Baada ya malalamiko makubwa ya wananchi kutokana na kupanda kwa gharama za matumizi ya virushi vya simu,hali iliyopelekea serikali kuingilia Kati na kutoa tamko la kusitisha gharama hizo mpya zilizopandishwa ,na kuwataka wahusika wa mitandao ya simu kurejesha gharama za awali kipindi ambacho watakuwa wanafanya marekebisho ya gharama mpya ambazo zitakuwa elekezi kwa mujibu wa serikali.
Tatizo kubwa linaloendelea hadi Sasa ni kwamba gharama za vifurushi bado zipo vilevile licha ya tamko kutolewa na mkuu wa nchi.
Bado virushi vipo bei ghali na bado wananchi wanalalamika licha ya taasisi ya mawasiliano kupata mkurugenzi mpya ambaye tulitarajia aanze na ufumbuzi wa suala hili.
Matumaini ya wananchi bado yapo katika serikali.
Na tumeona TCRA mpya imeanza kazi zake kwa kutoa matamko na maagizo mbalimbali kuhusu kutahadharisha watu kuendelea kuchukua tahadhari na kutokukingiuka Sheria ya mtandao.
Ila kuhusu suala la virushi bado hatuja sikia tamko lolote hadi sasa
Je tutarajie TCRA mpya itatoa tamko kuhusu utekelezaji wa kubadilisha gharama za bei za vifurushi?
Tunakuomba Mh.Jabir kuwe mkurugenzi wa TCRA wewe ni mchamungu na muadilifu Sana utendaji wako umetukuka sisi wanyonge tunahitaji gharama ya virushi ishuke tunaumia Sana .
View attachment 1751468