Makamba na nongwa za bodi ya TANESCO, ni marudio ya awamu nyingine japo yalifanyika kimya kimya

Makamba na nongwa za bodi ya TANESCO, ni marudio ya awamu nyingine japo yalifanyika kimya kimya

Sijasema watu wa JPM walikuwa wachafu, nimeongelea juhudi za makusudi za kuficha huo uchafu kwa kutumia media na hata kwa nguvu ya haiba ya JPM mwenyewe.

Aliwashindwa baadhi ya watu mfano ni Paul Makonda na wengine wachache wa karibu yake. Ujue kuwa JPM alipenda kuwa na msiri wa nyumbani kwake ambaye angeweza kuuanika wazi udhaifu wake wote, hii ni sifa ambayo sio kila mtu mwenye kuweza kuifikia.
mlimshindwa vp makonda? kwani makonda aliondolewa na nani madarakani. nipe kosa moja la makonda ambalo unahisi alistahili kufukuzwa
 
mtoa post SIO KWELI KWAMBA WAKATI WA JPM HAKUKUWA NA UWAZI SIKUBALIANI NA WEWE kwa sababu mambo yalikuwa yanakwenda vizuri tena kwa vitendo sio maneno ushuhuda wa utulivu katika mambo ya umeme tunao na utumiaji wa majenereta ulipungua na huo ndio ukweli wenyewe na tunategemea kuendelea kuona utulivu huo na zaidi, tofauti na hapo msije kutuletea sababu dhaifu ya kusema sijui mambo yalikuwa yanafichwa na sasa yako wazi HUO NI UONGO.
 
Uzi mzuri, watu hawakujua yaliyojiri wakati wa mwendazake kwani vyombo vyote vilikuwa vinaimba mapambio tu. Watulie waone nchi ikipaa.
waandike basi sasa tujue kama walizibwa kipindi hicho
 
Ndio maana nikasema kila mtu anayo mabaya yake na mema yake. Mafuru anaangukia katika kundi hilo, kumbuka kimtazamo hakufanana na rais JPM. Kwa maana ya rais kuwaogopa wafanyabiashara huku akiwa na kundi lake analotaka lifaidike.

Kwa ufupi kwenye haya maisha ukiondoa Mama yako anayetumia tumbo lake kama njia ya wewe kufika hapa duniani usimuamini mtu yoyote yule baki.
Mkuu kuna vitu ukifanya vinaenda beyond repair....
Leo hii unaiona Nchi ya china ilipofikia na tunaisifia kama moja ya super power ukae ukijua hawakufika hapo kwa bahati mbaya...hawacheki na wezi kama ninyi...
Maana yake ni kwamba hao watu unaowatetea wasingekuwepo duniani kuendelea kupunguza oxygen levels...nadhani umenielewa.
 
mtu kaiba alafu unampa 2nd chance. afrika ni shida sana na haitoendelea. china huo upuuzi hamna na wanakupoteza tu
Msingi wa China na ule wa Tanzania ni vitu viwili tofauti. Unaweza kuwa na mwizi mbunifu na mwenye maono kuliko mwaminifu ambaye ni mtupu kichwani.
 
Mkuu kuna vitu ukifanya vinaenda beyond repair....
Leo hii unaiona Nchi ya china ilipofikia na tunaisifia kama moja ya super power ukae ukijua hawakufika hapo kwa bahati mbaya...hawacheki na wezi kama ninyi...
Maana yake ni kwamba hao watu unaowatetea wasingekuwepo duniani kuendelea kupunguza oxygen levels...nadhani umenielewa.
Hizi ni dhana za hayati JPM, unaweza kuziona kama vile ni zenye haki kumbe upande wa pili ni ukatili unaohalalishwa mchana kweupe.
 
mlimshindwa vp makonda? kwani makonda aliondolewa na nani madarakani. nipe kosa moja la makonda ambalo unahisi alistahili kufukuzwa
Kuvamia clouds FM muda wa kazi na kuwanyanyasa wafanyakazi wakitimiza wajibu wao mpaka akagombana na RIP Ruge Mutahaba.

