu Lissu ni sauti isiyotetereka katika mapambano ya haki, uwajibikaji na utawala wa sheria.

Hivi sasa, akiwa amewekwa rumande kwa tuhuma za uhaini ambazo kwa sheria za Tanzania hazina dhamana, jina la kiongozi huyu wa chama kikuu cha upinzani limerudi tena kwenye vichwa vya habari kitaifa na kimataifa, lakini hii si mara ya kwanza kwani Lissu ni mtu wa historia ndefu sana toka miaka 1990s

Ili kumuelewa kwa undani Lissu ni muhimu kumtazama kwa jicho pana: ni nani hasa huyu mtu? Haya hapa ni mambo saba muhimu yanayomtambulisha.

01. Msomi aliyelelewa kwenye taaluma na tafakuri ya sheria.

Tundu Lissu ni msomi wa sheria mwenye taaluma pana na ya kina wa kiwango cha shahada mbili (Masters), aliyezaliwa katika kijiji cha Mahambe wilayani Ikungi, mkoa wa Singida - Tanzania na kusoma sekondari ya awali (O'Level) katika Shule ya Sekondari ya Ilboru, Arusha (shule ya wanafunzi wenye vipaji maalumu kiakili) na baadaye Elimu ya juu ya sekondari (A'Level), Shule ya Sekondari Galanos iliyoko Tanga

Alipata Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1994, mojawapo ya taasisi kongwe na zenye heshima kubwa Afrika Mashariki na baadaye kufanya shahada yake ya pili ya sheria nchini Uingereza

Hapa ndipo alipoweka msingi wa uelewa wake wa kisheria, hasa kuhusu haki za binadamu, utawala wa sheria na uwajibikaji wa taasisi za dola.

02. Lissu alianza kujitambulisha kama mwanaharakati kabla hajavaa rasmi koti la kisiasa.

Tangu miaka ya 1990, alikuwa mstari wa mbele katika kutetea wananchi waliokuwa wakinyanyaswa na mfumo wa sheria usio wa haki.

Aliwahi kuwa mshauri wa kisheria wa mashirika kama vile Legal and Human Rights Centre Environmental Law Alliance Worldwide na pia alikuwa mjumbe wa Bodi ya International Federation for Human Rights.

Kazi hizi zilimuwezesha kushughulika na kesi zinazohusu mazingira, haki za binadamu, ardhi na uwajibikaji wa makampuni ya kimataifa barani Afrika.

Kama wakili alitoa msaada wa kisheria kwa watu wanaoishi katika mazingira ya uchimbaji madini walioathiriwa na ufukuzwaji ktk ardhi zao lakini wasio na uwezo wa kugharamia huduma hizo na hivyo kujijengea jina kama mtetezi wa wanyonge

03. Mwanasiasa mshawishi na mwalimu wa kujenga hoja.

Akiwa bungeni, Lissu alitokea kuwa mmoja wa wabunge wenye ushawishi mkubwa.

Alijijengea heshima kubwa kama mzungumzaji mahiri, mwenye uwezo wa kutoa hoja nzito zenye mashiko ya kisheria na kitaalamu.

Alipewa nafasi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambapo aliongoza mijadala mizito kuhusu bajeti, sheria kandamizi, masuala ya madini na mikataba mibovu ya serikali.

Alijulikana kwa kutumia takwimu, nyaraka na vielelezo thabiti katika kuibua hoja, jambo lililowafanya wabunge na wananchi kumheshimu hata kama hawakukubaliana naye.

04. King'ang'anizi mwenye matumaini na asiyekata tamaa

Mojawapo ya sifa kuu inayomtambulisha Tundu Lissu ni kuwa mtu mwenye matumaini yasiyotikisika na kutokata tamaa, hata katika mazingira ya hatari au kukataliwa na kukimbiwa na wenzake.

Lissu amekuwa mstari wa mbele katika kudai Katiba mpya ya Tanzania kwa zaidi ya muongo mmoja, akiitazama kama msingi wa haki, uwajibikaji wa watawala, na ujenzi wa taifa lenye misingi ya demokrasia ya kweli.

