MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

Sijui nn tatizo lkn kwangu kinafunguka
Mkuu hakifunguki
Screenshot_20191002-123034_Drive.jpeg
 
Safi
MUHIMU: UPDATE
MABADILIKO YA VIWANGO VYA KODI NA MENGINEYO KUANZIA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

Katika makala hii ya kodi, sehemu ya pili kuna mabadiliko ya viwango vya kodi ambavyo vimerekebishwa ukilinganisha na mara ya kwanza ya uwasilishaji wa mada. Vlvl uandaaji wa hesabu za mizania kwa mtu binafsi kun a mabadiliko pia. Pitia kwa faida yako na jamii pia

MAKALA: SEHEMU YA KWANZA
Habari zenu wanajukwaa
1. Utangulizi
makala hii inahusu masuala ya kodi kwa wanaoanza biashara lakini vilevile itagusa sheria na biashara kwa ujumla wake. lengo ni kuzidi kuelimishana kwa wasiofahamu na vilevile kukumbushana kwa wenye ufahamu na kuongezeana elimu kwa michango mbalimbali itakayoletwa kutoka kwa wanajukwaa.
2. Biashara na aina zake
Biashara ni kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalmu, wito na makubaliano ya kipekee yenye nia ya kupata faida kwa kifupi ili nisiwachoshe.
kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, biashara zimegawanyika katika makundi manne:
1. Biashara ndogo sana
Ina idadi ya waajiriwa kuanzia mmoja hadi wanne, na Mtaji wake ni kuanzia Sh 1 hadi 5mil

2. Biashara ndogo
Ina idadi ya waajiriwa 5 hadi 49, na mtaji wake ni kuanzia mil5 hadi mil 200

3. Biashara za kati
Ina idadi ya waajiriwa 50 hadi 99 na mtaji ni kati ya mil 200 hadi mil 800

4. Biashara Kubwa
Ina idadi ya waajiriwa zaidi ya 100 na mtaji zaidi ya mil 800.

Vingezo vingine vinavyotumika na Mamlaka ya Mapato kuweka madaraja ya walipa kodi ni kulingana na kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka

3. SHERIA ZA KODI
Shera hizi zinamgusa anaeanza biashara:
1. Sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004
2. sheria ya kodi ya Ongezeko la thmani (VAT) ya mwaka 2014 kwa anefuzu kusajiliwa
3. Sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972
4. sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015
Sheria hizi zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia kodi za ndani

A: Sheria ya Kodi ya Mapato
Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapto yake yanatokana na vyanzo mbalimbali km vilivyoainishwa ktk sheria kama vile
a) Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika
b) Ajira yoyote afanyayo mtu
c) Uwekezaji ktk rasilimali. Mfano nyumba, ardhi na hisa
d) Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio "Final Withholding Tax. Mf: Kodi ya malipo ya pango, malipo ya gawio kutoka ktk kampuni kwa Mtz, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (mrahaba)

B: Mapato yatokanayo na biashara
kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 ikarejewa mwaka 2006, Mapato yanayotozwa kodi kutokana na biashara ni Faida au Ziada itokanayo na biashara kwa mwaka wa mapato. Mapato hayo ni pamoja na:
1. Faida kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma za biashara
2. Malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya au kutofanya biashara kulingana na makubaliano ya upande wa pili
3. Zawadi au Takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara
4. Kiasi cha mapatoyanayohusiana na biashara ambayo vinginevo yangekuwa mapato ya uwekezaji ktk rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba`

Inaendelea.......
B: Taratibu za kufuatwa na mtu anaeanza biashara kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) pamoja na malipo ya kodi na mengineyo:

Mtu anaeanza biashara atatakiwa kuomba TIN kutoka TRA ambapo vielelezo hv vitahitajika
1. Fomu za maombi ya TIN kwa mtu binafsi (zinatolewa TRA)
2. Barua ya utambulisho wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (hutolewa na TRA)
3. Mkataba wa pango kwa aliepanga eneo la biashara au kielelzo cha umiliki wa eneo la biashara kama hati, ofa au karatasi za malipo ya kodi ya majengo
4. Kopi ya kitambulisho cha Taifa, Leseni ya udreva, paspoti ya kusafiria au kitambulisho cha kupigia kura
5. Picha ndogo ya paspoti saizi

Mhusika utaulizwa juu ya biashara yako "business assessment". baada ya hapo utaambiwa kiasi cha kodi utakayostahili kulipa kutokana na mauzo ya biashara unayofanya au unayotarajia kuifanya. baada ya maelezo haya taratibu nyingine zitaendele na hatimaye utapata TIN.
Kwa leo naomba tuishie hapa sehemu ya kwanza kutokana na majukumu. Tutaendelea sehemu ya pili
 
MKUU, Utaratbu wa kulipia hiyo witholding Tax (kodi ya zuio) na ushuru wa stempu, inakuwaje ikiwa jengo ni la kwangu na sikupanga?


Nazani itategemea kama unafanya biashara kama kampuni (Entity) au binafsi yaani (Sole proprietorship)

Kama ni ni binafsi jibu ni hilo alokupa jamaa, lakini kama ni limited Company na ukaipunguza kwenye faida gafi uloonesha kwenye hesabu zako basi huenda ukakadiria kodi ya zuio ya pango pamoja na riba.

Ikumbukwe kuwa kuna kanuni za biashara ya kampuni mojawapo ni “separate legal entity “

Kwamba maswala yahusuyo kampuni hayapaswi kuchanganywa na maswala ya mkurugenzi/mmiliki wa hiyo kampuni.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mkuu Ramzy Classic kwa changamoto. Anyway maisha lazima yaendelee.
Majibu yako ni
1. Kwa mwaka 2015, TIN na makadirio
Kwa wakati huo baada ya "kulazimishwa" kulipa kiasi ambacho si stahiki kutokana na biashara yako ambayo wewe binafsi umesema mauzo hayakuwa yanazidi mil 4 kwa mwaka, ungeandika barua kwa meneja wa hilo tawi ulilopata huduma juu ya kupinga makadirio hayo.

LAKINI ANGALIZO HILI LIZINGATIWE
Suala la kuandika barua ya kupinga litakuwa sawa kama na kama tu wakati wa mahojiano ulisema kiwango ambacho Afisa wa kodi akifanya hesabu za mauzo kwa mwaka kinakuwa chini ya mil 4. Hivyo basi kama mauzo ulisema mwenyewe yanakuja zaidi ya mil 4 hiyo ni kosa lako mwenyewe, ulitakiwa ulipe

2. Malipo ya kodi toka 2015......2019
Kama hujaenda kutoa taarifa zozote TRA tambua penati itabaki pale pale kwa muda wote huo ambapo ni sh 225,000 kwa kila mwezi unaoongezeka toka mwezi wa malipo ya kodi. Hivyo tarajia ukienda kukutana na faini hii. Sio nakuogopesha usiende laaah bali tatizo hutatuliwa kwa kukabiliana nalo. Nakushauri nenda kaangalie hali halisi naamini utasikilizwa na kusaidiwa kutatua changamoto hii.

3. Kukadiriwa upya mwaka huu 2019
Ndiyo utakadiriwa upya lkn viporo vya madeni yako vipo pia. Kila mwaka makadirio mapya hufanyika.