Kuwanyanyasa wafanyakazi waliokuwa chini yake mpaka wakapatwa na mshtuko wa moyo mbele ya kamera za runinga yaani live.
 
mtoa post SIO KWELI KWAMBA WAKATI WA JPM HAKUKUWA NA UWAZI SIKUBALIANI NA WEWE kwa sababu mambo yalikuwa yanakwenda vizuri tena kwa vitendo sio maneno ushuhuda wa utulivu katika mambo ya umeme tunao na utumiaji wa majenereta ulipungua na huo ndio ukweli wenyewe na tunategemea kuendelea kuona utulivu huo na zaidi, tofauti na hapo msije kutuletea sababu dhaifu ya kusema sijui mambo yalikuwa yanafichwa na sasa yako wazi HUO NI UONGO.
Siwezi kusema kwamba RIP Magufuli hakufanya kazi kubwa ya kuinyoosha serikali, alikuwa na udhaifu wake kama mimi na wewe tunavyokuwa nao tunapopewa madaraka makubwa.
 
Unajua hata JPM ni mteule wa JK? Nae ni fisadi sio??

Vyombo gani vya ulinzi vinapambana nchi isianguke? Hivi nyie watu mnapenda sana kujilisha matango pori kumbe?[emoji23][emoji23][emoji23]

Nchi inaangukaje wakati uchumi unakuwa? Biashara zinazidi kufunguka? Miradi inaendelea tena kwa kasi ya ajabu? Takwimu za biashara zinatubeba na sasa tunauza Kenya na Uganda kuliko wao wanavyouza kwetu?

Hizo chuki zenu na Kikwete ambazo mmeziamishia kwa Samia na Wateule wake hazitawafikisha popote chato gang!

Kwa kifupi nyie wote mmejaaa chuki tu hamna hoja yeyote!
Ukweli mchungu kwakweli masoko yamefunguka saiz Kila nafaka inauzika tofaut na enzi za JPM
 
Watu waibe kwa makusudi unasema kula nao sahani moja ni ukatili.?...Ok ila nikuhakikishie siku yaja...
Kumbuka kuweka akiba ya maneno siku zote, ukija kumjua unayemuamini kuwa ni mkweli utajikuta unao unyonge usioweza kuandikwa hadharani.
 
With due respect....unasema watu wanawahisi vibaya..hivi mkuu are serious?...watu wana full data mzee tena solid evidence....
Ni vyema ukawaweka akiba ya maneno otherwise utakuja kupata aibu
..Nikuulize swali dogo tu unajua kwa nini Mafuru aliondoka NBC?....kama hujui find out....watu hawabahatishi.
Halafu Mafuru akawa Treasury Registrar mwaka 2015, acheni hizo hisia. Mtu yeyote anabakia innocent mpaka Mahakama iseme ana hatia. Hili lipo kwenye Katiba ya JMT ya mwaka 1977, toleo la 2000.

DURACEF leta uwongo mwingine
 
Siwezi kusema kwamba RIP Magufuli hakufanya kazi kubwa ya kuinyoosha serikali, alikuwa na udhaifu wake kama mimi na wewe tunavyokuwa nao tunapopewa madaraka makubwa.
sentensi yako ya usiri na uwazi IMENISHANGAZA

NI YA UONGO

JPM atakumbukwa kwa kuwa kiongozi wa kwanza Tanzania kuweza kuondoa viongozi kwa ubadhirifu bila kupepesa macho wala kumuonea mtu aibu/ haya.

UKWELI UTABAKI KUWA TAIFA LILIMPOTEZA KIONGOZI MAKINI PERIOD.
 
Hakuna mtu anayepinga juu ya yeye kuwa kiongozi makini, watu wanapinga juu ya huo 'utakatifu' bandia anaovyikwa siku zote anapozungumziwa.
 
Halafu Mafuru akawa Treasury Registrar mwaka 2015, acheni hizo hisia. Mtu yeyote anabakia innocent mpaka Mahakama iseme ana hatia. Hili lipo kwenye Katiba ya JMT ya mwaka 1977, toleo la 2000.