Alianza kampeni hii akiwa bado Mbunge na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, akihudumu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete 2005 - 2015

Wakati baadhi ya wanasiasa walijitoa au kukata tamaa kutokana na changamoto zilizokumba mchakato huo, Lissu aliendelea kusimama imara hata baada ya Bunge hilo kuvunjika bila kufikia muafaka wa kitaifa.

Katika kila jukwaa la kisiasa, iwe ndani ya nchi au akiwa uhamishoni baada ya jaribio la mauaji, Lissu ameendelea kuhubiri umuhimu wa Katiba mpya.

Hata katika kampeni yake ya urais mwaka 2020, suala la Katiba mpya lilikuwa mojawapo ya nguzo kuu ya ajenda yake.

Alikuwa akirudia mara kwa mara kuwa, "Katiba ya mwaka 1977 ni Katiba ya chama kimoja, haikidhi mahitaji ya taifa la vyama vingi," akisisitiza kuwa bila mabadiliko ya msingi ya kikatiba, uchaguzi wowote hauwezi kuwa huru na wa haki.

Hadi leo, anapokumbwa na kesi nzito ya uhaini kutokana na msimamo wake wa "No Reform, No Election", anaendelea kusisitiza kuwa Tanzania haiwezi kusonga mbele bila katiba mpya ya wananchi.

Kwa Lissu, unaweza kumuita king'ang'anizi anapolitaka jambo lake, na muhimu zaidi ni kuwa, matumaini, imani itendayo kazi, uelewa wa maarifa mapana aliyonayo ktk mambo anayosimamia ndizo silaha zake za hatari na muhimu ambazo huangusha mlima wowote ulio mbele yake. Haamini katika kukata tamaa wala kushindwa kwa jambo lililo haki, bali katika kusimama imara hadi haki ipatikane.

Katika kampeni ya No reform no election ambayo sasa inaongozwa na Makamu mwenyekiti wake chadema, Ndugu John Heche, imekuwa ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa Tume huru ya uchaguzi, siasa safi, na uongozi bora na mengine mengi.

05. Mpambanaji, Jasiri na mkosoaji asiyetishwa na chochote, na yeyote

Haijawahi kuwa rahisi kumtisha Lissu. Ana historia ya kusema kile anachokiamini bila kujali nafasi ya anayekisema. Katika kipindi chake bungeni, Lissu aliibua mijadala mikubwa kama sakata la akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 300 zilichotwa kwa njia ya utata.

Aliwataja wahusika kwa majina na kuwasilisha ushahidi wa maandishi, hatua ambayo ilionyesha kiwango cha ujasiri na weledi wake. Pia aliongoza mijadala kuhusu matumizi ya fedha za umma, sheria za uchaguzi na udhaifu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akionyesha namna mfumo ulivyoegemea upande mmoja kwa faida ya chama tawala. Kwa Lissu, ukweli ama anachokiamini ni silaha yake kuu, hata kama inamgharimu maisha.

Alikosoa waziwazi serikali ya Mkapa na serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, hasa kuhusu haki za wachimbaji wadogo na rushwa katika sekta ya madini na mikataba isiyofaa kwa taifa.

Alipofika awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, Lissu hakusita kusema wazi kwamba serikali imegeuka ya kiimla, kifamilia na kikabila na ilitumia vyombo vya dola kuwakandamiza wapinzani, hali iliyowafanya baadhi ya viongozi wa upinzani kukimbilia nje ya nchi.

Katika moja ya hotuba zake kati ya mwaka 2016 na 2017, Lissu alisema "Naibu Waziri Kalemani (Medard, alikuwa Naibu wa Wizara ya Madini wakati huo), mtoto wa dada sijui wa kaka, wote Chato( Kanda ya Ziwa anakotokea Magufuli)". Hapa alikuwa akizungumzia kufukuzwa kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kuachwa Naibu wake (Kalemani), kwa tuhuma ambazo aliamini Lissu kwamba zilipaswa kumfukuzisha pia na Kalemani, lakini alidai alilindwa kindugu.

