KWELI Makamu wa Rais akishika nafasi ya Rais kwa muda wa miaka 3 au zaidi ataruhusiwa kugombea kipindi kimoja tu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimeona mjadala kuhusu mihula anayoruhusiwa kugombea makamu aliyeshika madaraka ya Urais kutokana na kuchukua kiti katikati ya muhula baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kuendelea aidha kwa kufariki akiwa madarakani, kujiudhuru au sababu za kiafya.

Mjadala umechagizwa na kauli ya Sophia Mjema aliyesema Rais Samia ni hadi 2035, huku wanaharakati wakipinga vikali kuwa hana sifa ya kugombea mihula miwili tena.

Je, ukweli ni upi?

1696993958659.jpeg
 
Tunachokijua
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa haki raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 40, na atakayekuwa karidhiwa na chama chake cha siasa kushika nafasi ya kugombea na kuwa Rais wa Jamhruri ya Tanzania.

1696998174915-png.2778464

Hata ivyo katiba inaeleza kupitia ibara ya 40(1) mtu aliyewahi kuwa Rais anaweza kuchaguliwa tena ila hataruhusiwa kuchaguliwa zaidi ya mihula miwili ya Urais, (Muhula mmoja ni kipindi cha miaka 5).

1696998598282-png.2778465

Je, kiti cha Urais kikibaki wazi katiba inasemaje?
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 37(3) ibara ndogo ya (2) inataja sababu mbalimbali za kufanya kiti cha Rais kihesabike kuwa kiko wazi kama, Rais kujiuzulu, kufariki, kupata tatizo la kiafya na kushindwa kumudu madaraka ikiwemo afya ya akili basi Makamu wa Raisi, Spika wa bunge au Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufani anaweza kushika nafasi hiyo.

Ibara ya 37(5) inaeleza Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.

Mwaka 2021, Machi 17, nchi yetu ya Tanzania ilikumbwa na msiba mzito wa kufiwa na Rais aliyekuwa madaraka Hayati, John Pombe Joseph Magufuli, na kusababisha kiti cha Urais kubaki wazi na ivyo kujazwa na aliyekuwa makamu wake, ambaye ni Samia Suluhu Hassan kama katiba inavyotaja kwenye ibara 37(5).

Rais Samia aliapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania tarehe 19, Machi 2021 akimalizia kipindi cha muhula wa pili kilichoachwa wazi na Hayati Magufuli.

Je, katiba inasemaje kuhusu muda wa Makamu wa Rais kushika kiti cha Urais baada ya kiti cha Urais kubaki wazi?

Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaeleza, Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais kwa sababu zilizoelezwa kikatiba, Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40 (ib.37(5)).

Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ib.37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka 3 ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara 2, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka 3 au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara 1 tu (ib.40(4))

1697003850457-png.2778466

Kwa mantiki hiyo, kauli inayodaiwa kuwa ya Sophia Mjema kwamba Rais Samia ni mpaka 2035, inakwenda kinyume na katiba kwani Rais Samia aliingia madarakani tar 19, Machi 2021 na kufanya kuwa na kipindi cha miaka 4 na miezi 8 kumalizika awamu ya 5 ya utawala wa Rais John Magufuli (aliyeapishwa 05.11.2020)ya kukamilisha miaka 5 ya muhula wa pili iliyobaki wakati akichukua kiti cha Urais kutokana na aliyekuwa Rais kufariki.

Kwa mujibu wa Katiba (ib 40(4)) Rais Samia anaruhusiwa kugombea kiti cha Urais Kwa muhula 1 tu wa kipindi cha miaka 5.
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Wewe akili huna! Magufuli alikuwa awamu ya tano! Kama ni hivyo SSH uongozi wake angeuhita "awamu" ya tano. Sasa anauihita "awamu ya sita" kikatiba huwezi kuongoza taifa hili zaidi ya miaka 10. RIP JKN!
 
Katiba hairuhusu kwa sasa anaruhusiwa kugombea 2025 tu, ingekua magufuli kafa 2023 hapo sawa angeruhusiwa kugombea 2025-30 na 2030-35
 
Umekurupuka kijana jipange tena.... Kabakisha Round ya 2 ya Utawala ila natamani tumpe miaka mingine kama 10 hivi ikiwezekana ili atuamshe akili watanganyika.
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Ingekuwa hivyo hii isingeitwa awamu ya 6.

Awamu ni Rais ,hakunaga Marais 2 ndani ya awamu 1.

Mwisho Hilo lingewezekana ikiwa Magu angekufa ikasalia chini ya miaka 3,ila Kwa kuwa ni miaka 4.5 ,inahesanika awamu kamili hivyo atamalizia awamu ya pili 2026-2030.
 
CCM Ilisigina Katiba Kwa Kukataa Eti Awamu Ya Tano Iliisha Alipokufa Jiwe
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Acha kwanza amalizie hii deiwaka. Tuhakikishe hakuna wizi wa kura tuone kama atapata urais
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Kama mambo hayajaharibika mbeleni by JK.
 
Ingekuwa hivyo hii isingeitwa awamu ya 6.

Awamu ni Rais ,hakunaga Marais 2 ndani ya awamu 1.

Mwisho Hilo lingewezekana ikiwa Magu angekufa ikasalia chini ya miaka 3,ila Kwa kuwa ni miaka 4.5 ,inahesanika awamu kamili hivyo atamalizia awamu ya pili 2026-2030.
Hilo ni suala la kikatiba ambapo tutaomba mahakama ya rufaa ifafanue
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
20240919_080623.jpg
 
Kwani ni lazima kua akimalizia muda wa mpito ni yeye anatakiwa kugombea au kuteuliwa Tena kua raisi!!? Yaani hapo ccm hawatoi form za uraisi kwa watu wengine kugombea!!? Maana ya muda wa mpito kuisha inabidi taratibu za ugombea uraisi zirudi Tena zipigwe kura apatikane atakae gombea uraisi kushindana na vyama vingine ila sidhani kua ni lazima akimalizia muda wa mpito kua hakuna mwingine wa kugombea zaidi ya yeye, ni nawazo yangu tu
 
Wewe akili huna! Magufuli alikuwa awamu ya tano! Kama ni hivyo SSH uongozi wake angeuhita "awamu" ya tano. Sasa anauihita "awamu ya sita" kikatiba huwezi kuongoza taifa hili zaidi ya miaka 10. RIP JKN!
Nilipoona hapo RIP JKN NKahisi JK Kakata kamba. Ila nkakumbukwa wazuri hawafi.
 
Ukweli ambao watu hampendi kuusikia ni huo,
Hii miaka ni ya mpito, ambayo ni ya Rais magufuli,
Rais Samia akigombea 2025 ataongoza miaka mitano, hiyo ikiisha ndio atatakiwa agombee tena miaka mingine 5 yaani 2030 agombee tena ndio atimize miaka yake 10,
Hii anamalizia sera na maono ya magufuli, ili atuvushe baada ya kifo cha marehemu magufuli,
Huo ndio ukweli ambao mnatakiwa muishi nao wala msiogope,
Iyo inafahamika,samia anamaliza 2035.
 
😂 katiba haisemi hivyo samia amerithi miaka 3 ya rais aliepita hivyo anamuhula mmoja tu wakugombea angekuwa amerithi miaka 2 hapo ndo angekuwa anamihula 2 yakugombea.
Hapana,anamalizia awamu ya magufuli,2025 ndo anaanza awamu yake hadi 2035
 
Back
Top Bottom