Makamu Mwenyekiti CHADEMA, comrade Tundu Lissu mbona upo kimya kwenye maridhiano?

Uchaguzi serikali za mitaa sio mwakani?, Au nabugi?.
Halafu 2025 uchaguzi mkuu,, hatuwezi kwenda na vyote kwa pamoja,, vilevile katiba haiwezi kupita leo, kesho ianze kazi,, bado sheria zitatakiwa kutungwa kuendana na katiba mpya,, itachukua at least two years minimum
Mkuu Cha msingi tume huru hayo mengine yanaweza subiri. Ukifika uchaguzi wamesema task force kwamba kunaweza fanyika minimum reforms kwenye sheria za uchaguzi Ili walau kupisha kura ya maoni ya katiba mpya na uchaguzi mkuu yote yanawezekana. Hata Kenya wakibadili katiba na uchaguzi ukafanyika ndani ya siku kama 90 hawakusubiri sheria zote zibadilishwe.
 
Wanaosema kwamba katazo lilikuwa batili ni kwa hoja ya kwamba hiyo mikutano ya kisiasa ni haki kikatiba, ndio maana wanasema katazo halikuwa halali ndio sababu ya kumtaka Samia aondoe hilo katazo.
Katiba wapi imesema mikutano ya siasa ni halali au sio halali? Katiba imetamka tu kuwa watu Wana haki na uhuru wa kujieleza ila sheria ya vyama imespecify haki hiyo Iko limited kwa vyama vya siasa majimbo husika tu. So katazo lilikua haramu ila baada ya sheria ya vyama vya siasa ya 2006 kufanyiwa marekebisho na wabunge nadhani 2019 Ile ndio ikahalalisha zuio la mikutano ya kisiasa nje ya majimbo ya wabunge au nje ya muda wa kampeni.

So kuondolewa kwa zuio lazma litaenda sambamba na kufanywa amendments ya kifungu kilichoweka limit kwa vyama kufanya mikutano ya hadhara more so nje ya majimbo ya wabunge wake.
 
Kwahiyo issue ilikuwa kufanyika mabadiliko ya sheria au Rais kuondoa hilo katazo?
 
Wewe unataka sera gani?
Mtaji wa kura umeliwa[emoji23] kuna watu wanafaidika na shari. Sasa kilichobaki wajipange na sera. Kitu ambacho hawana maana tumechoka kila siku kuwaskia mkiongelea kasoro tunazozijua. Mnaacha kusema mtafanya nini mnakazana kutafuta huruma ya wananchi.
 
Kwahiyo issue ilikuwa kufanyika mabadiliko ya sheria au Rais kuondoa hilo katazo?
Watu wanadai Mbowe hakupaswa kushukuru kwa katazo haramu kuondolewa.

Wanasema sababu katazo HALIKUWEPO maana halipo kisheria Wala kikatiba.

Ndio Mimi nasema katazo lilikuwepo kisheria maana baada ya JPM kupiga marufuku mikutano akaambiwa ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa kwa mabadiliko ya 2006.

So alichofanya JPM ni kupeleka amendments bungeni Ili zuio lake hewa lipate uhalali wa kisheria.

Kwahiyo ZUIO kisheria lilikuwepo hivyo likageuka ZUIO HALALI.

So Rais kupindua zuio liliopo kisheria ni suala la kishujaa na Mbowe alikua sawa kumsifia maana mwingine angesema analiachia bunge lifanye kazi yake!!
 
Kwahiyo rais karuhusu kufanyika jambo lilokinyume cha sheria?
 
Sio kinyume ila kaongeza wigo tu wa application ya sheria Ina maana hapo itafanyika ammendments ya sheria husika hata kwa hati ya dharura Ili iwe rasmi kisheria.
 
Magufuli alitoa katazo lisilo la kisheria na baadaye ndio likawekewa sheria na Samia nae kaja katoa ruhusa ya kufanyika jambo ambalo ni kinyume cha sheria kisha baadaye ndio hiyo ruhusa itawekwa kisheria.

Inatafakarisha sana.
 
Hakuna sera? Ilani ya 2020 ulisoma?
Sera ya ugatuzi/majimbo
Sera ya soko huria? Yaani miradi iendeshwe kwa PPP kupunguza mzigo na ufisadi serikalini.
Katiba mpya Ili kuleta uwajibikaji
Sera ya bima ya afya kwa wote
Uchumi wa kidijitali
Masoko ya usiku n.k

Sera hazijawahi kuisha kwenye chama chochote duniani maana changamoto za wanadamu zinabadilika Kila siku.
Hiyo ya Majimbo wanawadanganya wanachama wao. Hilo ni suala la kikatiba sio la kukimbilia.
 
Back
Top Bottom