Aliongeza kuhusu ukabila akimuhusiha Rais Magufuli ambaye alikuwa Msukuma kutoka kanda ya Ziwa na viongozi waliopewa nafasi mbalimbali serikalini; "Mkuu wa Majeshi Msukuma, (anatoka) Kanda ya Ziwa, Mkuu wa Polisi Kanda ya Ziwa, Mwanasheria Mkuu, Kanda ya Ziwa, Mwendesha Mashtaka Kanda ya Ziwa, Kaimu Jajim Mkuu, Kanda ya Ziwa, Mlipaji Mkuu wa Serikali, Kanda ya Ziwa, nani asiyejua, tupaosema nchi imeingia kwenye Udikteta ndiyo hivi".

Msemaji wa serikali wakati huo, Hassan Abbas alijibu matamshi ya Lissu wiki hiyo hiyo alipoyatoa akikanusha Serikali kuegemea ukabila, undugu ama ujamaa na kwamba serikali haitakubali mtu ama kundi la watu kutumia vibaya uhuru wa kujieleza.

Kumkosoa kwa kumuita Rais Magufuli 'Dikteta Uchwara", kulizua mijadala sana mwaka 2016 mpaka 2017 kabla ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana na kusurika kifo. Alitumia zaidi nafasi yake kama Mbunge na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupata majukwaa ya kumkoa Magufuli na kuikosoa serikali kwa kina.

06. Mwanasiasa mwenye misimamo mikali, asiyeogopa "kumlipua yeyote" na kwa sababu hiyo baadhi humuona kama 'Mropokaji'

Kwa tukio la kushambuliwa risasi na kunusurika kufa, kwa mtu mwingine asiye imara na misiamo, asingeweza kurejea kwenye siasa, uanaharakati ama shughuli yoyote inayoweza kuleta uadui hata mdogo. Lakini Lissu wala hajatetereka mpaka leo.

Kwa misimamo yake, amekuwa akikataa pia kushiriki mazungumzo ya maridhiano na Chama Cha Mapinduzi, CCM, akiyaita "mazungumzo hewa yasiyo na dhamira ya kweli."

Baada kurejea nchini mwaka 2020, na kugombea urais, Lissu alirejesha nguvu ya upinzani katika siasa za Tanzania, iliyoanza kudorora, baada ya mikutano ya kisiasa kufungwa. Akaendelea kukosoa mfumo wa uchaguzi Tanzania, akionyesha unaipendelea chama tawala, CCM, jambo ambalo Mamlaka na CCM wenyewe wanapinga.

Disemba 2024 Chadema chini ya mwenyekiti aliyepita, Freeman Mbowe, kilipitisha 'No Reforms, No Election', ambao ni msimamo wa kisera wa chama hicho unaotaka mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa na uhuru wa mikutano ya hadhara kabla ya kushiriki uchaguzi.

Lissu amekuwa msitari wa mbele kutetea msimamo huu tangu awe mwenyekiti Januari, 2025, akisisitiza kuwa kushiriki uchaguzi bila marekebisho ni kushiriki udanganyifu. Hata pale baadhi ya wanachama wa CHADEMA walipoanza kuyumba kwenye msimamo huo, Lissu alibaki imara.

Kuanzia kwenye uchaguzi wa ndani wa chama, ambapo alipokataa kukaa pembeni na kumpisha Mbowe agombee uenyekiti, mpaka kupigia debe msimamo wa "No Reforms, No Election', Lissu alisemwa kama mropokaji.

Lakini yeye ameendelea kusimamia hilo na kuendelea kuhubiri kwa wananchi ili wamuunge mkono, msimamo ambao sasa unamgharimu sasa, amekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhaini.

