Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Wabunge wa upande wa pili (CHADEMA, ACT na CUF) ni vema mkajiunga CCM ili kwa pamoja tujenge nchi

Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Wabunge wa upande wa pili (CHADEMA, ACT na CUF) ni vema mkajiunga CCM ili kwa pamoja tujenge nchi

Huyu kaanza vibaya anakuwa na mawazo mfu kama mungu yule asiyeishi!
 
Kwani wapinzani walifanikiwa kupata wabunge!!!?

Mi nachojua bungeni ni Ccm tu.
Kujenga nchi mpaka uwe Mbunge? Kwani hawawezi teuliwa sehemu nyingine kama Mama Mngwira, DC Nanyumbu, DC Tunduru n.k
 
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema wabunge wa upande wa pili akimaanisha Chadema ACT wazalendo na CUF ni vema wakajiunga na CCM ili kwa pamoja tuijenge mama Tanzania.

Dkt. Mpango amewashauri wabunge hao kwamba kama kuna ugumu wa wao kuhamia CCM basi wawe hata wanajenga hoja zenye kuleta maslahi ya kimaendeleo kwa mama Tanzania na siyo vinginevyo.

Chanzo: TBC.

Maendeleo hayana vyama!
Dr Mpango kama wewe ni mcha Mungu kweli tuambie ndani ya roho yako kama uliopita Ubunge wako kihalali na Mungu anakuona kwenye kaulia yako hii.
 
Usisahau mkuu, CCM ni CHAMA CHA MAZEZETA
Lakini ndio wanaokuongoza hao.. Ili ujue uzezeta wao nenda ofisi yoyote ya CCM atamke hayo maneno uone utaingizwa nini kwenye shimo lako linalotoa uchafu
 
Kwa mtazamo huu Dr. Mpango anapotea. Propoganda kama hizi awaachie akina Polepole. Yeye kama msomi anatakiwa kujua kuwa si lazima mtu uwe CCM ndo ujenge taifa. Mtazamo mpotofu kama huu pia alikwa nao marehemu Magufuli. On that point Dr Mpango umenifadhaisha!
Yule hafai anakiburi sn
 
Kwani wapinzani walifanikiwa kupata wabunge!!!?

Mi nachojua bungeni ni Ccm tu.
Aliumwa sana mpango karibia azikwe, akufe kabla ya Magufuli kufa.
Akili yake imeshasahau au anafikiri bado yupo kwenye bunge la Magufuli, la kununua wapinzani.

Tuendelee kumshangaa tu, hakuna namna.
 
1617176576694.png
 
Huyu ameshafeli kabla ya kuanza,nadhani corona imemuathiri vibaya sana
 
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema wabunge wa upande wa pili akimaanisha Chadema ACT wazalendo na CUF ni vema wakajiunga na CCM ili kwa pamoja tuijenge mama Tanzania.

Dkt. Mpango amewashauri wabunge hao kwamba kama kuna ugumu wa wao kuhamia CCM basi wawe hata wanajenga hoja zenye kuleta maslahi ya kimaendeleo kwa mama Tanzania na siyo vinginevyo.

Chanzo: TBC.

Maendeleo hayana vyama!
MATAGA mmepoteana.
 
Huyu naye, mbona anaongea sana, tangu lini makamu wa Rais akawa mtu wa matamko. Hakika Magufuli kaharibu nchi sana. Itachukua miaka mingine 5-10 kuondoa kichwani mentality za ajabu.
 
Kwa hiyo hao ndio wanakwamisha maendeleo? Anataka kuanza vibaya. aache mawenge mawenge ya Jiwe. yeye afanye kazi na wote. Heshimuni kanuni ya dunia kwamba daima kuna nguvu mbili zinazovutana na ndizo hutufanya tutembee, tusonge mbele.

Yeye ni msomi wa uchumi, anajua kabisa kwamba maendeleo yoyote ni matokeo ya ushindani. Kwenye mji tukiwa na duka moja tu hakuna maendeleo. Tutapanga foleni hadi kuchelewa kazi za nyumbani, shambani na ofisini.

Hivi ni utafiti gani uliowahi kufanywa ukaonyesha kwamba nchi ya chama kimoja hupinga hatua kubwa ya maendeleo kuliko nchi ya mfumo wa vyama vingi? Mbona mnakuwa wasomi halafu bado ni wajinga?
Makamu wa Rais mteule jana amekiri kuwa nchi yetu ina maskini wa kutupwa takriban milioni 14. Hii ni baada ya chama chake kushika usukani toka tupate uhuru bila kupokezana na chama kingine. Miaka 60 ya bajeti zao kupita bila kupingwa, matokeo yake ni asilimia 20 ya raia wa nchi yetu wanaishi duni ya umaskini uliopitiliza! Na katika miaka hiyo, yeye alikuwa ndie msimamizi na mshauri Mkuu wa Rais kuhusu masuala ya uchumi kwa miaka 6 ( 10% ya miaka ya uhuru wetu). Inasikitisha sana.

Amandla...
 
Ni ujinga kufikiri kuwa maendeleo ya nchi hii yanakwamishwa na wapinzani. Ni ujinga wa kutosha tena sana! Nchi za Marekani, Uingereza, Ujerumani ni nchi tajiri na zina vyama vingi. Mbona hawalalamiki kukwamishwa na mfumo wa vyama vingi?

Mpango akitaka afanye kazi nzuri aache kuwaona wapinzani kuwa ni maadui. Vinginevyo atachekwa hata akiwa anapumua kwa msaada wa oxygen
 
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema wabunge wa upande wa pili akimaanisha Chadema ACT wazalendo na CUF ni vema wakajiunga na CCM ili kwa pamoja tuijenge mama Tanzania.

Dkt. Mpango amewashauri wabunge hao kwamba kama kuna ugumu wa wao kuhamia CCM basi wawe hata wanajenga hoja zenye kuleta maslahi ya kimaendeleo kwa mama Tanzania na siyo vinginevyo.

Chanzo: TBC.

Maendeleo hayana vyama!
Mbona Chadema ina mbunge mmoja tu, anazungumzia nini wale COVID19 wa Ndugai!
 
Nimeona Lissu leo amejipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lisu ni makamu mwenyekiti hewa wa Chadema mnalipa mshahara wa bure.
Lisu hataki kuwa mnafiki. Anasumamia yale yote aliyoyasema hayati akiwa hai. Ulitaka kwa sababu hayati hatunaye tena amsifu ?
 
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema wabunge wa upande wa pili akimaanisha Chadema ACT wazalendo na CUF ni vema wakajiunga na CCM ili kwa pamoja tuijenge mama Tanzania.

Dkt. Mpango amewashauri wabunge hao kwamba kama kuna ugumu wa wao kuhamia CCM basi wawe hata wanajenga hoja zenye kuleta maslahi ya kimaendeleo kwa mama Tanzania na siyo vinginevyo.

Chanzo: TBC.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani Chadema wana wabunge? Ninavyojua mimi wale wa chadema 19 walifukuzwa, sasa sijui ni wa chama gani.
 
Lissu hanaga habari mpya afadhali hata Maria sarungi!

Tunataka ukweli na sio habari mpya. Maana hata Qoran na Bible hazina habari mpya, lakini ni vitabu tunavyoviamini. Nataka Lisu leo apige mule mule. Hata Mandela enzi za makuburu wa Afrika kusini, walikuwa wanasema anachafua nchi kwa yale aliyokuwa anayesema.
 
Back
Top Bottom