Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu sijaelewa hiyo Avatar yako inataka tuchukue muda wetu kutazama movie au hiyo picha
Oohh SawaView attachment 1745905hua napendelea sana movie ndio mana nikaweka avatar iyo mkuu
In mwenda zake voice chapa kazi mtanzaniaChapeni kazi
Baada ya malalamiko makubwa ya wananchi kutokana na kupanda kwa gharama za matumizi ya virushi vya simu,hali iliyopelekea serikali kuingilia Kati na kutoa tamko la kusitisha gharama hizo mpya zilizopandishwa ,na kuwataka wahusika wa mitandao ya simu kurejesha gharama za awali kipindi ambacho watakuwa wanafanya marekebisho ya gharama mpya ambazo zitakuwa elekezi kwa mujibu wa serikali.
Tatizo kubwa linaloendelea hadi Sasa ni kwamba gharama za vifurushi bado zipo vilevile licha ya tamko kutolewa na mkuu wa nchi.
Bado virushi vipo bei ghali na bado wananchi wanalalamika licha ya taasisi ya mawasiliano kupata mkurugenzi mpya ambaye tulitarajia aanze na ufumbuzi wa suala hili.
Matumaini ya wananchi bado yapo katika serikali.
Na tumeona TCRA mpya imeanza kazi zake kwa kutoa matamko na maagizo mbalimbali kuhusu kutahadharisha watu kuendelea kuchukua tahadhari na kutokukingiuka Sheria ya mtandao.
Ila kuhusu suala la virushi bado hatuja sikia tamko lolote hadi sasa
Je tutarajie TCRA mpya itatoa tamko kuhusu utekelezaji wa kubadilisha gharama za bei za vifurushi?
Tunakuomba Mh.Jabir kuwe mkurugenzi wa TCRA wewe ni mchamungu na muadilifu Sana utendaji wako umetukuka sisi wanyonge tunahitaji gharama ya virushi ishuke tunaumia Sana .
View attachment 1751468
Sasa kama iko kwa top ten ndo isisikilize amri toka juu?Kwa ninavyofahamu Vodacom Tanzania ni moja kati ya top 10 ya walipa kodi.
Rostam kazini.Hawa watu wanaojiita vodacom inaonekana wana nguvu na jeuri kuliko serikali.
Kwa inavyoonekana, kuna mizizi mirefu sana ya watu wasiojulikana na wenye vyeo huko ambao wameshikilia roho na uchumi wa vodacom.
Rais wa nchi alishasema, vifurushi vishuke, lakini agizo lake limepuuzwa na kudharauliwa.
Inawezekanaje agizo la Rais na Amiri jeshi mkuu wa nchi likapuuzwa? Haya ni matusi mazito.
Hivi angekuwa ni Jemedari Chuma Magufuli ndio ametoa hilo agizo, hawa vinyangarika wa TCRA na Voda wangekuwa bado wanajivuta kwa kiburi namna hii?
Kumbe wakati mwingine udhaifu ni wa kujitakia?
Wanataka tuamini nini? Kwamba Rais samia ni mwepesi sana ama? Halafu?
Kwanini hawataki kushusha vifurushi? Wanafikiri tunaokota hela mchangani?
Hii njama ya utapeli wa vifurushi inahitaji mpaka Yesu ashuke mbinguni au vipi?
Hivi hii nchi ina serikali?