Ni habari ya kushitua kwa kiongozi wa juu kukiri kuwepo kwa mapenzi ya jinsia moja. Maana yake kuna tatizo hilo miongoni mwa jamii na wanashangaa mahusiano hayo. Niwaombe msimuingize mama mkenge naye akataoa kauli kisha ikahamia bungeni kutungiwa sheria kuwatia korokoroni wapenzi hao.
Tunahofia nchi yetu isije ikawekewa vikwazo vya uchumi kuwa inakadamiza haki za binadamu kwa kuingilia faragha zao. Habari za mashoga nimeanza kuzisoma miaka 20 ishirini iliyopita, tena mashoga yakijiremba kama wanawake na kushiriki shughuli za burudani hadharani hasa muziki wa taarabu na kitchen part. Kulikuwa na mashoga maarufu yale majina yao yalianza na title aunt ...
Ina maana serikali haikuona wapenzi hao miaka hiyo? Sasa nini kinawafanya washangae uwepo wa mashoga wakati wapo muda mrefu? Yaani hapa wanaukoleza badala ya kuufifisha. Hebu wasitake kukwaruzana na marekani na washirika wake wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja. Mambo mengine unasukumiwa uingie kingi ili msimamo wako ujulikane, ni mtego wa kuepukwa.