07. Mtu wa kesi 'lukuki'

Aprili 09, 2025, Lissu alikamatwa akiwa mkoani Ruvuma baada ya kufanya mkutano wa hadhara kupigia debe msimamo wa "No Reforms, No Election'. April 10, 2025 akafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam na akafunguliwa mashitaka ya uhaini, kosa ambalo linahusishwa na kutishia usalama wa taifa.

Kosa hili halina dhamana, na hivyo Lissu anasubiri hatma yake akiwa rumande. Hii si kesi ya kwanza, Lissu amekuwa na kesi nyingi, na nyingi zikiwa za uchochezi kwa maneno aliyoongea kwenye majukwa ya siasa, ama majukwaa mengine yanayohusisha ukosoaji wake.

"Hafungwi mtu hapa....., sikilizeni niwaambie nina kesi sita Kisutu (Mahakama), na zote za uchochezi', alisema Lissu wakati wa harakati za uchaguzi Mkuu wa 2020, akiwatoa hofu wanachama wa Chadema kwamba kesi hizo hazitamzuia kugombea Urais.

Hata hivyo, kesi ya sasa ya uhaini ni kubwa na ya aina yake. Akikutwa na hatia adhabu yake ni kifo kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Lakini kwa Lissu mwenyewe labda kwa sababu ni mbobevu wa sheria, haonyeshi usoni ukubwa wa kesi hiyo zaidi ya kuendelea na ari yake ya kisiasa.

"Msiogope hii ndiyo njia ya kwenda Ikulu kama Mandela (Nelson Mandela, Rais wa zamani wa Afrika Kusini)", anasema Lissu kuwatoa hofu wafuasi wa chama chake, waliofika Mahakamani.

Kwa wafuasi wake, wanaiona kesi hii ni kama muendelezo wa uonevu kwa wanasiasa wa upinzani. Kwa Serikali, huenda kesi hii ni jaribio la kudhibiti kile wanachokiona kama uchochezi na usalama wa taifa. Lakini kwa wachambuzi wa siasa na haki za binadamu, kesi hii ni kipimo cha hali ya uhuru wa kisiasa na demokrasia ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Kesi yake inaweza kuwa mojawapo ya matukio muhimu zaidi katika historia ya kisasa ya Tanzania. Kama atapatikana na hatia, inaweza kubadilisha sura ya siasa ya upinzani nchini. Kama atashinda vita hii ya kisheria, huenda akawa alama hai ya ushindi wa haki dhidi ya woga.

Mwisho, Asanteni​
Hii jamaa ni namba nyingine...

Ukiwa na maarifa (knowledge) na uelewa/ufahamu (understanding) wa mambo ktk ulimwengu huu, wewe unakuwa na silaha muhimu tayari za ushindi ktk msukosuko wowote utakaokumbana nao....

This guy is full of knowledge. He knows Tanzania A - Z and the whole world by in large....

Kwa sababu ya kubeba silaha hii, si rahisi kumshinda kwa hoja mtu kama huyu isipokuwa kukuabaliana naye tu au uzipige hoja zake kwa bunduki za SMG na AK47 kama alivyofanya Magufuli mwaka 2017...

Tunaona na Bi Samia Chura Kiziwi naye ameamua kuzipiga hoja za bingwa huyu kwa mtindo wa kumsingizia makosa makubwa...

SAMIA HAWEZI KUSHINDA KAMWE!!
 
Haki haiombwi hata km utaweka upanga shingoni ni bora kufa

Huyu mwamba Lissu anamaanisha na anasimamia anachomaanisha

We never beg we never bow!
 