4. Kitambulisho vya mjasiriamali
Kama biashara yako ni ndogo sana bhasi ni vema ununue hicho kitambulisho na pia uende TRA kutoa taarifa juu ya mabadiliko ya hali ya kibiashara kuwa biashara yako imekuwa ndogo sana. Nenda na kitambulisho hicho kama ushahidi wa biashara yako ni ndogo sana na hapo elezea na hali halisi ya wakati huo wa makadirio makubwa ambayo hayaendani na biashara yako
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi. Mimi pia hili linanihusu, kwani nilifanya process zote za kupata TIN no. lakini baadae nikapata matatizo, sikufanya tena biashara na TIN sikuchukua. Hapa nafanyaje mkuu? Na kama kuna deni linalipwa kwa mfumo gani? TIN yangu nili-process 2012 mkuu. Nitashukuru kwa maelezo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea.....
MAKALA: SEHEMU YA PILI
Habari za leo
Tuendelee na makala yetu juu ya ulipaji kodi kwa mtu anaeanza kufanya biashara. Katika sehemu ya kwanza tumeangalia mambo mbalimbali kama sheria za kodi, mgawanyiko wa makundi ya biashara, namna ya kuomba TIN na vielelezo vinavyotakiwa ktk kuomba TIN kutoka TRA. Makala ya leo tutaangazia masuala mbalimbali kama ifuatavyo:

1. VIWANGO VYA KODI YA MAPATO
Kodi hii hulipwa kutokana na mapato ya biashara na vinatofautiana kulingana na pato la mtu. Kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato jedwali na. 1 viwango vya kodi vimegawanyika ktk makundi matatu ambayo ni:
kundi la kwanza
Viwango vinavyowahusu wafanyabiashara wadogo wenye mauzo ghafi kuanzia mil 4 hayazidi mil 100 kwa mwaka. Hawa hutozwa kodi kutegemeana na mauzo yao ya mwaka.

Kundi la pili
Viwango vywa wafanyabiashara binafsi ambao mauzo ghafi kwa mwaka ni zaidi ya mil 100. Hawa hutozwa kwa kutegemea faida inayokokotolewa kulingana na kumbukumbu za biashara na hesabu za mizania

Kundi la tatu
Inahusisha makampuni, mashirika, vilabu, ushirika na taasisi zingine na kiwango cha kodi ni 30% ya faida iliyopatikana kwa mwaka

2. UTARATIBU WA KULIPA KODI
Ulipaji wa kodi ya mapato itokanayo na makisio "provison tax" hufanyika kwa awamu nne ambazo ni
Awamu ya kwanza
Kuanzia tarehe 1 Januari hadi 31 Machi

Awamu ya pili
Kuanzia tarehe 1 Aprili hadi 30 Juni

Awamu ya tatu
Kuanzia tarehe 1 Julai hadi 30 Septemba

Awamu ya nne
Kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 31 Disemba

Kuchelewa kulipa awamu yyt kati ya hizo penati yake ni Sh 225,000 kwa kila mwezi unaoongezeka toka awamu husika ipite

3. VIWANGO VYA KODI KWA WAFANYABIASHARA WADOGO WAKAZI
Kwa kuzingatia kifingu cha 35 cha Sheria ya usimamizi wa kodi (utunzaji wa kumbukumbu) kodi zimegawanyika kama ifuatavyo:
(Note: Mauzo ni kwa mwaka, Tsh)
1. Mauzo yasiyozidi mil 4
Hakuna kodi kwa asietunza na anaetunza kumbukumbu

2. Mauzo kati ya mil 4 hayazidi mil 7.0
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu kodi atalipa sh 100,000
b) Kwa anaetunza kumbukumbu kodi atalipa 3% ya mauzo yanayozidi mil 4

3. Mauzo kati ya mil 7.0 hayazidi mil 11.0
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu analipa sh 250,000
b) Kwa anaetunza kumbukumbu atalipa sh 90,000+3.0% ya mauzo yanayozidi mil 7.0

4. Mauzo kati ya mil 11.0 na hayazid mil 14
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu atalipa sh 450,000
b) Kwa anayetunza kumbukumbu atalipa sh 230,000+ 4.0% ya mauzo yanayozidi mil 11.0

5. Mauzo zaidi ya mil 14 hayazid mil 100
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu atalipa sh 450,000
b) Kwa anaetunza kumbukumbu kodi atalipa sh 450,000+ 3.5% ya mauzo yanayozidi mil 14

