MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

Safi
 
MKUU, Utaratbu wa kulipia hiyo witholding Tax (kodi ya zuio) na ushuru wa stempu, inakuwaje ikiwa jengo ni la kwangu na sikupanga?


Nazani itategemea kama unafanya biashara kama kampuni (Entity) au binafsi yaani (Sole proprietorship)

Kama ni ni binafsi jibu ni hilo alokupa jamaa, lakini kama ni limited Company na ukaipunguza kwenye faida gafi uloonesha kwenye hesabu zako basi huenda ukakadiria kodi ya zuio ya pango pamoja na riba.

Ikumbukwe kuwa kuna kanuni za biashara ya kampuni mojawapo ni “separate legal entity “

Kwamba maswala yahusuyo kampuni hayapaswi kuchanganywa na maswala ya mkurugenzi/mmiliki wa hiyo kampuni.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi. Mimi pia hili linanihusu, kwani nilifanya process zote za kupata TIN no. lakini baadae nikapata matatizo, sikufanya tena biashara na TIN sikuchukua. Hapa nafanyaje mkuu? Na kama kuna deni linalipwa kwa mfumo gani? TIN yangu nili-process 2012 mkuu. Nitashukuru kwa maelezo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu samahani, naomba ufafanuzi kidogo hapa, unamaanisha aje kusema "utalipa asilimia 3 ya mauzo yanayozidi 4milion"
Je unamaanisha mauzo yakiwa milion 6, hiyo asilimia 3 ya kodi itakua ya milioni 6? Au hapa itakua ya milion 2(kama zidio kutoka kwenye mil4)
Na kama ni asilimia 3 ya milioni 6, si ni bora nisitunze kumbukumbu ili mlipe laki moja tu!
Ahsante.
 
Bila samahani
Ufafanuzi: Ni kwamba unalipa ile tofauti (zidio) kati ya mil 6 na 4. ie (6mil-4mil) *3%=60,000

Wakati mfanyabiashara asieweka rekodi atalipa sh 100,000
 
Pitia kitabu hiki kidogo kwa kujiongezea maarifa juu ya kodi. Ni cha lugha ya kiswahili toleo la 2019/2020View attachment 1221404
Mkuu naomba kujua...

1. Kama nimesajili kampuni kama individual (au mmiliki binafsi) je kodi itakua sawa na ile ya Ltd?? Mfano zote zitakua 30%?

2. JE nikisajili kama individual nitaweza vipi kutengenisha mapato ya biashara na yale kazi ajira yangu (salary)?

2. Mfano kampuni yangu inatoa huduma ya uwekezaji kwa watu wa nje (sio watanzania), mfano katika hiyo huduma nimepata 1000usd je hapa nitatakiwa kulipia VAT?

3. Je ikiwa mapato yangu kwa 1st quoter ni hiyo 1000usd, je nitatakiwa lipia kodi gani na gani ikiwa silipii VAT?

4. JE naweza sajili coorporate au ltd company alafu nikawa na share 95% alafu wengine wawili wakawa na share 2.5% kwa 2.5%?

5. Je kuna tofauti gani kati ya share holders na directors?? Je, minimumly, share holders wanatakiwa kuwa wangapi na directors wanatakiwa kuwa wangapi?

6. Je katika ugawaji wa faida, ni muda gani faida inatakiwa ku gaiwa? Kila mwezi au kila mwaka?

7. Je ikiwa faida imegaiwa je walio pata mgao wa faida watatakiwa kulipia kodi % ngapi katika faida waliyo pata?

8. Je kuna tofauti gani kati ya "individual" na "coorpotare/Ltd" in terms of mgawanyo wa faida na malipo ya kodi?

9. Je nikisajili kama individual naweza kuja badalisha kwenda coorporation/Ltd kwa badae?

Naomba kuwasilisha!
 
Upepo wa Pesa
1. Usajili:
Unaposema kampuni una maana ni yenye ukomo ie Limited Company? Kwa sababu kwa sheria za usajili wa makampuni ya mwaka 2002 huwezi kusajili kampuni yenye ukomo ya mwanahisa mmoja pekee. Hivyo bhasi swali lako ungeuliza kwamba je kodi ya mtu binafsi ni sawa na kodi za kampuni yenye ukomo? Jawabu lake ni hapana si sawa. Kampuni yenye ukomo ni 30% wakati kwa mtu binafsi inategemea na kiwango cha mapato

2. Mapato ya biashara vs Mapato kutokana na ajira
Swali lako halijawa lenye ufafanuzi wa kutosha maana unasema kutengenisha mapato kwa muktadha upi? "Be specific".

