Makamba na nongwa za bodi ya TANESCO, ni marudio ya awamu nyingine japo yalifanyika kimya kimya

Makamba na nongwa za bodi ya TANESCO, ni marudio ya awamu nyingine japo yalifanyika kimya kimya

Unajua wabongo Kuna muda sisi wenyewe ni tatizo.
Kiuhalisia kabisa unaweza vipi mteua mtu ambaye anawakilisha kampuni zenye kesi na Tanesco?
Kipindi hicho Makamba mwenyewe alikiri hilo suala la Maajar na rex attorneys yake. Akaenda mbali kabisa na kushangaa imekuwaje JK kamteua mtu huyo kuwa balozi. Anyway.......
Asante kwa kutukumbusha ujinga wa mtu.
 
Kama hujui 2025 ni Mama tena. Sisi hatutaki nyie Sukuma Gang kutawala tena. Lengo letu msitawale milele.
Pumbavu kabisa,una Vita na kabila au waungaji mkono wa magu,tambua kuwa Hilo genge Ni kubwa kuliko mnavyo dhania umma unasubiri mfanye chini ya kiwango Cha Magufuli. Wote wanakuwa sukuma gang sijui Ni kwa vipi utawazuia! Ulishawahi kujiuliza hilo?
 
Uwezo wa watanzania ni kulalamika kwa vitendo, kwa kutumia ushahidi wa video zilizopita. Yaani ilimradi walalamike, waweke hisia zao wazi ndio huwa furaha yao kuu. Tangu JPM alale usingizi wake wa milele, kuna wanaoishi kwa hasira na majonzi yasiyosemeka. Kila ambacho Mama atakifanya kitaonekana kama kimefanywa na JK kwa mlango wa nyuma.

Bodi mpya ya TANESCO baada ya kuwa imeshajulikana hadharani zimeibuka nongwa za kila aina. Yanasemwa mengi na yote yanamtia hatiani Mama Samia kwa njia moja au nyingine. Kwamba hawezi kuteua watu mpaka apate kwanza baraka za JK.

Kuna pande mbili za wanaosemwa sana mitandaoni. Kwamba wawe wabunifu maana kwa hatua ya kwanza kabisa mpaka wao wakarudishwa na kupewa vyeo vya juu ni ubunifu ulioacha alama wa siku zilizopita. Pia maoni hasi juu ya kwanini wapewe vyeo walivyonavyo sasa japo walishachafuka, ni ukweli kwamba uaminifu wao sio mzuri mpaka leo. Kwamba madudu yao yanaendelea kufuata siku zote, rekodi zao zimeshachafuka na uchafu huo unatokana na rekodi zao za nyuma zinavyosomeka.

Hawa wenye wepesi wa kulalamikia juu ya rekodi hizo chafu za hawa wateule wapya wa Mama Samia wanachoshindwa kufahamu ni kuwa hata JPMa alipowaondoa hawa wa sasa aliwaweka wale alionao na sauti juu yao. Aliondoa kundi moja la wapigaji akaja na kundi jingine lenye kufanya uchafu ule ule lakini hakukuwa na uwazi wa vyombo vya habari wa kuweza kuuanika.

Hivyo jamii haijatendewa haki kwani inafahamu uchafu wote wa watendaji wa zamani wa JK lakini haifahamu uchafu wa wale waliokuwa ni wa JPM. Hayati hakuwa msafi kama tunavyojaribu kujulishwa kwenye media, la hasha. Uchafu wa watu wa JK unatokana na maamuzi yake na utayari wa kuweka kila kitu wazi.

Hivyo ni matarajio ya wadau wa sekta ya umeme kuwaona watendaji waliokuwa wachafu na bado ikaonekana wanafaa kupewa vyeo hivyo, wakiwa na uhuru na utendaji wenye ufanisi kuliko ile awamu ya kwanza walipochafuka na kuchafuliwa zaidi watu wakiaminiswa ni wachafu kumbe ni uchafu wa kisiasa unaopewa kipaumbele kuliko ule halisia.

Waitumie hii fursa ya pili waliyopewa na Mama Samia kwa kuwaonyesha wenye wasiwasi na utendaji kazi wao kwamba ni mawazo potofu kuamini kuwa wanatakiwa watiliwe shaka milele yote.

Kuna watu wamenuna na muda wote kosa dogo wapo tayari lionekane ni kubwa sana, hii ni kutokana na kuishi tofauti na matarajio yao. Ghafla tu wamelazimika kuwa wapole huku wakichekea machoni tu, wanalolishauri linaweza kuonekana ni la kweli na la dhati ya moyoni kumbe linao mtego wa hatari ndani yake.

Wajumbe wapya wa bodi ya TANESCO, wapige kazi kadri wawezavyo pasipo kujaziwa mabegani zile shauku na mioyo ya hasira kutoka kona mbalimbali za wanajamii.
Acha uongo kuwakingia hawa majambazi wanaoletwa tanesco. Enzi za magufuli watu waliona huduma bora kwa hivyo usijidai kusema wateule wake walikua wapigaji. Tunachoona sasa ni wazalendo wenye Phd wakiondolewa na kuwekwa wenye ujuzi na uzoefu wa kupiga hela na mali ya umma.
 
Acha uongo kuwakingia hawa majambazi wanaoletwa tanesco. Enzi za magufuli watu waliona huduma bora kwa hivyo usijidai kusema wateule wake walikua wapigaji. Tunachoona sasa ni wazalendo wenye Phd wakiondolewa na kuwekwa wenye ujuzi na uzoefu wa kupiga hela na mali ya umma.
Yule yule muumini mwingine wa JPM mwenye kuishi kwa maumivu ya moyoni.
 
Watu hawalalamiki bila sababu. Na hawawezi kusema ndio kwa kila jambo.

Kusema watu wa magu walikuwa wachafu ni kutaka kuipa uhalali hoja yako. Kila mtu anajua JPM hakushindwa kumtumbua mtu yeyote aliyezingua na kumchana hadharani, labda asijue.

Ndio serikali ya pekee iliyomudu kusimamia viongozi bila aibu wala kuogopana.
Ulikua unajua chochote kuhusu serikali au hadi uambiwe
Yaani mtu azuie uhuru ili atawale gizan ndio aonekane bora
Kiongozi bora ni tule anayeruhusu changamoto na kushinda sio anaeogopa changamoto
Ishu ndoto ya trillion 1.5 nusu afungie vyombo vyote vya habari
 
Back
Top Bottom