Hivi sasa, akiwa amewekwa rumande kwa tuhuma za uhaini ambazo kwa sheria za Tanzania hazina dhamana, jina la kiongozi huyu wa chama kikuu cha upinzani limerudi tena kwenye vichwa vya habari kitaifa na kimataifa, lakini hii si mara ya kwanza kwani Lissu ni mtu wa historia ndefu sana toka miaka 1990s
Mwisho wa kunukuu
 
Alipata Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1994, mojawapo ya taasisi kongwe na zenye heshima kubwa Afrika Mashariki na baadaye kufanya shahada yake ya pili ya sheria nchini Uingereza
Kumbe Mwamba alisomea Nje na kupata exposure ya ustaarabu kitambo sana, ndio maana yuko hivyo alivyo. Ni alama ya Elimu na kustaarabika kwa viwango vya juu sana
 
Aliwahi kuwa mshauri wa kisheria wa mashirika kama vile Legal and Human Rights Centre Environmental Law Alliance Worldwide na pia alikuwa mjumbe wa Bodi ya International Federation for Human Rights
Kuna siku Rais Dr Samia Suluhu hassan aliwahi kueleza hii historia akidai kuwa walifanya kazi ofisi moja kwenye mashirika haya. Na kuna makala iliwahi kuzunguka kwenye media platforms zikieleza ukaribu wa Dr Samia na Mh Lissu
 
MAMBO SABA USIYO YAJUA KUHUSU TUNDU LISSU.
-
Courtesy: BBCSwahili.com​
Katika historia ya siasa za Tanzania, ni vigumu kutaja majina ya wanasiasa walioteka hisia za watu kwa hoja, ujasiri na misimamo bila kumtaja Tundu Antiphas Lissu.

Kwa wengi, yeye ni alama ya mapambano ya haki, demokrasia na uwajibikaji wa serikali. Kwa wengine, ni mpinzani mkorofi anayependa kugonganisha fikra na utawala.

Lakini kwa wengi, Tundu Lissu ni sauti isiyotetereka katika mapambano ya haki, uwajibikaji na utawala wa sheria.

Hivi sasa, akiwa amewekwa rumande kwa tuhuma za uhaini ambazo kwa sheria za Tanzania hazina dhamana, jina la kiongozi huyu wa chama kikuu cha upinzani limerudi tena kwenye vichwa vya habari kitaifa na kimataifa, lakini hii si mara ya kwanza kwani Lissu ni mtu wa historia ndefu sana toka miaka 1990s

Ili kumuelewa kwa undani Lissu ni muhimu kumtazama kwa jicho pana: ni nani hasa huyu mtu? Haya hapa ni mambo saba muhimu yanayomtambulisha.

01. Msomi aliyelelewa kwenye taaluma na tafakuri ya sheria.

Tundu Lissu ni msomi wa sheria mwenye taaluma pana na ya kina wa kiwango cha shahada mbili (Masters), aliyezaliwa katika kijiji cha Mahambe wilayani Ikungi, mkoa wa Singida - Tanzania na kusoma sekondari ya awali (O'Level) katika Shule ya Sekondari ya Ilboru, Arusha (shule ya wanafunzi wenye vipaji maalumu kiakili) na baadaye Elimu ya juu ya sekondari (A'Level), Shule ya Sekondari Galanos iliyoko Tanga

Alipata Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1994, mojawapo ya taasisi kongwe na zenye heshima kubwa Afrika Mashariki na baadaye kufanya shahada yake ya pili ya sheria nchini Uingereza

Hapa ndipo alipoweka msingi wa uelewa wake wa kisheria, hasa kuhusu haki za binadamu, utawala wa sheria na uwajibikaji wa taasisi za dola.

02. Lissu alianza kujitambulisha kama mwanaharakati kabla hajavaa rasmi koti la kisiasa.

Tangu miaka ya 1990, alikuwa mstari wa mbele katika kutetea wananchi waliokuwa wakinyanyaswa na mfumo wa sheria usio wa haki.

Aliwahi kuwa mshauri wa kisheria wa mashirika kama vile Legal and Human Rights Centre Environmental Law Alliance Worldwide na pia alikuwa mjumbe wa Bodi ya International Federation for Human Rights.

Kazi hizi zilimuwezesha kushughulika na kesi zinazohusu mazingira, haki za binadamu, ardhi na uwajibikaji wa makampuni ya kimataifa barani Afrika.