3. Ulipaji kodi ya Ongezeko la Thamani ie VAT
Sio kila kampuni inalipa VAT. Utatakiwa kulipa VAT kama umekidhi vigezo vya kisheria kwa mujibu wa sheria ya ongezeko la kodi ya thamani ya mwaka 2014 ambapo unaweza sajiliwa VAT kama una mauzo yanayofikia au kuzidi mil 100 kwa mwaka au kampuni ya utaalam mfano engineering, accountants etc. Kama unakidhi vigexo hivyo utalipa

4. Ulipaji kodi kwa awamu
Hili nakushauri rejea mada pale juu uone namna gani kodi inalipwa na kodi zipi na zinalipwa kwa vipindi gani kwa ufafanuzi wa kina. Lakini kwa kifupi ni 1. Utajikadiria na kulipa awamu nne za usawa iwapo mauzo yamepanda au kushuka una haki ya kuomba marekebisho ya makadirio ie revise estimates, kama una wafanyakazi kuanzia 10 utatakiwa kulipa kodi ya ufundi ie SDL kila mwezi, Mishahara kama ni kuanzia 270,000+ baada ya makato ya mchango wa mfuko wa jamii utalipa kodi ya zuio ie PAYE kila mwezi, kodi za mikataba, ushuru wa stempu et al

5. Umilikiwa hisa katika kampuni yenye ukomo
Jawabu ni ndiyo unaweza kumiliki hadi 99% na 1% ukampa mwingine kukidhu matakwa ya kisheria

6. Mwanahisa (shareholder) vs Mkurugenzi (Director) na idadi ya watu katika kufungua kampuni yenye ukomo
Idadi ni kuanzia watu wawili na mwisho ni watu 50. Mwanahisa ni mmiliki wa sehemu ya kampuni na mkurugenzi ni mtendaji katika kampuni. Sio lazima mkurugenzi akawa mwanahisa kwn unaweza kumwajiri mkurugenzi nje ya wamiliki wa kampuni

7. Ugawaji wa faida
Inategemea na mfumo wa kampuni wa ugawajinjapo mara nyingi huwa mwisho wa mwaka baada ya kufunga mahesabu ya mwaka then faida ikishajulikana bhasi kuna sehemu ya faida hurudishwa katika kampuni na sehemu hugawiwa kwa wanahisa. Kiwango cha mgawanyiko wa faida hiyo kwa kila mwanahisa hutegemea na idadi ya hisa ambazo mwanahisa anamiliki ndani ya kampuni

8. Mgao wa faida ni 10%

9. Mtu binafsi vs Kampuni yenye ukomo: Faida na kodi
Mtu binafsi hana hana mgawanyiko wa faida na kodi atalipa baada ya ukokotoaji wa kodi na itategemea anaweka kumbukumbu au haweki kumbukumbu. Ukija upande wa kampuni ni 30% kodi na faida hugawanya kwa mujibu wa idadi ya hisa zinazomilikiwa na wanahisa

10. Inakubalika ukisajili jina la biashara baadae kubadilisha kuwa kampuni yenye ukomo

Angalizo: Huenda kuna maswali nimejibu ndiyo siyo kutokana na namna ulivyouliza kwani hayaeleweki kutokana na kuwa na mkanganyiko wa muundo wa maswali yako.

Pia wachangiaji wengine wapo huru kuongeza zaidi maelezo, ufafanuzi na hata kukosoa makosa ya majibu na kuleta majibu sahihi zaidi

Wasalaam
 
2. Mapato ya biashara vs Mapato kutokana na ajira
Swali lako halijawa lenye ufafanuzi wa kutosha maana unasema kutengenisha mapato kwa muktadha upi? "Be specific".
Nilicho maanisha ni kwamba kama nitaisajili kama "individual" na sio Ltd, je mapato ya kampuni hayata weza kuchanganywa na mapato yangu binafsi mfano mshahara ua biashara nyingine nnazo fanya wakati wa kulipa kodi?

Maana ulisema ukisajili kampuni kama individual basi panakua hakuna separation kati ya mtu na biashara!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…