ZINGATIA KUWA:
1. Endapo mauzo ghafi kwa mwaka yatazidi mil 100 ni LAZIMA KUTENGENEZA HESABU ZA MIZANIA kulingana na biaahara
2. Mlipakodi ambaye mauzo ghafi kwa mwaka yanazidi mil 14 ANATAKIWA KUTUMIA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI ZA KODI (EFD)
3. Mlipakodi mwenye mauzo chini ya mil 14 anatakiwa kutoa risiti ya kuandikwa kwa mkono zenye nakala zikionyesha TIN, Jina la Muuzaji, Jina la mnunuzi, aina ya bidhaa na thamani yake.
Hii ni kwa mujibu wa kifingu na. 36 (3&4) cha sheria ya usimamizi wa kodi

KOSA LA KUTOKUTOA RISITI YA KODI YA ELEKTRONIKI (EFD)
1. Kulipa faini kati ya mil 3 hado 4.5 au kifungo cha miaka mitatu jela
2. Kutozwa faini ambayo itakuwa mara mbili ya kodi iliyokwepwa
3. Kushindwa kudai risiti na hukutoa taarifa adhabu yake ni kati ya sh 30,000 hadi mil 1.5
Hivyo tujitahidi ukiuza TOA RISITI na UKINUNUA DAI RISITI.

ULIPAJI WA KODI YA MAKISIO NA MENGINEYO
Baada ya kupata bili yako ya kulipa kodi ya makadirio/makisio una muda wa siku 90 wa kujipanga kuilipa sehemu (robo ya jumla ya kodi yote). Hivyo basi
1. Utaomba Certificate of Tax Clearance ambayo itakufaa ktk kuombea leseni au vibali kwaujibu wa mahitaji yako.
2. Ili kuipata hii itakulazimu kulipa baadhi ya kodi km kodi ya zuio "withholding tax" ambayo ni 10% ya thamani ya kodi ya pango uliyolipa.
3. Utaulipia mkataba wako ushuru wa stempu ambao ni 1%
Ikumbukwe kama mkataba umechelewa kuasilishwa nje ya mwezi ule uliosainiwa, basi kuna adhabu. (Hili tutaangalia mbele)
Tutaendeleaaa...
Mkuu samahani, naomba ufafanuzi kidogo hapa, unamaanisha aje kusema "utalipa asilimia 3 ya mauzo yanayozidi 4milion"
Je unamaanisha mauzo yakiwa milion 6, hiyo asilimia 3 ya kodi itakua ya milioni 6? Au hapa itakua ya milion 2(kama zidio kutoka kwenye mil4)
Na kama ni asilimia 3 ya milioni 6, si ni bora nisitunze kumbukumbu ili mlipe laki moja tu!
Ahsante.
 
Mkuu samahani, naomba ufafanuzi kidogo hapa, unamaanisha aje kusema "utalipa asilimia 3 ya mauzo yanayozidi 4milion"
Je unamaanisha mauzo yakiwa milion 6, hiyo asilimia 3 ya kodi itakua ya milioni 6? Au hapa itakua ya milion 2(kama zidio kutoka kwenye mil4)
Na kama ni asilimia 3 ya milioni 6, si ni bora nisitunze kumbukumbu ili mlipe laki moja tu!
Ahsante.
Bila samahani
Ufafanuzi: Ni kwamba unalipa ile tofauti (zidio) kati ya mil 6 na 4. ie (6mil-4mil) *3%=60,000

Wakati mfanyabiashara asieweka rekodi atalipa sh 100,000
 
Pitia kitabu hiki kidogo kwa kujiongezea maarifa juu ya kodi. Ni cha lugha ya kiswahili toleo la 2019/2020View attachment 1221404
Mkuu naomba kujua...

1. Kama nimesajili kampuni kama individual (au mmiliki binafsi) je kodi itakua sawa na ile ya Ltd?? Mfano zote zitakua 30%?