Kama wakili alitoa msaada wa kisheria kwa watu wanaoishi katika mazingira ya uchimbaji madini walioathiriwa na ufukuzwaji ktk ardhi zao lakini wasio na uwezo wa kugharamia huduma hizo na hivyo kujijengea jina kama mtetezi wa wanyonge

03. Mwanasiasa mshawishi na mwalimu wa kujenga hoja.

Akiwa bungeni, Lissu alitokea kuwa mmoja wa wabunge wenye ushawishi mkubwa.

Alijijengea heshima kubwa kama mzungumzaji mahiri, mwenye uwezo wa kutoa hoja nzito zenye mashiko ya kisheria na kitaalamu.

Alipewa nafasi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambapo aliongoza mijadala mizito kuhusu bajeti, sheria kandamizi, masuala ya madini na mikataba mibovu ya serikali.

Alijulikana kwa kutumia takwimu, nyaraka na vielelezo thabiti katika kuibua hoja, jambo lililowafanya wabunge na wananchi kumheshimu hata kama hawakukubaliana naye.

04. King'ang'anizi mwenye matumaini na asiyekata tamaa

Mojawapo ya sifa kuu inayomtambulisha Tundu Lissu ni kuwa mtu mwenye matumaini yasiyotikisika na kutokata tamaa, hata katika mazingira ya hatari au kukataliwa na kukimbiwa na wenzake.

Lissu amekuwa mstari wa mbele katika kudai Katiba mpya ya Tanzania kwa zaidi ya muongo mmoja, akiitazama kama msingi wa haki, uwajibikaji wa watawala, na ujenzi wa taifa lenye misingi ya demokrasia ya kweli.

Alianza kampeni hii akiwa bado Mbunge na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, akihudumu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete 2005 - 2015

Wakati baadhi ya wanasiasa walijitoa au kukata tamaa kutokana na changamoto zilizokumba mchakato huo, Lissu aliendelea kusimama imara hata baada ya Bunge hilo kuvunjika bila kufikia muafaka wa kitaifa.

Katika kila jukwaa la kisiasa, iwe ndani ya nchi au akiwa uhamishoni baada ya jaribio la mauaji, Lissu ameendelea kuhubiri umuhimu wa Katiba mpya.

Hata katika kampeni yake ya urais mwaka 2020, suala la Katiba mpya lilikuwa mojawapo ya nguzo kuu ya ajenda yake.

Alikuwa akirudia mara kwa mara kuwa, "Katiba ya mwaka 1977 ni Katiba ya chama kimoja, haikidhi mahitaji ya taifa la vyama vingi," akisisitiza kuwa bila mabadiliko ya msingi ya kikatiba, uchaguzi wowote hauwezi kuwa huru na wa haki.

Hadi leo, anapokumbwa na kesi nzito ya uhaini kutokana na msimamo wake wa "No Reform, No Election", anaendelea kusisitiza kuwa Tanzania haiwezi kusonga mbele bila katiba mpya ya wananchi.

Kwa Lissu, unaweza kumuita king'ang'anizi anapolitaka jambo lake, na muhimu zaidi ni kuwa, matumaini, imani itendayo kazi, uelewa wa maarifa mapana aliyonayo ktk mambo anayosimamia ndizo silaha zake za hatari na muhimu ambazo huangusha mlima wowote ulio mbele yake. Haamini katika kukata tamaa wala kushindwa kwa jambo lililo haki, bali katika kusimama imara hadi haki ipatikane.

Katika kampeni ya No reform no election ambayo sasa inaongozwa na Makamu mwenyekiti wake chadema, Ndugu John Heche, imekuwa ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa Tume huru ya uchaguzi, siasa safi, na uongozi bora na mengine mengi.

05. Mpambanaji, Jasiri na mkosoaji asiyetishwa na chochote, na yeyote

Haijawahi kuwa rahisi kumtisha Lissu. Ana historia ya kusema kile anachokiamini bila kujali nafasi ya anayekisema. Katika kipindi chake bungeni, Lissu aliibua mijadala mikubwa kama sakata la akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 300 zilichotwa kwa njia ya utata.

