Makalla atua Katavi na kusema Watasikiliza kero za Wananchi lakini siyo zile zilizopo Mahakamani

Huyu makonda atakuja kuwa kama job, maana atakosa upande. Amejichanganya sana. Mara anatetea wanyonge mara anasimama na mama yake hataki asemwe kwa mabaya. Atajikuta anaishia kujiuzulu
Sahihi
 
Awapo ndio nini mleta mada?
awapo = whenever (njeo ya wakati usio dhahiri, ujirudiao).

Pia humaanisha ^wakati wowote^ unaorejelea tukio husika, au tukio linalojirudia.

Whenever he speaks, people are happy.

1. [Wakati wowote] azungumzapo, watu hupata furaha.

2. Azungumzapo watu hupata furaha.

3. Awapo katika mazungumzo, watu hupata furaha.
 
MAKALA YUPO SAHIHI YULE MWINGINE NI KICHAA
 
Kesi iko mahakamani unataka mwenezi aamue kama nani? Jaman majukum ya mahakama yaachwe huko huko
 
Ulichokielezea wewe hakiendani na mantiki ya mtoa hoja.
'Awapo' yake alimaanisha ...'hawapo'...
Kwa viswahili vyao vya 'akuna' nk nk.
 
Hata kama issue iko mahakamani, si aelezee position au maamuzi sahihi yanayitakiwa kufanyika? Mbona Waziri wa Ardhi, Jerry Slaa, amekuwa akieleza waziwazi kuwa wasimazi wa mirathi hawana authority kuuza ardhi au majengo ya mirathi, na mahakama zimekuwa zikibariki ardhi au majengo yaliyouzwa na wasimamizi wa mirathi, sasa kama hiyo elimu isingetolewa, wasimamizi wa mirathi wangeendelea kudhulumu.
 
Walimu huwa mna mbwembwe sana!
 
Jamaa cha wapiga dili tupu
 
Safi sana
Naamini kweli Nchimbi ana akili.

Sio upuuzi ule uliokuwa unafanywa kwa watu kuingilia mhimili wa Mahakama as if Tanzania ni banana Republic na haina Katiba wala Sheria
 
Ulichokielezea wewe hakiendani na mantiki ya mtoa hoja.
'Awapo' yake alimaanisha ...'hawapo'...
Kwa viswahili vyao vya 'akuna' nk nk.
Nadhani wewe ndiye hukumwelewa muuliza-swali.

Muulizaji akiungana na wewe katika hili, basi naye atakuwa hajielewi. 😂😂😂
 
Mkuu, huko ni kukwepa uwajibikaji. Tuliosomea Q-ba tushamsoma mwenezi kitambo.
 
Umeishia darasa la ngapi?

Unajua maana ya (Independence of Judiciary) Uhuru wa Mahakama?

Unajua maana ya Les subjudice?

Au watu waanze kukupa darasa hapa ili ujione kuwa wewe ni kilaza wa mwisho duniani?
 
Jamani, hivi kwa sasa watanzania, wengi, mumechanganyikiwa Sana. Hivi, kweli unaweza, kuandika Uzi mrefu kama gazeti, na ukaongea uongo mtupu. Ni lini na wapi Makonda alisema au aliingilia, issue za mahakamani? Nakumbuka Makonda alisema tena akiwa Njombe, kuwa watanzania wasikimbilie mahakamani. Lakin hakuingilia kesi za mahakamani. Yaan hoja yako muhimu ni kutaka kumsifia bumunda,, Makalla. Pole Sana.
 
Nadhani wewe ndiye hukumwelewa muuliza-swali.

Muulizaji akiungana na wewe katika hili, basi naye atakuwa hajielewi. 😂 Emb jaribu kusoma thread ili uone mantiki ya mtoa mada katika muktadha huo.
Mkuu imekuwaje tena!

Kiswahili ni lugha yetu bhana.

Rudia kusoma thread ili uone mantiki ya mwandishi katika muktadha wake.

Wewe umekuja kutafsiri kwa usahihi 'kitenzi' kilichokwisha kukosewa.

Sasa, tafsiri yako sahihi kwa neno lililokosewa haiwezi kuhalalisha makosa ya matumizi ama makosa ya uandishi wa neno husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…