KWELI Makamu wa Rais akishika nafasi ya Rais kwa muda wa miaka 3 au zaidi ataruhusiwa kugombea kipindi kimoja tu

KWELI Makamu wa Rais akishika nafasi ya Rais kwa muda wa miaka 3 au zaidi ataruhusiwa kugombea kipindi kimoja tu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimeona mjadala kuhusu mihula anayoruhusiwa kugombea makamu aliyeshika madaraka ya Urais kutokana na kuchukua kiti katikati ya muhula baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kuendelea aidha kwa kufariki akiwa madarakani, kujiudhuru au sababu za kiafya.

Mjadala umechagizwa na kauli ya Sophia Mjema aliyesema Rais Samia ni hadi 2035, huku wanaharakati wakipinga vikali kuwa hana sifa ya kugombea mihula miwili tena.

Je, ukweli ni upi?

1696993958659.jpeg
 
Tunachokijua
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa haki raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 40, na atakayekuwa karidhiwa na chama chake cha siasa kushika nafasi ya kugombea na kuwa Rais wa Jamhruri ya Tanzania.

1696998174915-png.2778464

Hata ivyo katiba inaeleza kupitia ibara ya 40(1) mtu aliyewahi kuwa Rais anaweza kuchaguliwa tena ila hataruhusiwa kuchaguliwa zaidi ya mihula miwili ya Urais, (Muhula mmoja ni kipindi cha miaka 5).

1696998598282-png.2778465

Je, kiti cha Urais kikibaki wazi katiba inasemaje?
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 37(3) ibara ndogo ya (2) inataja sababu mbalimbali za kufanya kiti cha Rais kihesabike kuwa kiko wazi kama, Rais kujiuzulu, kufariki, kupata tatizo la kiafya na kushindwa kumudu madaraka ikiwemo afya ya akili basi Makamu wa Raisi, Spika wa bunge au Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufani anaweza kushika nafasi hiyo.

Ibara ya 37(5) inaeleza Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.

Mwaka 2021, Machi 17, nchi yetu ya Tanzania ilikumbwa na msiba mzito wa kufiwa na Rais aliyekuwa madaraka Hayati, John Pombe Joseph Magufuli, na kusababisha kiti cha Urais kubaki wazi na ivyo kujazwa na aliyekuwa makamu wake, ambaye ni Samia Suluhu Hassan kama katiba inavyotaja kwenye ibara 37(5).

Rais Samia aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania tarehe 19, Machi 2021 akimalizia kipindi cha muhula wa pili kilichoachwa wazi na Hayati Magufuli.

Je, katiba inasemaje kuhusu muda wa Makamu wa Rais kushika kiti cha Urais baada ya kiti cha Urais kubaki wazi?

Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaeleza, Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais kwa sababu zilizoelezwa kikatiba, Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40 (ib.37(5)).

Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ib.37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka 3 ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara 2, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka 3 au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara 1 tu (ib.40(4))

1697003850457-png.2778466

Kwa mantiki hiyo, kauli inayodaiwa kuwa ya Sophia Mjema kwamba Rais Samia ni mpaka 2035, inakwenda kinyume na katiba kwani Rais Samia aliingia madarakani tar 19, Machi 2021 na kufanya kuwa na kipindi cha miaka 4 na miezi 8 kumalizika awamu ya 5 ya utawala wa Rais John Magufuli (aliyeapishwa 05.11.2020)ya kukamilisha miaka 5 ya muhula wa pili iliyobaki wakati akichukua kiti cha Urais kutokana na aliyekuwa Rais kufariki.

Kwa mujibu wa Katiba (ib 40(4)) Rais Samia anaruhusiwa kugombea kiti cha Urais Kwa muhula 1 tu wa kipindi cha miaka 5.
Mie nimesoma lkn kama sijaelewq vile,kwa maana hiyo samia ataruhusiwa kuwa mgombea 2025 na katiba?. Kama jibu ni ndio,basi taifa hili bado lina kazi kubwa,na tutafika tumechoka mno.
 
Pamoja na kwamba katiba iliyopo ina mapungufu mengi ila kuna mambo yako wazi na yanaeleweka vizuri.Hayo mengine yanaropokwa kwasababu ya uwepo wa chawa wanaojali matumbo yao badala yakuzingatia weledi.
 
Naona Wananchi tunaandaliwa Kisaikolojia kwamba aliyepo ataendelea hadi 2030 huko 🙌
 
Asije kurudia "Nilisema katiba ni kijitabu tu..."
 
Miongoni mwa Awamu zilizopita, Awamu hii ya Tano ndio iliyojiwekea Historia kubwa Nchini.

Hakika hili litakuwa ni somo la Siasa(case study)huko mbeleni.

Mfano:Kuna nguvu kubwa iliyotumika, imetumika kuhadaa Umma kushusu mihula. Ni dhahiri huu ni muhula wa Awamu ya Tano.

Sababu kubwa ni kufunika fikra za kwamba "Tunaweza" kama Taifa kuwa na misimamo thabiti dhidi ya Ukoloni Mamboleo, Usimamizi wa Rasilimali zetu Uchumi wetu and so forth, bila ya kuwa tegemezi wa Misaada na Mikopo yenye masharti magumu.

Sababu zingine ni vita za Kiuchumi ambazo baadhi ya waliopo madarakani wameamua kutelekeza kwa visingizo vilivyotokana na kampeni kubwa kuwahi kutokea katika karne hii, Kampeni za kinafiki, Kampeni hasi za kumchafua Raisi alikuwepo madarakani.

Maua yamfikie aliyeleta mada hii Jamii Check, kwani, karibia tutawajua masaliti, manafiki na wasiopenda Nchi yetu Tanzania
 
Hamtakiwi kuwa na shaka maana hata yule alitaka aongezewe ila kafa
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
 
Kama hivyo aruhusu wapinzani wane kina Kipara waakapambane kwenye kura za maoni kule CCM- NEC
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Matusi mengi huwa mnajitakia tu....... Haya mbwa wewe umeandika nini hapa sasa
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Elimu elimu elimu. Wazazi tupeleke watoto shule.
 
😂 katiba haisemi hivyo samia amerithi miaka 3 ya rais aliepita hivyo anamuhula mmoja tu wakugombea angekuwa amerithi miaka 2 hapo ndo angekuwa anamihula 2 yakugombea.
 
Hii ina maana fomu zitatolewa kwa wote kama utaratibu ulivyo mnapogombea awamu ya kwanza. Si ndio hivyo?
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Yani Mwigulu hadi 2035? Hapana asee hatutakubali. 2035 mbali sana.
 
Back
Top Bottom