Aliwataja wahusika kwa majina na kuwasilisha ushahidi wa maandishi, hatua ambayo ilionyesha kiwango cha ujasiri na weledi wake. Pia aliongoza mijadala kuhusu matumizi ya fedha za umma, sheria za uchaguzi na udhaifu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akionyesha namna mfumo ulivyoegemea upande mmoja kwa faida ya chama tawala. Kwa Lissu, ukweli ama anachokiamini ni silaha yake kuu, hata kama inamgharimu maisha.

Alikosoa waziwazi serikali ya Mkapa na serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, hasa kuhusu haki za wachimbaji wadogo na rushwa katika sekta ya madini na mikataba isiyofaa kwa taifa.

Alipofika awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, Lissu hakusita kusema wazi kwamba serikali imegeuka ya kiimla, kifamilia na kikabila na ilitumia vyombo vya dola kuwakandamiza wapinzani, hali iliyowafanya baadhi ya viongozi wa upinzani kukimbilia nje ya nchi.

Katika moja ya hotuba zake kati ya mwaka 2016 na 2017, Lissu alisema "Naibu Waziri Kalemani (Medard, alikuwa Naibu wa Wizara ya Madini wakati huo), mtoto wa dada sijui wa kaka, wote Chato( Kanda ya Ziwa anakotokea Magufuli)". Hapa alikuwa akizungumzia kufukuzwa kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kuachwa Naibu wake (Kalemani), kwa tuhuma ambazo aliamini Lissu kwamba zilipaswa kumfukuzisha pia na Kalemani, lakini alidai alilindwa kindugu.

Aliongeza kuhusu ukabila akimuhusiha Rais Magufuli ambaye alikuwa Msukuma kutoka kanda ya Ziwa na viongozi waliopewa nafasi mbalimbali serikalini; "Mkuu wa Majeshi Msukuma, (anatoka) Kanda ya Ziwa, Mkuu wa Polisi Kanda ya Ziwa, Mwanasheria Mkuu, Kanda ya Ziwa, Mwendesha Mashtaka Kanda ya Ziwa, Kaimu Jajim Mkuu, Kanda ya Ziwa, Mlipaji Mkuu wa Serikali, Kanda ya Ziwa, nani asiyejua, tupaosema nchi imeingia kwenye Udikteta ndiyo hivi".

Msemaji wa serikali wakati huo, Hassan Abbas alijibu matamshi ya Lissu wiki hiyo hiyo alipoyatoa akikanusha Serikali kuegemea ukabila, undugu ama ujamaa na kwamba serikali haitakubali mtu ama kundi la watu kutumia vibaya uhuru wa kujieleza.

Kumkosoa kwa kumuita Rais Magufuli 'Dikteta Uchwara", kulizua mijadala sana mwaka 2016 mpaka 2017 kabla ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana na kusurika kifo. Alitumia zaidi nafasi yake kama Mbunge na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupata majukwaa ya kumkoa Magufuli na kuikosoa serikali kwa kina.

06. Mwanasiasa mwenye misimamo mikali, asiyeogopa "kumlipua yeyote" na kwa sababu hiyo baadhi humuona kama 'Mropokaji'

Kwa tukio la kushambuliwa risasi na kunusurika kufa, kwa mtu mwingine asiye imara na misiamo, asingeweza kurejea kwenye siasa, uanaharakati ama shughuli yoyote inayoweza kuleta uadui hata mdogo. Lakini Lissu wala hajatetereka mpaka leo.

Kwa misimamo yake, amekuwa akikataa pia kushiriki mazungumzo ya maridhiano na Chama Cha Mapinduzi, CCM, akiyaita "mazungumzo hewa yasiyo na dhamira ya kweli."

Baada kurejea nchini mwaka 2020, na kugombea urais, Lissu alirejesha nguvu ya upinzani katika siasa za Tanzania, iliyoanza kudorora, baada ya mikutano ya kisiasa kufungwa. Akaendelea kukosoa mfumo wa uchaguzi Tanzania, akionyesha unaipendelea chama tawala, CCM, jambo ambalo Mamlaka na CCM wenyewe wanapinga.

