Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Yapo mengi ya kujifunza kwa nguli mpigania haki huyu:

1. Kutambua siasa ni sayansi yenye kubadilika kulingana na mazingira.
2. Hakuna rafiki wala adui wa kudumu bali agenda.
3. Maandamano yasiyo na ukomo ndiyo njia pekee ya kupata tunachohitaji na kwa wakati.
4. Hakuna nguvu iliyo kuu kuizidi nguvu ya Umma.
5. Maandamano hupangwa na kuratibiwa kikamilifu kuweza kufanikiwa na hata kufika kuliko dhamiriwa.
6. Maandamano hayawezi kuja spontaneous kama mvua.
7. Kwenye maandamano huwa casualties hawakosekani na anaweza kuwa awaye yote.
8. Raila au wakenya katika Mapambano si wajinga wanayo hoja na wanakijua wanachokipigania.

View attachment 2559513

Mafunzo mengine karibuni tuongezee.

View attachment 2559510

"Hatuna haja ya kupoteza muda na vijana wa hovyo."

Hadi hapo:

"Shikamoo Raila Amolo Odinga."
Hii model inafaa hapa nyumbani pia.
 
Inafaa nini ikiwa ana paralyze uchumi, jinga kabisa.Kama retired senior government leader he must know better than that. Useless

Hiyo nyomi inamwuunga mkono nyumbani Kenya:

Screenshot_20230321-071500.jpg


Kwamba wewe Nanjilinji Kilwa huko ndiyo anakukera?

Kwani wale vijana wa hovyo watakuwa nani basi?
 
Nakumbuka makamanda waliambiwa kwenye maandamano wakae mbele ili wamwagwe mkojo vizuri...tangia hapo wakapoteana mazima [emoji4][emoji4]
Viongozi wenu walizoea kutanguliza masikini kama chambo huku wao wanatafuna ruzuku wakakutanana na Chuma. No asali ni pumzi ya moto tu [emoji28][emoji28][emoji91][emoji91][emoji91]
Kuna madikteta ulimwengu huu walikuwa na nguvu, jeshi imara na mkono wa chuma lakini pale wananchi walipochoka ilibidi watawala hao wakimbie tena kwa kutumia baibui.

Ogopa sana nguvu ya umma hata uwe na jeshi imara kiasi gani wananchi wakiamua lao hakuna wa kuwazuia.

Hapa kwetu bado watu hawajaamua ila kila kitu kina mwanzo wake.

Hawa vijana wanaozaliwa sasahivi waliokata tamaa ya maisha na ukosefu wa ajira ni bomu linalokuja. Tuombe uzima tutashuhudia ambayo hatukuwahi kufikiria kama yanaweza kutokea.
 
Hapa home ni ngumu hadi mvunje like agano la kichawi (la Mwenge) aliloimgia yule babu anaedaiwa kuwa mwanzilishi wa hii nchi lililopumbaza na linaloendelea kupumbaza wananchi wake! Period
 
Hiyo nyomi inamwuunga mkono nyumbani Kenya:

View attachment 2560028

Kwamba wewe Nanjilinji Kilwa huko ndiyo anakukera?

Kwani wale vijana wa hovyo watakuwa nani basi?
Angalia vitu katika big picture. Kuungwa mkono siyo issue, unaungwa mkono na nani. Sehemu kubwa ya hiyo halaiki ni ignorant, with little or no knowledge.
 
Tanzania hatuwezi kukubali ujingaa huu utokee mpaka pale wale wanaohimiza maandamano wawepo mbele ya mstari na familia zao.

I mean hauwezi kuandaa mandamano afu siku ya kuandamana ushinde kwenye TV na familia yako ukiwaangalia uliowarubuni wakila mkong'oto kutoka kwa polisi brutal.
Unaamini umma ukiamua kuandamana kuna polisi atakayethubutu kuzuia?

Wote watakimbia kunusuru maisha yao mkuu.

Rejea nchi mbalimbali namna watawala walivyolewa madaraka wakaamini hakuna mbwa atakasogea barabarani kwakuwa watatumia jeshi kuwapa kichapo lakini siku isiyotarajiwa waliacha starehe zote walizozoea kuponda nakukimbia makazi yao ya kifahari.
 
Yaan daaaa
Bidhaa zimepanda bei, umeme unakatika Mara kwa mara, huduma za jamiii hazitolewi kwa usawa, ili kupata kazi lazima uwe na connection sio suala la kuwa na sifa Tena hiyo amani unayojivunia ni ipi?
 
Issue sio makamanda. Issue ni sisi watanzania. Unafikiri mtanzania ataandamana akitishiwa bomu la machozi? Sisi waoga, period. Naomba waniprove wrong. Nitafurahi.

Sisi siyo waoga na issue ni sisi makamanda:

1. Kwanini tunahangaika na vijana wa hovyo? Kuwalalamikia waoga ni kuhangaika na vijana wa hovyo.
2. Raila hataki wavae sare za vyama kwa suala la wakenya. Tusinyoosheane vidole hapa. Hili si la Chadema, ACT, CUF au Rungwe. Hili ni la watanzania.
3. Tusimkere anayeweza kuwa mshirika. Tuwe na Kauli thabiti za kuwaongelea watanzania siyo kuwakwaza
4. Nk

Rejea #1 - #9 pale PoSt #192 kuona tunapokwama.
 
Watoto wake mpaka sasa wako nje ya nchi wakifuatilia maandamano kupitia kwenye TV.
Kwahiyo hata Winnie Odinga yupo nje ya nchi?

Unafuatilia mambo kweli wewe? Winnie ni mbunge wa bunge la Afrika mashariki na jana ameamka asubuhi kwenye mji wa Kisumu alikokuwa anaongoza maandamano akakuta vifaa vyake vyote vya mawasiliano vimefungwa ili asihamasishe wafuasi wake.
 
Bidhaa zimepanda bei, umeme unakatika Mara kwa mara, huduma za jamiii hazitolewi kwa usawa, ili kupata kazi lazima uwe na connection sio suala la kuwa na sifa Tena hiyo amani unayojivunia ni ipi?
Hii hii ya kutokuuana inatosha mkuu
 
Odinga atulizane. Kuendesha nchi si kitu rahisi. Amuunge mkono na kumsaidia kumpa ushauri na mengineyo mwenzake.
 
Angalia vitu katika big picture. Kuungwa mkono siyo issue, unaungwa mkono na nani. Sehemu kubwa ya hiyo halaiki ni ignorant, with little or no knowledge.

Kwamba kuungwa mkono si issue? Kwani democracy ni nini? Hukuwahi kusikia wengi wape vinginevyo watachukua kwa nguvu. Hiyo ndiyo demokrasia sasa. Wewe huna uungwaji mkono tambua kuwa huna hoja!
 
Odinga nae ni njaa na uchoyo wa madaraka hana jipya la maana!!, Huyu sio aliyelambishwa asali na kibaki?.

Afu Kenya ni Nchi ya watu hai sio watu mfu Kama ninyi Tz!!, Watu ambao sukari imetoka kuuzwa kwa kilo 1600 hadi 3000 huku mchele ukiuzwa Mara mbili ya awali!!. Unategemea Mbowe au Lema ambao wanaweza kuitwa ikulu wakahakikishiwa kila mwezi 20m+ ndio waingie barabarani kufanya maandamano huku kapuku anachekelea bila kujali!!.
Chadema ni Slaa pekee alikuwa anaweza kuwafanya watu waandamane hawa wengine hawana nguvu na ni waoga.
 
Back
Top Bottom