2. JE nikisajili kama individual nitaweza vipi kutengenisha mapato ya biashara na yale kazi ajira yangu (salary)?

2. Mfano kampuni yangu inatoa huduma ya uwekezaji kwa watu wa nje (sio watanzania), mfano katika hiyo huduma nimepata 1000usd je hapa nitatakiwa kulipia VAT?

3. Je ikiwa mapato yangu kwa 1st quoter ni hiyo 1000usd, je nitatakiwa lipia kodi gani na gani ikiwa silipii VAT?

4. JE naweza sajili coorporate au ltd company alafu nikawa na share 95% alafu wengine wawili wakawa na share 2.5% kwa 2.5%?

5. Je kuna tofauti gani kati ya share holders na directors?? Je, minimumly, share holders wanatakiwa kuwa wangapi na directors wanatakiwa kuwa wangapi?

6. Je katika ugawaji wa faida, ni muda gani faida inatakiwa ku gaiwa? Kila mwezi au kila mwaka?

7. Je ikiwa faida imegaiwa je walio pata mgao wa faida watatakiwa kulipia kodi % ngapi katika faida waliyo pata?

8. Je kuna tofauti gani kati ya "individual" na "coorpotare/Ltd" in terms of mgawanyo wa faida na malipo ya kodi?

9. Je nikisajili kama individual naweza kuja badalisha kwenda coorporation/Ltd kwa badae?

Naomba kuwasilisha!
 
Mkuu naomba kujua...

1. Kama nimesajili kampuni kama individual (au mmiliki binafsi) je kodi itakua sawa na ile ya Ltd?? Mfano zote zitakua 30%?

2. JE nikisajili kama individual nitaweza vipi kutengenisha mapato ya biashara na yale kazi ajira yangu (salary)?

2. Mfano kampuni yangu inatoa huduma ya uwekezaji kwa watu wa nje (sio watanzania), mfano katika hiyo huduma nimepata 1000usd je hapa nitatakiwa kulipia VAT?

3. Je ikiwa mapato yangu kwa 1st quoter ni hiyo 1000usd, je nitatakiwa lipia kodi gani na gani ikiwa silipii VAT?

4. JE naweza sajili coorporate au ltd company alafu nikawa na share 95% alafu wengine wawili wakawa na share 2.5% kwa 2.5%?

5. Je kuna tofauti gani kati ya share holders na directors?? Je, minimumly, share holders wanatakiwa kuwa wangapi na directors wanatakiwa kuwa wangapi?

6. Je katika ugawaji wa faida, ni muda gani faida inatakiwa ku gaiwa? Kila mwezi au kila mwaka?

7. Je ikiwa faida imegaiwa je walio pata mgao wa faida watatakiwa kulipia kodi % ngapi katika faida waliyo pata?

8. Je kuna tofauti gani kati ya "individual" na "coorpotare/Ltd" in terms of mgawanyo wa faida na malipo ya kodi?

9. Je nikisajili kama individual naweza kuja badalisha kwenda coorporation/Ltd kwa badae?

Naomba kuwasilisha!
Upepo wa Pesa
1. Usajili:
Unaposema kampuni una maana ni yenye ukomo ie Limited Company? Kwa sababu kwa sheria za usajili wa makampuni ya mwaka 2002 huwezi kusajili kampuni yenye ukomo ya mwanahisa mmoja pekee. Hivyo bhasi swali lako ungeuliza kwamba je kodi ya mtu binafsi ni sawa na kodi za kampuni yenye ukomo? Jawabu lake ni hapana si sawa. Kampuni yenye ukomo ni 30% wakati kwa mtu binafsi inategemea na kiwango cha mapato

2. Mapato ya biashara vs Mapato kutokana na ajira
Swali lako halijawa lenye ufafanuzi wa kutosha maana unasema kutengenisha mapato kwa muktadha upi? "Be specific".

