Makamishna wastaafu wa Polisi wataka jamii iwatumie kwa ushauri, pia wako tayari kutangaza utalii

Ushauri wa kusingizia watu kesi na kupokea rushwa huo hatuutaki.

Pambaneni na hali zenu.

Kova alipomsingizia yule mkenya kuwa kamteka Dr. Ulimboka alijiona mjanja sana.

Leo hii hata mia mbovu hana.

KARMA!
 
Makamishna wastaafu wa jeshi la polisi wamesema kupitia umoja wao wako tayari kuitumikia jamii kwa kutoa ushauri na kutumia elimu yao kuisaidia jamii.

Kamishna mstaafu Mohamed Mpinga amesema jamii isisite kuwaendea kwa ushauri popote walipo.

Naye kamishna mstaafu Jamal Rwambo ameiomba serikali iwatumie katika kuutangaza utalii wa nchi yetu.

Umoja wa makamishna wastaafu wa jeshi la polisi ulitembelea familia ya hayati Moringe Sokoine na kuzuru kaburi lake.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Hata yule wa ngunguli naye yumo?
 
Mnoooo . Watulie ni wakati wa kuisogelea foleni ya kuhesabiwa.

Hapo ndio napompendea Mungu, fanya ubabe , dhulma na uonevu lakini muda utafika utasinyaa na kuzeeka nguvu zitaisha. Vyeo na mamlaka vitakaliwa na wengine wale waliokuwa wanyonge na watu wa kawaida ambao walikuaa hawaruhusiwi na ma-ps kumfikia mwenye mamlaka ndio watarudi kuwa rafiki na jirani wa kweli.

Wenye mamlaka wa wakati huo huja msibani kusaini kitabu na pole ya vijipesa na kuwahi kuondoka wakisema wanamajukumu mengi na misiba huachiwa wasio na lolote na ndio wanamsitiri marehemu aliyekuwa na kibri kwa hao wanyonge.

Hili ni fumbo kubwa sana la Imani.

Watulie hao makamishna

Katika watu ambao huwa wanajisahau kuwa kuna kesho ni Polisi. Utukufu wa duniani unawapa kiburi kiasi ambacho huwa wanasahau kuwa kuna adhabu ya kaburi!
 
Ushauri wa kusingizia watu kesi na kupokea rushwa huo hatuutaki.

Pambaneni na hali zenu.

Kova alipomsingizia yule mkenya kuwa kamteka Dr. Ulimboka alijiona mjanja sana.

Leo hii hata mia mbovu hana.

KARMA!

Kova kova alimkimbia rashidi Gwajima kwa aibu walipokutana supermarket baada ya kustaafu upolisi.Rashid alimshika bega akamwambia kova unanikumbuka?
Huwa wanadhani watastaafu na upolisi wao.
 
Jeshi la Polisi la Tanzania, limejaa dhulma, ubabe, uonevu na kiburi. Jeshi la Polisi, wakati wa uchaguzi hutumika kwenye mambo maovu kama kuwalinda CCM wanapoiba kura.

Hawa wanaosema tuwaendee kuomba ushauri, wanataka tukaombe ushauri upi? Ushauri wa uovu? Hawa ndio huua mahabusu kwa kipigo, na kisha hutoa taarifa za uwongo kuhusu vifo vilivyotokea kwenye nyumba za polisi za kutesea. Tukaombe ushauri gani kwao? Ushauri wa kuua watu na kisha kuihadaa jamii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wanataka nawashauri waanzishe timu ya mpira waingiewkucheza ligi kuu maana group la WhatsApp najua wanalo tayari.
 
Mnoooo . Watulie ni wakati wa kuisogelea foleni ya kuhesabiwa.

Hapo ndio napompendea Mungu, fanya ubabe , dhulma na uonevu lakini muda utafika utasinyaa na kuzeeka nguvu zitaisha. Vyeo na mamlaka vitakaliwa na wengine wale waliokuwa wanyonge na watu wa kawaida ambao walikuaa hawaruhusiwi na ma-ps kumfikia mwenye mamlaka ndio watarudi kuwa rafiki na jirani wa kweli.

Wenye mamlaka wa wakati huo huja msibani kusaini kitabu na pole ya vijipesa na kuwahi kuondoka wakisema wanamajukumu mengi na misiba huachiwa wasio na lolote na ndio wanamsitiri marehemu aliyekuwa na kibri kwa hao wanyonge.

Hili ni fumbo kubwa sana la Imani.

Watulie hao makamishna
Aisee!

Mkuu umeandika maneno mazito sana, uzito wake usiomithilika. Umeandika kama mwanazuoni. Mauti ni mazito.
 
Makamishna wastaafu wa jeshi la polisi wamesema kupitia umoja wao wako tayari kuitumikia jamii kwa kutoa ushauri na kutumia elimu yao kuisaidia jamii.

Kamishna mstaafu Mohamed Mpinga amesema jamii isisite kuwaendea kwa ushauri popote walipo.

Naye kamishna mstaafu Jamal Rwambo ameiomba serikali iwatumie katika kuutangaza utalii wa nchi yetu.

Umoja wa makamishna wastaafu wa jeshi la polisi ulitembelea familia ya hayati Moringe Sokoine na kuzuru kaburi lake.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Katika huo umoja wa makamishna na Zombe yumo?
 
Back
Top Bottom