chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,865
- 29,608
Kwa kweliMchukueni kabisaa,zawadi ya Zanzibar tumewapa buree.
Kwa kweliMchukueni kabisaa,zawadi ya Zanzibar tumewapa buree.
Mbona Shoo kanukuu maneno ya Mwanasiasa Nyerere badala ya Biblia? Hapo tu kuchemka .Hana cha Kazi ya Mungu huyo ana Kazi ya chademaKanisa kwanza, serikali baadaye. Kanisa ni kazi ya Mungu, ilihali serikali ni kazi ya wanadamu. Serikali hazidimu, kanisa litadumu milele
Ujembe wake umesheheni mambo makuu man4:Makamu wa Rais Samia Suluhu aikisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Dkt. Isaac Kissiri Laiser mkoani Tabora leo.=====
Tathmini nzuri hiyoUjembe wake umesheheni mambo makuu man4:
1) Kusimamia haki (asishirikiane na wenye mamlaka kuipoka haki ya mnyonge)
2) Kuepuka kiburi cha madaraka
3) Kutunze utakatifu na usafi wa kanisa
4) Kutojipendekeza ili uheshimiwe
Atakapo maliza MagufuliMwaka gani?
Ccm sasa wanachungulia kama kumepoaOgopa sana watu aina hii!
![]()
Huyu Mama Samia hata kule Bunge la Katiba alijitahidi kuweka hekima mbele akiwa Naibu Spika.Huyu Mama commands respect from the public. Anaonekana ni mwenye hekima, siyo mtu wa kuzua taharuki, siyo mropokaji, ametulia akilini na moyoni. Na sijawahi kuwasikia watu wakimsema kwa lolote baya, iwe kwa wale wa wakereketwa wa CCM au wafurukutwa wa upinzani au wale wasioegemea kokote.
Tanzania would be better with her.
Huku akinukuu maneno ya Mwalimu Julius Nyerere, Askofu Shoo amesema, “pale kanisa litakaposimama na watu wenye mamlaka na kumsahau mnyonge hilo halistahili kuwa kanisa na wala hastahili kuwa mtumishi wa Mungu.”
Kuna vitu unajidanganya.Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
Hata mme wake nadhani ana enjoy the marriage, sio vipuuzi fulani vikipata hata ukuu wa wilaya ni shidaNampenda huyu bure.
Hana binti above 18?
Bila kuzingatia ukanda utakuwa huna hoja?Maoni ya askofu shoo wa kaskazini akimpa ushauri askofu mteule Laizer wa kutoka kaskazini pia huku akinukuu maneno ya Mwanasiasa Nyerere badala ya maneno ya Mungu yaliyoko kwenye Biblia.Askofu Shoo joho lake avae tu gwanda la chadema juu avae hilo kofia la uaskofu itapendeza zaidi
Makamu wa Rais Samia Suluhu aikisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Dkt. Isaac Kissiri Laiser mkoani Tabora leo.
=====
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dk Frederick Shoo amemtaka askofu mteule, Isaac Laizer kusimama katika haki na asitawaliwe na kiburi cha madaraka.
Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Juni 10, 2018 katika ibada ya kumsimika askofu Laizer inayofanyika katika viwanja vya Kanisa la KKKT Magharibi Kati mkoani hapa.
Amesema asitokee mtu yeyote mwenye mamlaka akamrubuni na kujikuta anasahau kanisa na kumtaka atunze utakatifu na usafi wa kanisa na kufanya kazi kwa uaminifu.
Huku akinukuu maneno ya Mwalimu Julius Nyerere, Askofu Shoo amesema, “pale kanisa litakaposimama na watu wenye mamlaka na kumsahau mnyonge hilo halistahili kuwa kanisa na wala hastahili kuwa mtumishi wa Mungu.”
Amesema askofu Laizer anapaswa kuwa mnyenyekevu asitafute kuheshimiwa, kwa maelezo kuwa kama asipoheshimiwa na watu, basi ataheshimiwa na Mungu, “kheri uheshimiwa na Mungu kuliko mwanadamu.”
Amemtaka kutekeleza mambo matatu ambayo ni kutunza roho za watu, kumhudumia mwanadamu kiroho na kimwili pamoja na kutoa, kutetea haki na heshima ya mwanadamu hasa walio wanyonge na wanaoteseka.
Nimeona umempongeza kiutu uzima na kumnanga mwingine kwa akiliUongozi ni Busara na mama amefanikiwa kupewa Busara na Mola mwenyewe....mambo mengine ni asili ya mtu.