3. Ulipaji kodi ya Ongezeko la Thamani ie VAT
Sio kila kampuni inalipa VAT. Utatakiwa kulipa VAT kama umekidhi vigezo vya kisheria kwa mujibu wa sheria ya ongezeko la kodi ya thamani ya mwaka 2014 ambapo unaweza sajiliwa VAT kama una mauzo yanayofikia au kuzidi mil 100 kwa mwaka au kampuni ya utaalam mfano engineering, accountants etc. Kama unakidhi vigexo hivyo utalipa

4. Ulipaji kodi kwa awamu
Hili nakushauri rejea mada pale juu uone namna gani kodi inalipwa na kodi zipi na zinalipwa kwa vipindi gani kwa ufafanuzi wa kina. Lakini kwa kifupi ni 1. Utajikadiria na kulipa awamu nne za usawa iwapo mauzo yamepanda au kushuka una haki ya kuomba marekebisho ya makadirio ie revise estimates, kama una wafanyakazi kuanzia 10 utatakiwa kulipa kodi ya ufundi ie SDL kila mwezi, Mishahara kama ni kuanzia 270,000+ baada ya makato ya mchango wa mfuko wa jamii utalipa kodi ya zuio ie PAYE kila mwezi, kodi za mikataba, ushuru wa stempu et al

5. Umilikiwa hisa katika kampuni yenye ukomo
Jawabu ni ndiyo unaweza kumiliki hadi 99% na 1% ukampa mwingine kukidhu matakwa ya kisheria

6. Mwanahisa (shareholder) vs Mkurugenzi (Director) na idadi ya watu katika kufungua kampuni yenye ukomo
Idadi ni kuanzia watu wawili na mwisho ni watu 50. Mwanahisa ni mmiliki wa sehemu ya kampuni na mkurugenzi ni mtendaji katika kampuni. Sio lazima mkurugenzi akawa mwanahisa kwn unaweza kumwajiri mkurugenzi nje ya wamiliki wa kampuni

7. Ugawaji wa faida
Inategemea na mfumo wa kampuni wa ugawajinjapo mara nyingi huwa mwisho wa mwaka baada ya kufunga mahesabu ya mwaka then faida ikishajulikana bhasi kuna sehemu ya faida hurudishwa katika kampuni na sehemu hugawiwa kwa wanahisa. Kiwango cha mgawanyiko wa faida hiyo kwa kila mwanahisa hutegemea na idadi ya hisa ambazo mwanahisa anamiliki ndani ya kampuni

8. Mgao wa faida ni 10%

9. Mtu binafsi vs Kampuni yenye ukomo: Faida na kodi
Mtu binafsi hana hana mgawanyiko wa faida na kodi atalipa baada ya ukokotoaji wa kodi na itategemea anaweka kumbukumbu au haweki kumbukumbu. Ukija upande wa kampuni ni 30% kodi na faida hugawanya kwa mujibu wa idadi ya hisa zinazomilikiwa na wanahisa

10. Inakubalika ukisajili jina la biashara baadae kubadilisha kuwa kampuni yenye ukomo

Angalizo: Huenda kuna maswali nimejibu ndiyo siyo kutokana na namna ulivyouliza kwani hayaeleweki kutokana na kuwa na mkanganyiko wa muundo wa maswali yako.

Pia wachangiaji wengine wapo huru kuongeza zaidi maelezo, ufafanuzi na hata kukosoa makosa ya majibu na kuleta majibu sahihi zaidi

Wasalaam
 
2. Mapato ya biashara vs Mapato kutokana na ajira
Swali lako halijawa lenye ufafanuzi wa kutosha maana unasema kutengenisha mapato kwa muktadha upi? "Be specific".
Nilicho maanisha ni kwamba kama nitaisajili kama "individual" na sio Ltd, je mapato ya kampuni hayata weza kuchanganywa na mapato yangu binafsi mfano mshahara ua biashara nyingine nnazo fanya wakati wa kulipa kodi?

Maana ulisema ukisajili kampuni kama individual basi panakua hakuna separation kati ya mtu na biashara!
 
Back
Top Bottom