Disemba 2024 Chadema chini ya mwenyekiti aliyepita, Freeman Mbowe, kilipitisha 'No Reforms, No Election', ambao ni msimamo wa kisera wa chama hicho unaotaka mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa na uhuru wa mikutano ya hadhara kabla ya kushiriki uchaguzi.

Lissu amekuwa msitari wa mbele kutetea msimamo huu tangu awe mwenyekiti Januari, 2025, akisisitiza kuwa kushiriki uchaguzi bila marekebisho ni kushiriki udanganyifu. Hata pale baadhi ya wanachama wa CHADEMA walipoanza kuyumba kwenye msimamo huo, Lissu alibaki imara.

Kuanzia kwenye uchaguzi wa ndani wa chama, ambapo alipokataa kukaa pembeni na kumpisha Mbowe agombee uenyekiti, mpaka kupigia debe msimamo wa "No Reforms, No Election', Lissu alisemwa kama mropokaji.

Lakini yeye ameendelea kusimamia hilo na kuendelea kuhubiri kwa wananchi ili wamuunge mkono, msimamo ambao sasa unamgharimu sasa, amekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhaini.

07. Mtu wa kesi 'lukuki'

Aprili 09, 2025, Lissu alikamatwa akiwa mkoani Ruvuma baada ya kufanya mkutano wa hadhara kupigia debe msimamo wa "No Reforms, No Election'. April 10, 2025 akafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam na akafunguliwa mashitaka ya uhaini, kosa ambalo linahusishwa na kutishia usalama wa taifa.

Kosa hili halina dhamana, na hivyo Lissu anasubiri hatma yake akiwa rumande. Hii si kesi ya kwanza, Lissu amekuwa na kesi nyingi, na nyingi zikiwa za uchochezi kwa maneno aliyoongea kwenye majukwa ya siasa, ama majukwaa mengine yanayohusisha ukosoaji wake.

"Hafungwi mtu hapa....., sikilizeni niwaambie nina kesi sita Kisutu (Mahakama), na zote za uchochezi', alisema Lissu wakati wa harakati za uchaguzi Mkuu wa 2020, akiwatoa hofu wanachama wa Chadema kwamba kesi hizo hazitamzuia kugombea Urais.

Hata hivyo, kesi ya sasa ya uhaini ni kubwa na ya aina yake. Akikutwa na hatia adhabu yake ni kifo kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Lakini kwa Lissu mwenyewe labda kwa sababu ni mbobevu wa sheria, haonyeshi usoni ukubwa wa kesi hiyo zaidi ya kuendelea na ari yake ya kisiasa.

"Msiogope hii ndiyo njia ya kwenda Ikulu kama Mandela (Nelson Mandela, Rais wa zamani wa Afrika Kusini)", anasema Lissu kuwatoa hofu wafuasi wa chama chake, waliofika Mahakamani.

Kwa wafuasi wake, wanaiona kesi hii ni kama muendelezo wa uonevu kwa wanasiasa wa upinzani. Kwa Serikali, huenda kesi hii ni jaribio la kudhibiti kile wanachokiona kama uchochezi na usalama wa taifa. Lakini kwa wachambuzi wa siasa na haki za binadamu, kesi hii ni kipimo cha hali ya uhuru wa kisiasa na demokrasia ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Kesi yake inaweza kuwa mojawapo ya matukio muhimu zaidi katika historia ya kisasa ya Tanzania. Kama atapatikana na hatia, inaweza kubadilisha sura ya siasa ya upinzani nchini. Kama atashinda vita hii ya kisheria, huenda akawa alama hai ya ushindi wa haki dhidi ya woga.

Mwisho, Asanteni​
Hili andiko lako ni zuri na ChatGPT itakuwa inalitumia kuchakata taarifa kwa watumiaje wake
 
Back
Top Bottom