DURACEF leta uwongo mwingine
Unasema nasema uongo wakati hujajibu swali......nitake radhi mzee sibahatishi.
 
Uwezo wa watanzania ni kulalamika kwa vitendo, kwa kutumia ushahidi wa video zilizopita. Yaani ilimradi walalamike, waweke hisia zao wazi ndio huwa furaha yao kuu. Tangu JPM alale usingizi wake wa milele, kuna wanaoishi kwa hasira na majonzi yasiyosemeka. Kila ambacho Mama atakifanya kitaonekana kama kimefanywa na JK kwa mlango wa nyuma.

Bodi mpya ya TANESCO baada ya kuwa imeshajulikana hadharani zimeibuka nongwa za kila aina. Yanasemwa mengi na yote yanamtia hatiani Mama Samia kwa njia moja au nyingine. Kwamba hawezi kuteua watu mpaka apate kwanza baraka za JK.

Kuna pande mbili za wanaosemwa sana mitandaoni. Kwamba wawe wabunifu maana kwa hatua ya kwanza kabisa mpaka wao wakarudishwa na kupewa vyeo vya juu ni ubunifu ulioacha alama wa siku zilizopita. Pia maoni hasi juu ya kwanini wapewe vyeo walivyonavyo sasa japo walishachafuka, ni ukweli kwamba uaminifu wao sio mzuri mpaka leo. Kwamba madudu yao yanaendelea kufuata siku zote, rekodi zao zimeshachafuka na uchafu huo unatokana na rekodi zao za nyuma zinavyosomeka.

Hawa wenye wepesi wa kulalamikia juu ya rekodi hizo chafu za hawa wateule wapya wa Mama Samia wanachoshindwa kufahamu ni kuwa hata JPMa alipowaondoa hawa wa sasa aliwaweka wale alionao na sauti juu yao. Aliondoa kundi moja la wapigaji akaja na kundi jingine lenye kufanya uchafu ule ule lakini hakukuwa na uwazi wa vyombo vya habari wa kuweza kuuanika.

Hivyo jamii haijatendewa haki kwani inafahamu uchafu wote wa watendaji wa zamani wa JK lakini haifahamu uchafu wa wale waliokuwa ni wa JPM. Hayati hakuwa msafi kama tunavyojaribu kujulishwa kwenye media, la hasha. Uchafu wa watu wa JK unatokana na maamuzi yake na utayari wa kuweka kila kitu wazi.

Hivyo ni matarajio ya wadau wa sekta ya umeme kuwaona watendaji waliokuwa wachafu na bado ikaonekana wanafaa kupewa vyeo hivyo, wakiwa na uhuru na utendaji wenye ufanisi kuliko ile awamu ya kwanza walipochafuka na kuchafuliwa zaidi watu wakiaminiswa ni wachafu kumbe ni uchafu wa kisiasa unaopewa kipaumbele kuliko ule halisia.

Waitumie hii fursa ya pili waliyopewa na Mama Samia kwa kuwaonyesha wenye wasiwasi na utendaji kazi wao kwamba ni mawazo potofu kuamini kuwa wanatakiwa watiliwe shaka milele yote.

Kuna watu wamenuna na muda wote kosa dogo wapo tayari lionekane ni kubwa sana, hii ni kutokana na kuishi tofauti na matarajio yao. Ghafla tu wamelazimika kuwa wapole huku wakichekea machoni tu, wanalolishauri linaweza kuonekana ni la kweli na la dhati ya moyoni kumbe linao mtego wa hatari ndani yake.

Wajumbe wapya wa bodi ya TANESCO, wapige kazi kadri wawezavyo pasipo kujaziwa mabegani zile shauku na mioyo ya hasira kutoka kona mbalimbali za wanajamii.
Kazi ipo....
 
Unasema nasema uongo wakati hujajibu swali......nitake radhi mzee sibahatishi.
Kuhusu NBC mwajiri aliamua ku "part terms" na Mafuru ndiyo maana akawa eligible for Treasury Registrar post. Mengine ni majungu ya vijiweni
 
Back
Top Bottom