Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Hii model inafaa hapa nyumbani pia.
 
Inafaa nini ikiwa ana paralyze uchumi, jinga kabisa.Kama retired senior government leader he must know better than that. Useless

Hiyo nyomi inamwuunga mkono nyumbani Kenya:



Kwamba wewe Nanjilinji Kilwa huko ndiyo anakukera?

Kwani wale vijana wa hovyo watakuwa nani basi?
 
Kuna madikteta ulimwengu huu walikuwa na nguvu, jeshi imara na mkono wa chuma lakini pale wananchi walipochoka ilibidi watawala hao wakimbie tena kwa kutumia baibui.

Ogopa sana nguvu ya umma hata uwe na jeshi imara kiasi gani wananchi wakiamua lao hakuna wa kuwazuia.

Hapa kwetu bado watu hawajaamua ila kila kitu kina mwanzo wake.

Hawa vijana wanaozaliwa sasahivi waliokata tamaa ya maisha na ukosefu wa ajira ni bomu linalokuja. Tuombe uzima tutashuhudia ambayo hatukuwahi kufikiria kama yanaweza kutokea.
 
Hapa home ni ngumu hadi mvunje like agano la kichawi (la Mwenge) aliloimgia yule babu anaedaiwa kuwa mwanzilishi wa hii nchi lililopumbaza na linaloendelea kupumbaza wananchi wake! Period
 
Hiyo nyomi inamwuunga mkono nyumbani Kenya:

View attachment 2560028

Kwamba wewe Nanjilinji Kilwa huko ndiyo anakukera?

Kwani wale vijana wa hovyo watakuwa nani basi?
Angalia vitu katika big picture. Kuungwa mkono siyo issue, unaungwa mkono na nani. Sehemu kubwa ya hiyo halaiki ni ignorant, with little or no knowledge.
 
Unaamini umma ukiamua kuandamana kuna polisi atakayethubutu kuzuia?

Wote watakimbia kunusuru maisha yao mkuu.

Rejea nchi mbalimbali namna watawala walivyolewa madaraka wakaamini hakuna mbwa atakasogea barabarani kwakuwa watatumia jeshi kuwapa kichapo lakini siku isiyotarajiwa waliacha starehe zote walizozoea kuponda nakukimbia makazi yao ya kifahari.
 
Yaan daaaa
Bidhaa zimepanda bei, umeme unakatika Mara kwa mara, huduma za jamiii hazitolewi kwa usawa, ili kupata kazi lazima uwe na connection sio suala la kuwa na sifa Tena hiyo amani unayojivunia ni ipi?
 
Issue sio makamanda. Issue ni sisi watanzania. Unafikiri mtanzania ataandamana akitishiwa bomu la machozi? Sisi waoga, period. Naomba waniprove wrong. Nitafurahi.

Sisi siyo waoga na issue ni sisi makamanda:

1. Kwanini tunahangaika na vijana wa hovyo? Kuwalalamikia waoga ni kuhangaika na vijana wa hovyo.
2. Raila hataki wavae sare za vyama kwa suala la wakenya. Tusinyoosheane vidole hapa. Hili si la Chadema, ACT, CUF au Rungwe. Hili ni la watanzania.
3. Tusimkere anayeweza kuwa mshirika. Tuwe na Kauli thabiti za kuwaongelea watanzania siyo kuwakwaza
4. Nk

Rejea #1 - #9 pale PoSt #192 kuona tunapokwama.
 
Watoto wake mpaka sasa wako nje ya nchi wakifuatilia maandamano kupitia kwenye TV.
Kwahiyo hata Winnie Odinga yupo nje ya nchi?

Unafuatilia mambo kweli wewe? Winnie ni mbunge wa bunge la Afrika mashariki na jana ameamka asubuhi kwenye mji wa Kisumu alikokuwa anaongoza maandamano akakuta vifaa vyake vyote vya mawasiliano vimefungwa ili asihamasishe wafuasi wake.
 
Bidhaa zimepanda bei, umeme unakatika Mara kwa mara, huduma za jamiii hazitolewi kwa usawa, ili kupata kazi lazima uwe na connection sio suala la kuwa na sifa Tena hiyo amani unayojivunia ni ipi?
Hii hii ya kutokuuana inatosha mkuu
 
Odinga atulizane. Kuendesha nchi si kitu rahisi. Amuunge mkono na kumsaidia kumpa ushauri na mengineyo mwenzake.
 
Angalia vitu katika big picture. Kuungwa mkono siyo issue, unaungwa mkono na nani. Sehemu kubwa ya hiyo halaiki ni ignorant, with little or no knowledge.

Kwamba kuungwa mkono si issue? Kwani democracy ni nini? Hukuwahi kusikia wengi wape vinginevyo watachukua kwa nguvu. Hiyo ndiyo demokrasia sasa. Wewe huna uungwaji mkono tambua kuwa huna hoja!
 
Chadema ni Slaa pekee alikuwa anaweza kuwafanya watu waandamane hawa wengine hawana nguvu na ni waoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…